Kwimba imetekwa na chadema

Nipo hapa stand ya mabasi ngudu-kwimba,kuna mkutano wa chadema,unaöngozwa na Wenje,letisia nyerere,na mtoto wa mashishanga yule mkuu wa mkoa wa zaman wa mwanza,watu wanaipenda chadema hadi noma

Letisia Nyerere si alikwenda NCCR ama nimesahau?
 
huyo inabidi asirudi tena, akirudi tu wananchi waandamane na kumkataa mara moja
Mbunge wa hapa kwimba mh. Masoli (msambaza mafuta migodini),toka atanganzwe na DED(Mkurugenzi) wa hapa hajawaii onekana hapa kwimba-mwanza,juzi alipigiwa simu haje kwenye vikao na wananchi,akajibu yupo uarabuni kwenye biashara zake za mafuta,leo wamemshitaki kwa letisia nyerere,na Wenje
 
Mmmh Mch. naona utakuwa umesahau.

Kweli nimepitiwa hebu soma hapa!

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/90581-maelezo-juu-ya-leticia-musore-kuhamia-nccr-7.html

MWANANCHI
Monday, 22 November 2010 20:34

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chadema, Leticia Musori amehamia chama cha NCCR-Mageuzi huku akikiponda chama chake cha zamani kwa madai kuwa kimejaa udini, ukabila na ubinafsi. Musori amedai kuwa amechukua uamuzi huo baada ya kutofautiana na viongozi wa juu wa chama hicho, akiwemo mwenyekiti Freeman Mbowe, katibu mkuu Dk Willibrod Slaa na Tundu Lissu kuhusu uteuzi wa wabunge wa viti maalum, akisema kuwa baadhi ya watu wenye sifa walienguliwa.
Suala la viti maalum lilikuwa na utata mkubwa ndani ya Chadema kabla ya uchaguzi mkuu na kusababisha viongozi watofautiane, lakini mwishoni uongozi wa juu walikubaliana kumtafuta mtaalamu ambaye alitengeneza vigezo na sifa ambazo zilitumika kupata wabunge wa viti maalum, kikiwemo kigezo muhimu cha elimu, uzoefu na kuthubutu kugombea ubunge majimboni. Kwa mujibu wa mchanganuo huo wa kupata wabunge wa viti maalum, Musori alikuwa amepata alama za chini ambazo zingeweza kumpa ubunge tu iwapo Chadema ingefanya vizuri zaidi kwenye uchaguzi mkuu.
 
nipo hapa stand ya mabasi ngudu-kwimba,kuna mkutano wa chadema,unaöngozwa na wenje,letisia nyerere,na mtoto wa mashishanga yule mkuu wa mkoa wa zaman wa mwanza,watu wanaipenda chadema hadi noma

nchi ni yetu...ni mali ya umma...umma umeshaamua, utaikomboa nchi yao na hakuna intelijensia wala nguvu yoyote ya kuzuia maamuzi ya umma...tunisia wameweza, misri wameweza, libya wameweza, yemeni wameweza...na sasa nchi zote zilizokalia utawala kwa mabavu na kukuiuka nguvu ya umma...mwisho wao unakaribia....taifa nzima linakombolea...upepo huu ni upepo wa kisulisuli...hauna wa kuuzuia...pamoja daima na daima nguvu ya umma ndio mshindi.....! Jk jiandae, hakuna cha salia mtume....nchi inaelekea kwa wenyewe...wenye uhai wa taifa lao, yaani umma...utawale nchi yao ...ya maziwa na asali ambayo mafisadi na wezi wamekula kwa miaka karibia 50 sasa....!
 
Nipo hapa stand ya mabasi ngudu-kwimba,kuna mkutano wa chadema,unaöngozwa na Wenje,letisia nyerere,na mtoto wa mashishanga yule mkuu wa mkoa wa zaman wa mwanza,watu wanaipenda chadema hadi noma
poa tufanyeje sasa????
 
Mmmh Mch. naona utakuwa umesahau.
Leticia Nyerere hapo ndiyo kwao na aligombea ubunge kupitia CDM kwimba aliyetangazwa mshindi ni Mansori (MOIL) mfanyabiashara mwenye asili ya asia ambaye tangu kutangazwa hadi leo haijui Ngudu wala Kwimba. Akija wana Kwimba tumuondoe kama Mubarak
 
Mbunge wa hapa kwimba mh. Masoli (msambaza mafuta migodini),toka atanganzwe na DED(Mkurugenzi) wa hapa hajawaii onekana hapa kwimba-mwanza,juzi alipigiwa simu haje kwenye vikao na wananchi,akajibu yupo uarabuni kwenye biashara zake za mafuta,leo wamemshitaki kwa letisia nyerere,na Wenje


Wamemshitaki wa nini sasa? Waache wakome. Nani aliwaambia wamchague uyo gabachori? Walipata nafasi ya kumchagua Leticia wakakubali sumu za akina Madaraka! Waache waipate fresh ingawa mimi ni jirani yao hapo Sumve(ambako tuna fisadi Ndasa kutokana na uwizi wake,ila nina furaha watu wangu wa Sumve wameamka kidogo,kama ni moto unahitaji kupulizwa ili ukolee)
 
Back
Top Bottom