Kwikwi (Hiccups): Chanzo na Tiba (matibabu) yake

Kwikwi hutokana na kushtuka na kusinyaa kwa ghafla kwa misuli mikuu ya upumuaji (diaphragm) ambako hujirudia rudia na kusababisha hewa kuingia kwa kasi kwenye mapafu.

Hii husababisha milango ya sauti katika koo (vocal cords or voice making cords) kufunga ghafla na kutoa sauti inayosikika wakati wa kwikwi.



Kwikwi sio ugonjwa; kwikwi ya muda mfupi ni kero ndogo tu ambayo inapita, lakini kwikwi isiyokatika inaweza kuwa dalili ya tatizo lingine ambalo huenda likahitaji uchunguzi wa kitaalamu.

Sababu zinazopelekea kupata kwikwi;
  • Kula haraka haraka au kula sana (kuvimbiwa)
  • Kula vyakula vyenye viungo sana (very spicy foods)
  • Kunywa vinywaji vyenye gesi(carbonated beverages) au vya baridi sana
  • Ulevi au kunywa pombe nyingi kwa mpigo
  • Upungufu wa maji na madini mwilini (dehydration)
  • Tumbo kujaa gesi, asidi (hyperacidity) au vidonda vya tumbo
Sababu hizi mara nyingi husababisha kwikwi ya muda mfupi ambayo huisha bila kuhitaji matibabu wala uchunguzi wa kitaalamu.

Sababu nyingine (Rare but serious) ni pamoja na;
  • Upungufu au kuvurigikwa kwa kiasi cha madini mwilini(electrolyte imbalances)
  • Kukusanyika kwa sumu mwilini kama vile sumu ya figo (Uremia)
  • Magonjwa ya mapafu kama vile vichomi(pneumonia), pumu(asthma), TB au maji kukusanyika nje ya mapafu(pleural effusion),
  • Saratani au uvimbe kwenye mapafu, ubongo, uti wa mgongo au tumboni.
  • Magonjwa ya moyo (heart attack, arrhythmias, infections to the heart)
  • Kidole tumbo(Apendix illness) na magonjwa ya kufanania nayo
  • Magonjwa ya Ini, kongosho au mfuko wa nyongo
  • Madawa au kunywa sumu aina fulani
  • Kuumia katika eneo la misuli ya upumuaji (diaphragm injuries).
Kwikwi itokanayo na matatizo haya huwa ya muda mrefu au inayojirudia rudia sana, na huisha tu kama tatizo lililosababisha likigundulika na kutibiwa. Ukiona dalili ya kwikwi isiyoisha tafadhali muone daktari.

Sababu ya kisaikologia (psychological reason)– Hii huwapata watu wachache. Watu hawa hujidhania kuwa wana kwikwi isiyokatika, hivyo huendelea kutoa sauti kama mtu mwenye kwikwi. Kwikwi ya aina hii haina mfumo maalum, na haitokani na kusinyaa kwa misuli ya upumuaji; kwa mtu mwenye tatizo hili ni muhimu kutafuta tatizo alilo nalo kisaikologia na kulitatua.

Namna ya kuzuia Kwikwi
  • Kula taratibu – haraka haraka hujaza gesi tumboni na kusababisha kuvimbiwa
  • Kula kiasi kidogo kwa wakati – Inashauriwa kuongeza idadi ya milo kwa siku badala ya kiasi; milo mitano midogo midogo badala ya mitatu mikubwa kwa siku.
  • Punguza au ondoa kabisa vyakula vyenye viungo vingi/vikali.
  • Kunywa maji – Unywaji mzuri wa maji huzuia na kutibu kwikwi, pia hulinda mwili na maradhi kama vile upungufu wa maji na madini(dehydration) na figo kutofanya kazi vizuri.
  • Fanya mazoezi - huboresha ufanyaji kazi wa mapafu na misuli ya upumuaji, pia husaidia kuongeza kinga mwilini na kuimarisha ufahamu (mind state)
Kuzuia kwikwi ni muhimu tu kwa wale wanaopata mara kwa mara.

Matibabu ya asili: (Usifanye kwa mtoto)
  1. Kumshitua mhusika, au kumzubaisha ili kuondoa mawazo yake kwenye kwikwi
  2. Kunywa glasi ya maji iliyojaa bila kukata pumzi
  3. Kubana pumzi na kuhesabu mpaka kumi
  4. Kuweka sukari chini ya ulimi
  5. Kulala. Usingizi ni dawa moja nzuri sana ya kwikwi
  6. Kwa mtoto anayenyonya waweza kumnyonyesha, au kumuweka begani acheue.
  7. KWIKWI-twanga hiliki changanya na maziwa kisha kunywa glasi moja.

Matibabu ya kitaalam

Muone daktari kwa matibabu endapo:
  • Kwikwi haikatiki kwa muda mrefu (siku au zaidi),
  • Kwikwi inakusababisha kuchoka sana,
  • Kama mapigo ya moyo yanabadilika,
  • Kama unashindwa kulala kutokana na kwikwi
  • Kama inasababisha msongo mawazo kutokana na kujirudia mara kwa mara.
Kabla ya kuanzisha dawa ni muhimu kufanya vipimo ili kuhakikisha magonjwa yanayoweza kusababisha kwikwi yanapatiwa matibabu kama yapo.

Kama chanzo cha kwikwi kimefahamika katika uchunguzi, tibu chanzo na kwikwi itaisha.
 

Kivumah

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
2,428
1,050
Nina tatizo kila nikinywa bia inapofikia ya tatu au ya nne huwa nashikwa na kwikwi, hivi ni kwanini inanitokea hivyo?

Suluhisho ni nini?

Pia Soma, Kwikwi kwa mtoto mchanga: Chanzo na Tiba

-
habari za mchana wakuu hivi tatizo la kwikwi ya muda mrefu, inasababishwa na nini?
-
Habari!mimi nina tatizo la kusumbuliwa na kwikwi kila ifikapo usiku wakati wa kula chakula,kwa anayejuwa dawa au mtaalam naomba anisaidie kwa hili kwani ikifika usiku wakati wa kula sipati raha


--------- Maelezo--------

--
 
ninalo tatizo kila nikinywa bia inapofikia ya tatu au ya nne huwa nashikwa na kwikwi, hivi ni kwanini inanitokea hivyo?, na solution ni nini?.nisaidieni mabingwa

Kwikwi ni involuntary action mwilini ambapo mwili unakuwa unafanya marekebisho ya baadhi ya mifumo yake, na huwa haina dawa ya haraka, inaacha yenyewe ndani ya wastani wa dakika 20!

Lakini watu wengine wanasema ukishituliwa na kitu au na mtu kwikwi inaacha automatically, ndo maana baadhi ya watani akiona una kwikwi anaweza akakulamba ngumi ya mgongo, na kwikwi ikakatika hapohapo!
 
Ni kuondoa gesi mkuu, punguza au acha pombe. watoto wadogo inawatokea sana, kwasababu ya kunyonya maziwa.
 
Mwili unakuwa umepata kiasi kikubwa kuhimili kilevi na hivo mwili una alert kuwa sasa kiwango kinatosha. pata mbili tuu kwa afya na kama unataka ta tatu agiza na nyama choma kusindikizia. ukinywa kavu kavu tuu mbili inatosha.
 
Hi Doctor mimi ni kijana wa miaka 22 nina tatizo la kwikwi huanza nikiwa nakula au nikiamka asubui hukaa kwa masaa kama matano then hukata. Je hili tatizo hasababishwa na nini na dawa yake ni nini.
 
Hi Doctor mimi ni kijana wa miaka 22 nina tatizo la kwikwi huanza nikiwa nakula au nikiamka asubui hukaa kwa masaa kama matano then hukata. Je hili tatizo hasababishwa na nini na dawa yake ni nini.

Kwikwi inaweza kusababishwa na matatizo kwenye central nevous system, mfumo wa chakula, ubongo (mental), au hata miwasho (irritation) kwenye baadhi ya neva. Kimsingi ni kwikwi ni dalili ya tatizo fulani.

Nakushauri uende hospitali bila kuchelewa.
 
hivi jamani kwikwi ni ugonjwa au hali fulani tu ya mwili.kama ni ugonjwa, je tiba yake ni ipi? nakumbuka zamani tulikuwa tunabandika kipande kidogo cha karatasi usoni pindi kwikwi inapoanza kama tiba. sina uhakika kama kwikwi iliisha yenyewe au kwa sababu ya kile kikaratasi.na kwa kiengereza kwikwi inaitwaje,nimejaribu kuwauliza watu wengi hili swali bila mafanikio?
 
habari za mchana wakuu hivi tatizo la kwikwi ya muda mrefu, inasababishwa na nini?
 
Hujafafanu inakutokea wakati gani ili wataalamu wakusaidie, Kama inakutokea mara tu baada ya kula kunywa maji kila unapomaliza kula na jaribu kunywa maji nusu saa kabla ya mlo uone itakuwaje. Mimi si mtaalamu ila wanaojua watakuja na maelezo ya kina. Wapo wanaoamini kuwa kwikwi ni dalili ya mtu aliyelogewa chakula hivyo unapaswa ukatapishwe kwenu, hayo si maneno ya wataalamu subiri nao watasemaje.
 
Habari!mimi nina tatizo la kusumbuliwa na kwikwi kila ifikapo usiku wakati wa kula chakula,kwa anayejuwa dawa au mtaalam naomba anisaidie kwa hili kwani ikifika usiku wakati wa kula sipati raha
 
Dawa yake fanya mazoezi haya: ukishikwa tu na kwikwi jaribu kubana pumzi kwa muda wa kama dakika 1 halafu baada ya hapo shushu pumzi kwa nguvu hapo ndugu yangu hautashikwa na kwikwi tena.
 
Jaribu kutumia asali mbichi unapaka kwenye mkate unakula,tumia mala kadhaa itaisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…