Kwenye viwanda tulichemka, Bandari tuweze? Nionyesheni tulichowahi kubinafsisha tukapata faida!

Trable

JF-Expert Member
Jan 3, 2023
1,783
3,281
Watanzania tumerogwa siyo bule!

Siku zote mkaguzi wa hesabu za Serikali (CAG) mara zote ukaguzi wake katika sector ya Bandari amekuwa akisisitiza ufanisi uongezwe ili mapato yaongezeke ukilinganisha na Bandari zingine, lakini hakuwahi kusema kuna hasara iliyotokana na uendeshaji wa Bandari yetu,

Swali kwa serikali, kushauriwa ili kuongeza ufanisi katika Bandari yetu, jibu ni kubinafisisha?

Tuseme tumesahau yoote yaliyofanyika kipindi cha Aliyekuwa Rais awamu ya Tatu Benjamin Mkapa?

Tulibinafisisha viwanda vyoote na baadhi ya mashirika ya serikali, tulipata faida ipi licha ya ahadi nyingi kwamba tungepata faida kubwa kwenye biashara hiyo!

Tulishuhudia hasara kubwa kiasi kwamba washirika wa biashara hiyo walipoondoka, tulijikuta tumepoteza viwanda' vingi na mhimu katika nchi yeti kiasi ambacho mpaka sasa tumebaki kuvitamani tu viwanda vyetu vingelikuwepo kungelikuwa vile na vile!

Je! viongozi wetu hawawi na kumbukumbu ya hayo? wandishi wa habari kina Pascal Mayalla mko wapi kurejea hizi biashara haramu zilivyowahi kuigharimu nchi yetu?

Tunaongozwa na mihemko na ushabiki kwenye mambo mhimu

Kubinafisisha bandari zetu! Inaweza kusiwe kosa, lakini Je! Ni lini na wapi, mkataba kama huu uliowahi kufanywa huko nyuma ukaipa serikali yetu faida?

Tukumbuke! Kubinafisisha vichocheo vya uchumi katika nchi, ni kuji riski kama nchi

Ndani ya miaka hiyo ya ubinafisishaji Bandari, wataalam wetu wamechambua na kujiridhisha vema, kuona faida na hasara zake?

Ni wafanya kazi wangapi wataachoshwa kazi hapo, familia ngapi zitaathirika na ubinafisishaji huo?

Naweza kusema kwamba, huwenda sisi huwa tunatamani na kupenda mambo makubwa na kwa haraka ili hali upeo na uwezo wetu ni mdogo kuliko tunachokitamani!

Ilishindikanaje kupata faida kwenye kubinafisisha viwanda na leo inawezekanaje tupate faida ili hali utendaji wetu bado haujabadirika

Wenye kutaka 10% bado wapo! Wenye mkono wao kwenye mikataba kama hii wapo!

Kama tu suala la mafisadi limetushinda kushughurikia! Nina hakika, hasara ya kubinafisisha Bandari itakuwa kubwa kuliko tunavyoaminishwa!
 
Watanzania tumelogwa siyo bule!

Tuseme tumesahau yoote yaliyofanyika kipindi cha Aliyekuwa Rais awamu ya Tatu Benjamin Mkapa?

Tulibinafisisha viwanda vyoote na baadhi ya mashirika ya serikali, tulipata faida ipi licha ya kuambiwa tungepata faida kubwa kwenye biashara hiyo!

Tulishuhudia hasara kubwa kiasi kwamba washirika wa biashara hiyo walipoondoka, tulijikuta tumepoteza viwanda' vingi na mhimu katika nchi yeti

Tatizo la viongozi wetu, hawawi na kumbukumbu ya hayo, wandishi wa habari ndo kabisaa, kina Pascal Mayalla hawezi tena kuchambua kulinganisha na uwekezaji wa Aina hii hii ambayo imewahi kufanyika kipindi cha nyuma!

Tunaongozwa na mihemko na ushabiki kwenye mambo mhimu

Kubinafisisha bandari zetu! Inaweza kusiwe kosa, lakini Je! Tunafanyeje ili tusirejee kule tulikotoka?

Tukumbuke! Kubinafisisha vichocheo vya uchumi katika nchi, ni kuji riski mno'

Ndani ya miaka hiyo ya ubia, hasara zake ni zipi na faida zake ni zipi?

Mpaka sasa, kwa harakaharaka, hasara zake ndiyo nyingi kuliko faida,

Tunakwenda kupoteza wafanya KAZI wengi hapo bandarini, familia nyingi zitaathirika na ubinafisishaji wa bandari hii
Tusidanganyane. Uwezo kuendesha bandari hakuna. Hii nchi ni ya wapigaji tu.
 
Mtoa hoja umeuliza swali nzuri sana. Watuambie kwanza ni shirika Gani lilibinafsishwa likawa hai au likaleta faida ndani ya nchi. Mama kama umasikini ulitukuta nao tunaomba utuachie tu umasikini wetu tukomae nao tu lakini sio kuuzika kirahisi hivyo. Tunajua mnanguvu na mnaweza kuamua kutokutusikiliza kama ilivyokuwa kwenye NBC ya mkapa, viwanda vya mkapa, gas ya mtwara ya Kikwete, tunakumbuka vizuri sana kipindi mmebinafsisha reli, tunakumbuka sana General tyre ya arusha hatuna la kuwafanya.
 
Huko umeenda mbali sana nakumbuka ahadi za gesi ya mtwara tuliambiwa huo mradi utaleta tija kubwa sana kiuchumi pamoja na kushusha bei ya umeme na faida zingine kede kede

Ila sasa tulichopata na nachoona ni majuto na simanzi tu
 
Tatizo la CCM ni ulafi na kukosa uzalendo. Hizo 10% zitaligharimu taifa.
 
Kabla ya kubinafsisha, bandari ilikuwa inatupa faida (ukitoa matumizi) au hasara? Ilikuwa inaingizia serikali kiasi gani cha fedha za kigeni? Na je kwa sasa, tunategemea kupata kiasi gani cha fedha za kigeni?
Tujipime kwenye hayo maswali.​
 
Mliosoma kitabu cha Che Nkapa mtuambie,nimesikia amekiri humo kwamba aliingia chaka kwenye ubinafsishaji.

Ni Juzi tu hapa wahindi wa TRL waliharibu mkawanyang'anya.

Juzi tu tumeambiwa Dar port imempiku kwa ufanisi mshindani wake mkubwa Mombasa,hiki kifafa cha kuwapa waarabu cha nini wakati huu?

Uwekezaji mkubwa umefanyika na matunda yameanza kuonekana, waarabu wa nini tena?
 
Kabla ya kubinafsisha, bandari ilikuwa inatupa faida (ukitoa matumizi) au hasara? Ilikuwa inaingizia serikali kiasi gani cha fedha za kigeni? Na je kwa sasa, tunategemea kupata kiasi gani cha fedha za kigeni?
Tujipime kwenye hayo maswali.​
CAG ajibu hii,

Ukaguzi na ukaguzi sijawahi sikia hasara kwa Bandari yeti ila tu unaambiwa ufanisi uongezwe basi!
 
Naombeni mnisaidie Kwani hao waendeshaji wa awali kina TICS sijui walikuwa na udhaifu gani mpaka kumpa Mwarabua au tumechukua mkopo huko tumeshindwa kulipa kama Sri Lanka?

Au kuna mtu anatengeneza mfereji wa 10% ili kizazi chake kiendelee kula keki ya taifa?

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Ikiwezekana tuwape Kila kitu

Sisi hatuna uwezo na lolote kufanya

Tuwape vyote tu sisi hatuna AKILI
 
Nyoka anauma kichwani..kama kichwa cha nyoka kimekatwa, makali ya nyoka pia yamekwisha hapo hapo. Mwenye akili ana azitumie
 
Watanzania tumerogwa siyo bule!

Siku zote mkaguzi wa hesabu za Serikali (CAG) mara zote ukaguzi wake katika sector ya Bandari amekuwa akisisitiza ufanisi uongezwe ili mapato yaongezeke ukilinganisha na Bandari zingine, lakini hakuwahi kusema kuna hasara iliyotokana na uendeshaji wa Bandari yetu,

Swali kwa serikali, kushauriwa ili kuongeza ufanisi katika Bandari yetu, jibu ni kubinafisisha?

Tuseme tumesahau yoote yaliyofanyika kipindi cha Aliyekuwa Rais awamu ya Tatu Benjamin Mkapa?

Tulibinafisisha viwanda vyoote na baadhi ya mashirika ya serikali, tulipata faida ipi licha ya ahadi nyingi kwamba tungepata faida kubwa kwenye biashara hiyo!

Tulishuhudia hasara kubwa kiasi kwamba washirika wa biashara hiyo walipoondoka, tulijikuta tumepoteza viwanda' vingi na mhimu katika nchi yeti kiasi ambacho mpaka sasa tumebaki kuvitamani tu viwanda vyetu vingelikuwepo kungelikuwa vile na vile!

Je! viongozi wetu hawawi na kumbukumbu ya hayo? wandishi wa habari kina Pascal Mayalla mko wapi kurejea hizi biashara haramu zilivyowahi kuigharimu nchi yetu?

Tunaongozwa na mihemko na ushabiki kwenye mambo mhimu

Kubinafisisha bandari zetu! Inaweza kusiwe kosa, lakini Je! Ni lini na wapi, mkataba kama huu uliowahi kufanywa huko nyuma ukaipa serikali yetu faida?

Tukumbuke! Kubinafisisha vichocheo vya uchumi katika nchi, ni kuji riski kama nchi

Ndani ya miaka hiyo ya ubinafisishaji Bandari, wataalam wetu wamechambua na kujiridhisha vema, kuona faida na hasara zake?

Ni wafanya kazi wangapi wataachoshwa kazi hapo, familia ngapi zitaathirika na ubinafisishaji huo?

Naweza kusema kwamba, huwenda sisi huwa tunatamani na kupenda mambo makubwa na kwa haraka ili hali upeo na uwezo wetu ni mdogo kuliko tunachokitamani!

Ilishindikanaje kupata faida kwenye kubinafisisha viwanda na leo inawezekanaje tupate faida ili hali utendaji wetu bado haujabadirika

Wenye kutaka 10% bado wapo! Wenye mkono wao kwenye mikataba kama hii wapo!

Kama tu suala la mafisadi limetushinda kushughurikia! Nina hakika, hasara ya kubinafisisha Bandari itakuwa kubwa kuliko tunavyoaminishwa!
Upo sahihi ndo maan JPM aliona ni bora kua viwanda cherehani like!!
 
Back
Top Bottom