Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 8,729
- 11,988
nikiwa kiraia zaidi, nimejumuika na wananzengo vijiwe vya kahawa, kashata, kachori na pweza. Stori na hadithi nyingi zimetekwa na jina la Rais, Dr Samia Suluhu Hassan.
Kwamba huyu mama ni hodari, anajali sana, ana bidii mno ya kazi, anaskiza sana maoni ya wananchi, ni mahiri na makini sana kwenye kuchukua maamuzi magumu na hatua za kuwaletea wananchi uhuru, haki na maendeleo.
Wanadai mama amefungua nchi, fursa zipo na zinaonekana saivi na pesa inapatikana kwa wenye kuchapa kazi kwa bidii na inaonekana.
Ubora wa maisha na urahisi wake, unapanda na kuongezeka siku hadi siku. Wangwana na watafutaji hawa wasiochoka wala kukata tamaa, kwakweli wanafurahia na kunufaika kwa jitihada na hatua mbalimbali za kiuchumi anazochukua Raisi.
Wadau wanafunguka zaidi kwamba nchi ni tulivu mno, haijawahi kutokea. Ulinzi na usalama wa mipaka, mali na raia ni wa uhakika sana nchini. Amani imetawala pote Tanzania.
Hii ni sehemu ndogo tu ya makundi mengi sana wanaofurahia na kunufaika na mipango ya serikali ya Dr Samia mthalani bodabodas, mabajaji, madaladala nk.
Wanadai 2025 kama huyu muMama atagombea, basi uhakika wa kura zao ni asilimia 100%. Wanashauri watoa taarifa na wengineneo bora wakafanye mambo mengine lakini sio uongozi wa nchi hii wakati huu.
Kiufupi huyu muMama anapendwa sana na anakubalika mno vijiweni.
Kupambana na huyu mama ni kupoteza muda.....
Wacha tusubiri,
Time Will tell.....