Ndallo
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 7,619
- 4,293
Muheshiwa Raisi wangu Jakaya Mrisho Kikwete husika na kichwa cha habari hapo juu! Tumezoea kukuona kwenye kushiriki kwenye tafrija nyingi tu hususani kwenye misiba hata hapo jana tulikua wote pale Morogoro tulipokwenda kumsitiri mwanaharakati dada yetu Regia Mtema uliliwakilisha taifa letu kwenye mazishi yale pasipo kukereka na mvua iliyokua inanyesha siku ya tukio hilo.
Dhumuni la kuandika Thready hii sio kwamba nataka kuunda hoja ya kuwa ni lazima kwenye tukio lolote linalohusu misiba basi ni lazima uwepo la hasha, kunaweza kutokea dharura ya kikazi na ukawa nje ya nchi kwaajili ya kazi za kuleta maendeleo katika nchi yetu basi ukawakilishwa na makamu wako au hata na kiongozi mwingine wa kitaifa.
Lengo na madhumuni yangu kuhusiana na swali langu hapo juu ni kua, muheshimiwa Raisi wangu tokea kwa uchaguzi wa uraisi/madiwani na wabunge kuisha na matokeo kutolewa na wewe kupata ridhaa ya kutuongoza kwa awamu hii ya mwisho kwako ni kua, ni jukumu lako kama raisi wetu kupita mikoani kwa wananchi waliokupa ridhaa ya kuwaongoza na kutoa shukrani zako kama ulivyodai ulishinda kwa kishindo kwa wao kukupa kura za kishindo kuingia Ikulu tena.
Muheshimiwa JK mimi na wenzangu ni wakazi wa jiji ambalo limetawaliwa na migogoro mingi ya kisiasa tokea chaguzi ziishe na mpaka sasa hivi tunaongozwa kwa migogoro isioisha nazungumzia jiji la Arusha. Muheshimiwa tokea upate fursa ya kuingia Ikulu hujafika hata kwenye ule uwanja uliopewa jina la kiongozi mkubwa na sijui kama kizazi hiki tulichonacho kama wanaijua historia ya huyu bwana Sheik Amri Abeid Karume, angalau kukaa na sisi kwa masaa mawili na kutushukuru kwakukupa ridhaa ya kuingia hapo ulipo.
Basi muheshimiwa nisimalize wino wangu kwakwenda mbali kuhusiana na hoja hii, nakuomba tu muheshimiwa JK kama utapata fursa ya kuja kushiriki na sisi kwenye msiba wa ndugu yetu Jeremiah Sumari basi angalau chukua na fursa angalau ya kukaa na sisi japo baada ya mazishi kumalizika au utuahidi utakuja lini tena rasmi kwaajili ya kutupa shukrani zetu za sisi kukupa kura zakutosha za wewe kutuongoza kwa awamu nyingine.
Nakushukuru sana muheshimiwa JK kwakupata muda wa kupitia ujumbe huu hapa jamvini na ninamatumaini hutatuangusha kwa haya tuliyokuomba, tusisikie tu kuwa muheshimiwa yuko Serengeti/Ngorongoro anaangalia wanyama, basi na sisi tunaomba hiyo fursa ya kuwa na sisi japo kwa muda tu ili tupate hizo shukrani zako. Asante na namalizia kwa swali langu KWENYE MAZISHI YA MUHESHIMIWA JEREMIAH SUMARI JK JE UTAHUDHURIA?
Asante sana,
Ni mimi niliyekupa kura za kutosha,