Kwenye Mazishi ya Mhe. Jeremiah Sumari; JK atahudhuria? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwenye Mazishi ya Mhe. Jeremiah Sumari; JK atahudhuria?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ndallo, Jan 19, 2012.

 1. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Muheshiwa Raisi wangu Jakaya Mrisho Kikwete husika na kichwa cha habari hapo juu! Tumezoea kukuona kwenye kushiriki kwenye tafrija nyingi tu hususani kwenye misiba hata hapo jana tulikua wote pale Morogoro tulipokwenda kumsitiri mwanaharakati dada yetu Regia Mtema uliliwakilisha taifa letu kwenye mazishi yale pasipo kukereka na mvua iliyokua inanyesha siku ya tukio hilo.

  Dhumuni la kuandika Thready hii sio kwamba nataka kuunda hoja ya kuwa ni lazima kwenye tukio lolote linalohusu misiba basi ni lazima uwepo la hasha, kunaweza kutokea dharura ya kikazi na ukawa nje ya nchi kwaajili ya kazi za kuleta maendeleo katika nchi yetu basi ukawakilishwa na makamu wako au hata na kiongozi mwingine wa kitaifa.

  Lengo na madhumuni yangu kuhusiana na swali langu hapo juu ni kua, muheshimiwa Raisi wangu tokea kwa uchaguzi wa uraisi/madiwani na wabunge kuisha na matokeo kutolewa na wewe kupata ridhaa ya kutuongoza kwa awamu hii ya mwisho kwako ni kua, ni jukumu lako kama raisi wetu kupita mikoani kwa wananchi waliokupa ridhaa ya kuwaongoza na kutoa shukrani zako kama ulivyodai ulishinda kwa kishindo kwa wao kukupa kura za kishindo kuingia Ikulu tena.

  Muheshimiwa JK mimi na wenzangu ni wakazi wa jiji ambalo limetawaliwa na migogoro mingi ya kisiasa tokea chaguzi ziishe na mpaka sasa hivi tunaongozwa kwa migogoro isioisha nazungumzia jiji la Arusha. Muheshimiwa tokea upate fursa ya kuingia Ikulu hujafika hata kwenye ule uwanja uliopewa jina la kiongozi mkubwa na sijui kama kizazi hiki tulichonacho kama wanaijua historia ya huyu bwana Sheik Amri Abeid Karume, angalau kukaa na sisi kwa masaa mawili na kutushukuru kwakukupa ridhaa ya kuingia hapo ulipo.

  Basi muheshimiwa nisimalize wino wangu kwakwenda mbali kuhusiana na hoja hii, nakuomba tu muheshimiwa JK kama utapata fursa ya kuja kushiriki na sisi kwenye msiba wa ndugu yetu Jeremiah Sumari basi angalau chukua na fursa angalau ya kukaa na sisi japo baada ya mazishi kumalizika au utuahidi utakuja lini tena rasmi kwaajili ya kutupa shukrani zetu za sisi kukupa kura zakutosha za wewe kutuongoza kwa awamu nyingine.

  Nakushukuru sana muheshimiwa JK kwakupata muda wa kupitia ujumbe huu hapa jamvini na ninamatumaini hutatuangusha kwa haya tuliyokuomba, tusisikie tu kuwa muheshimiwa yuko Serengeti/Ngorongoro anaangalia wanyama, basi na sisi tunaomba hiyo fursa ya kuwa na sisi japo kwa muda tu ili tupate hizo shukrani zako. Asante na namalizia kwa swali langu KWENYE MAZISHI YA MUHESHIMIWA JEREMIAH SUMARI JK JE UTAHUDHURIA?

  Asante sana,
  Ni mimi niliyekupa kura za kutosha,
   
 2. m

  mariantonia Senior Member

  #2
  Jan 19, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 135
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huyu summari alikuwa mponda democrasia
  alikuwa akijibu maswali kiajabu nadhani ugonjwa wa ubongo ulimwaza siku nyingi

  RIP sumari
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Raisi wa kwenye Misiba lazima atie timu
   
 4. M

  MPG JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2012
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Limbukeni Kikwete sijui kama atakuja kwa kweli,Chadema aliwaogopa ndiyo mana alikwenda!
   
 5. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #5
  Jan 19, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 0
  mkuu ulipiga kura ngapi?
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,947
  Trophy Points: 280
  naona unamuuliza kenge kuwa ana mkia ??
   
 7. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Kama utasoma kwa umakini sehemu nimesema mimi na wenzangu! natumaini umenielewa!

   
 8. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Raisi Kikwete amekua akishiriki kwenye shuguli nyingi za kijamii kama misiba,harusi na kuangalia wagonjwa. Hii inahusiana zaidi na tabia yake binafsi ambayo inahusiana zaidi na malezi yake. Tabia hii ambayo inaendana na utamaduni wa kiafrika ni ya kuheshimiwa. Ni WATU wengi hujisahau katika neema za nyakati na kujitenga na " matatizo" misiba n.k. Inafahamika bayana kwamba Raisi Kikwete amekua mshiriki wa shuguli za kijamii Kabla na hata baada ya kupata nyadhifa mbalimbali hadi kufikia kuwa Raisi. Si busara kubeza au kuhusisha tabia hii ya Rais na mambo ya kisiasa Kama hiyo kiu ya WATU wa Arusha kukaa na kiongozi wa nchi. Kichwa cha Uzi huu kimenichefua kwa sababu kwa mtazamo wangu kina "kebehi" tabia ya kibinadamu ya kimaadili ambayo Raisi ameionyesha kwa jamii YETU. Waungwana "mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni"
   
 9. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Ninashauku kubwa sana ya kumuona JK pale Sheik Amri Abeid Karume! Uzinduzi wa chanjo kwa watoto ilikua imeshapangwa aje lakini alimtuma Bilali sijui kwanini!
   
 10. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Sipati picha ya wewe kwanini ushikwe na kichefuchefu kwa uzi huu! Watanzania tunahulka ya ukarimu sana na hii inajulikana, unapopata heshima huwa kwenu nyie hamtoi shukrani??
   
 11. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #11
  Jan 19, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  sijui na huko ataenda kuzindua daraja...
   
 12. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ashaenda mara 2 Arusha, lakini mara zote anashuka Uwanja wa ndege, anakatiza mahala panaitwa Canada, na kwenda zake Monduli...hasogei Arusha mjini!
  Anyway, kwa Sumari ataenda kwa vile ni Wilaya nyingine, si Arusha mjini!...kule kwa Wameru wenzangu hakutishi kama A-Town kwa vijana wa Lema bana!
   
 13. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #13
  Jan 19, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  kweli kabisa ni sawa nakuuliza kiremba kwa osama...
   
 14. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #14
  Jan 19, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  sijui labda anawezafanya hivyo
   
 15. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #15
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu SAHIHISHO dogo,
  Hapo kwenye red ni Sheikh Amri Abeid Kaluta na si Sheikh Abeid Amaan Karume

  Mpevu,
   
 16. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #16
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  In red colour should read....Sheikh Amri Abeid Kaluta iwapo unamaanisha uwanja ule maarufu wa A-town. Otherwise utakuwa sahihi iwapo unamaanisha uwanja wa aidha paleeee mtaa wa uhuru/Lindi jirani ya machinga complex au unamaanisha ule uwanja wa Amaan-ZNZ.
   
 17. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #17
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Akose? Hayo ndiyo majukwaa ya kuuzia sura.
   
 18. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #18
  Jan 19, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Watu wengi wanachanganya asli ya jina la uwanja wa SHEIKH AMRI ABEID.Si AMRI ABEID KARUME bali ni AMRI ABEID KALUTA!Hayati Amri Abeid Kaluta alipata kuwa waziri enzi ya Nyerere na mshairi maarufu.Kwa heshima yake uwanja wa Arusha ukapewa jina lake.
   
 19. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #19
  Jan 19, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mkuu, you have gone too far. Hata kama ushindi wake ni kama wa kijana wake Jose Kabila lkn anastahili staha.
   
 20. L

  Lsk Senior Member

  #20
  Jan 19, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ...alilazimika kujihusisha sana na msiba wa Regia Mtema (RIP) kwa kuogopa nguvu za umma. Lakini very possible hata huko kwa Sumari (RIP) akahudhuria,maana yeye ni mtu wa kupenda kuuza sura...ataenda kuonyesha tabasamu lake kule
   
Loading...