Kwenye kutangaza matokeo ya uchaguzi huwa hakuna giza

Ni aibu na fedheha sana,wapo tayari azima askari mikoa miwili mfano uchaguzi ukonga,Tanga na Pwani.light plant kanda ya ziwa ni nyingi migodini na mtaani.
 
Matokeo ya uchaguzi hutangazwa hata saa 9 usiku,bila kuahirisha zoezi eti kwa Sababu ya Giza.
Binadamu wamezama eti zoezi la kuwaokoa likaahirishwa kwa Sababu ya Giza,akili za kikatili hivi halafu eti mnataka kufanikiwa? Mtasubiri sana.
Acheni kulia lia. Si Mbowe keshajitoa?
 
Chama cha wanyonge hicho. Muoshimiwa jiwe kajifungia ikulu anakunywa wine na kuku mbona wakati wa Kigwangala alikwenda kumsaidia akambebea drip, miguu akaiweka sawa akamnyanyua akamuweka kwenye kitanda. LAKINI wanyonge akuuu Major Liwe alikuwa anaangalia kwa mbali kwa microscope mimi nilidhanani atakwenda ata asaidie kubeba maiti yeye anaangalia na miwani na kaunda suti yenye kalamu mfukoni alafu yanatanga account za rambirambi. Nimekuwa nashangaa sana hawa viongozi wa wanyonge au mashetani

Alafu kuna watu wanadiriki kuwapa kura. Ukiwapa kura hao masimbilisi ya khaki basi jiandae tuu kuwa shetani
 
Matokeo ya uchaguzi hutangazwa hata saa 9 usiku,bila kuahirisha zoezi eti kwa Sababu ya Giza.
Binadamu wamezama eti zoezi la kuwaokoa likaahirishwa kwa Sababu ya Giza,akili za kikatili hivi halafu eti mnataka kufanikiwa? Mtasubiri sana.
Tatizo ni Moja kwa nchi zetu.
Likitokea Janga kila mtu anataka kuwa wa kwanza kufika tu kutizama ndio maana usiku wanaahirisha kwa sababu hawataona na hawataweza kufika haraka na kuonekana.
Suala la kuokoa linakuaga baadae. Hata kwenye ajali za kawaida ni hivyo hivyo.

Likitokea jambo la ghafla panakua na marathoni za nani atawahi kufika. Mkonini ameshika diary utafikiri ni mwandishi wa habari. RAIA wako hivyo hivyo na viongozi hivyo hivyo. Mpaka helkopta zinarushwa ili tu watu wawahi kuona ; sio kuokoa bali kuona tukio na kuhakikisha kundi kubwa la waandishi wa habari linamfutilia kuliko hata tukio lenyewe.

Hatukatai kuwa watu wasiwahi kufika lakini wawahi kwa ajili ya kuokoa sio kuona. Tunapaswa kuwa na utaratibu wa kuwahisha kundi la uokoaji na kundi la wataalam wa majanga . Kuna vitengo vinaitwa vya maafa lakini kiuhalisia vipo kisiasa na vipo kwa ajili ya kusaidia watu ambao tayari wameshaokolewa. Bajeti yake ipo lakini haipo kwa ajili ya kuokoa bali kusaidia wahanga. Ndio maana kinaitwa kitengo cha maafa yaani, kinasubiri maafa yatokee tu ,sio kuzuia maafa.

Serikali ya CCM inatakiwa isizuie maoni ya watu na pia isiwe nyepesi kupuuza na kupotosha mawazo mazuri ya watu kama mbinu ya propaganda za kisia. Kuna watu ni wepesi kuropoka lakini wana hoja za msingi sana. Mfano Zito Kabwe ni Mtu mdadisi au mtundu kwa Lugha ya Katibu wa Chama Tawala. Lakini anakua na maono makubwa sana na ni mwepesi wa kuona Tatizo na kupendekeza suluhisho. Huyu Kijana ni hazina kubwa sana kwa Taifa hili kama tutaacha Ubinafsi na chuki za kisiasa kama wale wengine walioshindwa kujua uwezo wake wakamtimua.

Tukio au Janga kubwa linapotokea ni vizuri wahusika wa uokoaji ndio wakawahishwa kwa Helkopta na vifaa vyao kwa haraka.
Wakiwa pia na wataalam wao wa kutathmini ukubwa wa janga na kuwapa taarifa viongozi wao wa juu ili wao watoe taarifa ya uzito wa janga kwa viongozi wa kisiasa na kiserikali. Ilivyo sasa wanasiasa ambao pia ni watawala wanawahi kwenye tukio ambalo hawana utaalama nalo na kukusanya waandishi wa habari na kulisemea wakati huo wanaohangaika na tukio ni watu wa kawaida kabisa wasio na vifaa zaidi ya uzoefu tu. Mfano hata ukiangalia mitumbwi ya kienyeji kabisa ndiyo inatumika zaidi tena kwa msaada mkubwa wa wavuvi wa kawaida kabisa.
Ni jambo la tofauti kidogo na fikra zangu ambapo nilijua waokoaji au wazamiaji waliopewa mafunzo maalum na serikali wanakua na jaket maalum za kuvaa na Mask Maalum zenye mitungi ya oxygen kwa ajili ya kukaa kwenye maji kwa masaa mengi ; Huku kichwani wakiwa wameninginiza Tochi maalum yenye mwanga mkali kwa ajili ya kuona wakati wa usiku. Ziwa lenye vyombo vya usafiri tulitegemea lisikose vifaa kama hivyo na vifikishwe kwa haraka kwa kutumia Helkopta ili kupata dira ya eneo husika kwa haraka.

Pia ni vizuri zaidi Wakubwa wa eneo husika baada ya kuhakikisha waokoaji wamefika eneo linalohusika kwa haraka na uokoaji unaendelea ,wao wakakaa Kikao hata kwa lisaa limoja kupeana mawazo ya kipi kinatakiwa kupatikana na wapi kwa namna gani kwa kuanzia wapi na kwa nguvu kubwa kiasi gani na kwa gharama kiasi gani na fedha kupatikana wapi kwa haraka. Mfano kama Kinapatikana Kampuni fulani au idara Fulani mfano Migodini au Jeshini au Wizarani basi taarifa ifikishwe kwa haraka na vifaa au nguvu ya uokoaji iongezeke kwa haraka.

Kusema kweli Mimi hua namkubali sana Ninja Lugola. Kuna watu wanamzihaki lakini anajua anachofanya . Nakumbuka kuna wakati amezungumzia suala la kuimarisha jeshi la Zima moto na uokoaji.
Na tukaambiwa aliwatimua kwenye kikao maafisa walioshindwa kulitaja jeshi hill kama Jeshi la zima Moto na Uokoaji.
Ni dhahiri kuwa Ninja anataka Suala la uokoaji lipewe kipao Mbele. Namuunga mkono sana waziri Kangi Lugola Ninja.
 
Niliwahi kusema ccm hawahangaiki na uhai wa RAIA wao wanachohangaika nacho sana ni kuhakikisha wanaendelea kuwepo madarakani.
 
Back
Top Bottom