Kwenye Kampeni JK alisema Lowasa ni mtu safi waliposhinda anaambiwa "Ajivue" Gamba HII SIO SAWA. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwenye Kampeni JK alisema Lowasa ni mtu safi waliposhinda anaambiwa "Ajivue" Gamba HII SIO SAWA.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Anold, Jun 24, 2011.

 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 298
  Trophy Points: 180
  Hili jambo bado linanighadhibisha, siwezi kuvumilia kuona unafiki huu unafanyika waziwazi, huku ni kuchezea akili za watu, wakati wa kampeni aliyekuwa mgombea wa kiti cha urais ccm alitutangazia kuwa Lowasa ni mtu safi, tena kama haitoshi akaenda tena jimboni kwa Rostam Ikaelezwa kuwa ni mtu wa manufaa, haikutosha mzee Chenge akanyanyuliwa mkono kuwa hakuna mtu safi kama huyu, baada ya uchaguzi watu walipoapishwa na kujihakikishia kuwa wako salama ikaja hoja ya kuwa hawa watu wajivue "gamba". Ni kweli tuna machungu na nchi yetu ila tuende mbele turudi nyuma, huu ni "UNAFIKI" haiwezekani tushabikie michezo hii ya kisiasa, Hawa watu kama wamefiia kuona kuwa watu hawa ni wachafu ni hakika kuwa wanaushahidi uanoweza kuwafikisha mahakamani ili haki itendeke, kumvua mwenzako gamba wakati wewe ni sehemu au chanzo cha tatizo hii ni sawa na Fitina na unafiki usioelezeka, hoja yangu ni kuwa wakishajivua gamba halafu kinachoendelea ni nini? utaratibu huu ukiendelea wa kuhukumu watu kwa tetesi je hautasababisha serikali yetu ionekane ni nchi ya KIDIKTETA? HAPA KUNA UTAWALA BORA.?

  Baada ya Lowasa kujiuzuru Rais aliitisha mkutano na wazee wa jiji la Dar es salaam, pamoja na kuwa haikuwa agenda ila aliingiza kiana na kutangazia wazee wale kuwa Lowasa asihukumiwe, magazeti mengi yaliandika kuwa rais amsafisha Lowasa.

  Katika kampeni za Uraisi kama nilivyokwisa eleza hapo juu akarudia maneno hayo kuwa ni mtu safi.

  Mzee Hosea akafuatwa na waandishi wa Habari aeleze kwa nini hajapeleka watuhumiwa WA UFISADI mahakamani akasema wanafanya kazi zao kwa mujibu wa sheria hivyo hawawezi kumpeleka mtu mahakamani bila kuwa na ushahidi.

  Kinachonisumbua ni kuona unafiki unaoendelea, leo hii umekwenda monduli ukawatangaziwa wananchi kuwa mchagueni mtu huyu ni safi, baada ya miezi mitatu unasikika ukitoa tamko kuwa "mtu huyohuyo ni fisadi ajivue gamba" hekima hii imekaaje jamani? kama wewe mwana JF ungeletewa kesi ya namna hii hukumu yako na lawama zako zingemwelekea nani? wengi ni watu wazima hebu tutafakari mambo haya kiutu uzima. Hapa pana kitu.
   
Loading...