Kwenye gambe hata yule hajaenda shule anaporomosha lugha ya malkia

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
8,154
11,560
Ndugu zangu hii hali ya lugha ya malkia mbona inanchanganya sana.

Unakuta kwenye interview msahiliwa msomi kabisa, ata introduction tu, jasho inatoka na mpaka sauti inapotea kabisa, na haitoki ng'oo. Hawezi kujieleza kiingereza anatetema tu msomi huyu wa chuo..

Lakini msahiliwa huyuhuyu akitoka kwenye interview, kule ambapo lugha ya malkia ilikata sauti, akienda kutupiamo gambe kadhaa. Yaani leta kama tulivyo, round tatu hazifiki lugha ya malkia inachukua mkondo na nafasi yake inatiririka kavizuri kama vilea amezaliwa mamtoni.. One for the road kama zote...

Na hapa kwenye gambe hata yule hajaenda shule anaporomosha lugha ya malkia kwa sauti madaha ,mikogo na slangs kama zote hata kama amekunya pombe mshenzi huko mitaani..

Ni nini siri ya hii kitu gambe, mbona nyingine zimezalishwa humuhumu nchini, zingine ni za kienyeji?
 
Kiufupi walevi hawana Huwezo wa kuongea lugha ya kiingereza kwa ufasaha hii nimejionea pale Bukoba .

Lugha ya malikia inahitaji uwe umejifunza na kuielewa ila kile kiingereza Cha Pombe kinakuwa kibovu Sana sema ukiwa upo maji huwezi elewa
Ndiyo maana yake hiyo mi huwa nashangaa kuhusisha pombe na kingereza kwanini siyo kichina, kijapani ambacho badhi tunafahamu, kirusi, kihindi, au hata kijerumani ila kingereza tu. Kuna vitu tunadanganyana mno kuna thread nilisoma humu jamaa alisema asilimia 98% ya sisi ni wapumbavu watu wengi walimrekebisha nikiri hakuwa sahihi ila tuna upumbavu sana nisamehe sana mkuu wangu Pascal Mayalla.
 
Kiufupi walevi hawana Huwezo wa kuongea lugha ya kiingereza kwa ufasaha hii nimejionea pale Bukoba .

Lugha ya malikia inahitaji uwe umejifunza na kuielewa ila kile kiingereza Cha Pombe kinakuwa kibovu Sana sema ukiwa upo maji huwezi elewa

Tafiti zinaonyesha mtu akilewa wastani uwezo wake wa kuongea lugha ya kigeni unaongezeka.

Bishana na tafiti usibishane namimi

wanakunywa kilevi muda mrefu kisha wakati wanaondoka wanaambianaga One for the road, mbona wakimaliza chai wanaondoka kimyakimya tu...
 
Ndugu zangu hii hali ya lugha ya malkia mbona inanchanganya sana.
Unakuta kwenye interview msahiliwa msomi kabisa, ata introduction tu, jasho inatoka na mpaka sauti inapotea kabisa, na haitoki ng'oo. Hawezi kujieleza kiingereza anatetema tu msomi huyu wa chuo..

Lakini msahiliwa huyuhuyu akitoka kwenye interview, kule ambapo lugha ya malkia ilikata sauti, akienda kutupiamo gambe kadhaa. Yaani leta kama tulivyo, round tatu hazifiki lugha ya malkia inachukua mkondo na nafasi yake inatiririka kavizuri kama vilea amezaliwa mamtoni.. One for the road kama zote...

Na hapa kwenye gambe hata yule hajaenda shule anaporomosha lugha ya malkia kwa sauti madaha ,mikogo na slangs kama zote hata kama amekunya pombe mshenzi huko mitaani..

ni nini siri ya hii kitu gambe, mbona nyingine zimezalishwa humuhumu nchini, zingine ni za kienyeji?
Secret of confidence! gambe increases confidence, at the same time removes fear!
 
Tafiti zinaonyesha mtu akilewa wastani uwezo wake wa kuongea lugha ya kigeni unaongezeka.

Bishana na tafiti usibishane namimi

shukran sana kwa hili,

najiulizaga sana kwanini kwenye chumba cha usahili ukwame kuongea kiingerea, kisha ukienda kupata moja, mbili tatu unaongea vizuri lugha hiyo hiyo ulokwama kujieleza nayo kwenye usahili...

observation za huu utafiti naanza kunipata picha sasa..
 
Back
Top Bottom