Kwanza kabisa kwenye blender kuna render engine mbili, eevee na cycles. Render engine inatumika kutengeneza picha ya mwisho ukishatengeneza scene yako. Kwahiyo ina calculate mwanga, mng'ao wa vitu kama chuma n.k. Eevee ni real time engine ambayo ni kama hizi za game (na ndio wabongo wengi wanatumia, ina render kwa muda mchache sana) kwahiyo ina calculate mwanga kwa makadirio na sio kutumia physics hivyo evee ina sacrifice quality kwa speed. Na mwanga ni kitu kikubwa sana kufanya kitu kionekane kama cha maisha ya kweli. Cycles yenyewe inatumia physics ku calculate mwale wa mwanga ukifika kwenye uso wa kitu utadunda kwenda wapi kama maisha ya ukweli (ray tracing au path tracing). Hivyo picha ya mwisho inakua na quality karibu na maisha ya kweli, lakini kwa cost ya GPU na CPU power. Hivyo ina render kwa muda mrefu sana kama computer ina gpu au cpu ndogo. Mfano hii video yenye sekunde 5 (warning volume ipo juu sana)
View attachment 2194466
nime render kwa cycles, resolution ndogo tu ya 640p lakini imechukua masaa 24 ku render kwenye ki laptop changu. Sasa imagine unatengeneza short movie ya dakika kadhaa, itachukua miezi ku render na computer zetu za kibongo. Pia tofauti na render engines kuna vitu kama ukungu, realistic reflections ambavyo vinaongeza uhalisia na ung'aavu wa picha, vinaongeza muda hata mara 5 kwenye cycles, hivyo wabongo wanavitoa.