road master
JF-Expert Member
- Jun 11, 2020
- 2,064
- 3,011
Nimekosa ajira ya ualimu mwaka wa nne sasa mwaka jana 2019 niliweka pembeni vyeti vya ngumu vyaBsc geography and physics nikaziungam kozi ya miezi miwili ya motor grader operator sijawahi kujutaUnajua maisha ya sasa hivi kila mtu analia kilio chake, huyu atalia sauti ndogo, yule kubwa, yule mwingine atalia kimoyo moyo ila wote tunalia na kubwa linalotoa watu machozi ni Ugumu wa maisha, ukosefu wa ajira, nk.
Leo nitaongea na walimu tu ambao wengi hulalamika ajira hamna,maisha magumu na mtu ana Certificate safi,Diploma mpk Degree ila kilio chake ni kile kile "ajira", hii nitaiongelea kama theory sana maana sijawahi ifanya wala sitegemei kuja kuifanya lkn naamini wapo watakaoweza igeuza hii ikae ki practical zaidi na sio ki blah blah za CONTROLA
Unajua katika hizi elimu tunazopitia ni kweli zipo fani tunazosomea ambazo ni ngumu kuanza kujiajiri kama huna mtaji au huna mtu wa kukuwezesha maana fani za namna hiyo zinahitaji mitaji pesa,mitaji vifaa nk nk, ila kuna hii fani ya ualimu ambayo nimeshashuhudia walimu wakiitumia kupiga mkwanja kuliko hata wale walimu walio ktk ajira maana ni moja ya fani ambazo mtaji wake mkubwa ni "kilichopo ndani ya ubongo wako"
Walimu wengi hujiajiri kwa njia za tuition(vizuri kabisa) lkn ktk hawa walimu wengi wao karibia 81% Tuition hizo hufa kifo cha mende miguu juu,unajua ni kwanini hizo tuition zao hufa? Hawa walimu si kwamba hawafundishi vizuri, si kwamba hawajulikani kama wanafundisha tuition,hapana ila shida ya hawa walimu woteee tuition zao zinazokufa ukiwauliza sababu ya wao kutoendelea na tuition jibu lao ni moja kwamba "wanafunzi hamna"
Mwalimu anakwambiia wanafunzi hamna,unamuuliza swali,wanafunzi hamna kivipi kwamba wale wanafunzi wamefika chuo wote au wamehama huo mtaa au imekuaje wanafunzi hamna wakati wanafunzi wale wale tunawaona wanaendelea kwenda shule??
Mwalimu anakwambia "wazazi hawana pesa" (sababu kuu) unakuta unamfundsha tuition mtoto wa mtu kufika mwisho wa mwezi Ada sh 30,000,15,000.10,000,nk mtoto hana au anakwambia hajapewa na mzazi, hivyo unajikuta unafundisha hata miezi mi3 wale watoto hawalipi ada unajikuta unafanya kazi kichaa mwisho unaamua ufunge tu tuition maana hamna jinsi.
Mwalimu akishakwambia hivyo,unagundua kitu kuwa huyu/hawa walimu Akili zao bado kuna kitu zimemiss,mtoto hana ada mzazi wake anajua kbsa hana ada lkn anaendelea kumwambia mtoto aende tuition tena wakati mwingine huko nyumbani akikutwa hajaenda tuition anachapwa fimbo kbsa ila huyu mzazi anamwambia mtoto aende tuition angali akijua Hajamlipia Ada ya tuition huu ni mwezi wa 3 sasa.
Kumbe shida si kwamba mwalimu hafundshi vizuri, wala si kwamba yule mwalimu kaacha kufundsha tuition ila unagundua sababu kubwa ya huyu/hawa wazazi kutoendelea kuwapeleka watoto tuition sababu kubwa ni ADA/PESA.
Sasa iko hivi mwalimu unatakiwa ufahamu kuwa wazazi wanahitaji sana watoto zao waende tuition,lkn mfahamu kuwa wazazi hao hao ADA za kuwalipia hawa watoto kwa mwezi zinawapiga chenga sometimes,sasa swali,Ufanyeje ili tuition yako iweze ku dumu kwa muda mrefu na wewe uendelee kupiga pesa miaka na miaka?
Katika maisha ya sasa hivi hamna kitu kinawashinda watu wengi kuanzia maskini mpk matajiri wakubwa na hata mimi CONTROLA ktk vitu vinanipa changamoto ni saving ya pesa,yani nimeshashindwa kbsa kuhifadhi pesa kama pesa(tuachane na hayo) sasa kama saving ni ngumu kwa kila mtu unafikiri hao wenye watoto wanaokosa ada unadhani hawapati hiyo 10k ya ada kwa mwezi? au unafkri n kweli kwa mwezi hawezi kukupa hiyo 30k yako? si kweli shda ni kwamba watu kukaa na pesa mbele yao hawawezi,sasa tunafanyaje ili kuipata pesa yao?
BADILISHA UTARATIBU WAKO WA UPOKEAJI ADA KWA WANAFUNZI WAKO
Unajua kila mwalimu kashakariri kuwa malipo ya tuition n kwa mwezi na hana option B yale malipo yanaposhindkana kulipika option yao kuu ni Kufunga tuition na kutafuta mishe zingine za kufanya.
Unajua kila mtu ana malengo yake ktk maisha ya sasa,ndio mana leo hii nikikwambia wewe njoo nikuajiri nikulipe 50,000 kwa mwezi utasema huwezi,hii n kwasababu 50k n ndogo ktk mahitaji yako,lakini 50k hyo hyo kuna mtu ukimpa inamtosha mpk na chenchi, (nataka kusema nini?)
Mwalimu unapokua unaanzisha tuition lazima uwe na malengo kwamba mimi naanzisha tuition ambayo nataka kwa mwezi inilipe mshahara wa 500,000 na si chini ya hapo,mwingine anaweza akasema nataka tuition ambayo kwa mwezi itanilipa 300k na si chini ya hapo,kila mtu ana malengo yake maana tumetofautiana.
Leo naomba tuanze na huyu mwalimu wa primary aliyejiwekea anataka malengo yake aingize 500k kwa mwezi kupitia tuition na si chini ya 500k,huyu mwalimu atafanyaje ili kuipata 500k yake (tupo na mwalimu wa shule ya msingi leo)
Nimesema utaratibu wa upokeaji ada lazima ubadilishwe,watu si wamezoea kulipa tuition kwa mwezi Sisi huyu mwalimu wetu naomba tuition Fee yake kwa kila mwanafunzi aichukue kwa siku ambayo ni sh.100 per Day/subject.
lazima ujiulize kwa sh.100 nahitaji wanafunzi wangapi kwa siku ili kufikia lengo langu la 500k kwa mwezi,huyu mwalimu ataenda kwa mpangilio ufuatao ili kukamilisha lengo lake.
Tumesema
somo 1 = 100tsh
Kwa hesabu zangu za chap chap hapa nahitaji wanafunzi si chini ya 70 ili kuweza kufikia lengo langu nililo jiwekea,sasa baada ya kujua hilo lazima ujiulize hawa wanafunzi 70 nawafundishia wapi? (tafuta mwenyewe utapowafundishia sio kila kitu utafuniwe)
Baada ya kupata eneo la kuwaweka hawa wanafunzi sasa tuje katika utendaji kazi,tumesema somo ni sh.100 ,hapa nahitaji wanafunzi 50 ambao hawa wanafunzi watasoma masomo matatu yani English,Hesabu na Science, na kwa kila mwanafunzi atakaesoma masomo matatu atapata bonus ya kufundisha "Kiswahili" BURE. (bonus subject)
Hapa maana yake
1=100
3=300
300 x 50 =15,000 (kwa siku)
15,000 x 30 = 450,000 (kwa mwezi)
Kwa wanafunzi wetu 50 wa kusoma masomo matatu kwa mwezi tunakunja 450,000 kibindoni,hapa bado hatujafikia lengo letu la 500k,sasa tuna wanafunzi wengine 20 pembeni waliobaki.
Hawa wanafunzi 20 ni wale wanafunzi ambao hawawezi kumudu gharama za masomo ma 3, hawa n wanafunzi ambao wako vizuri masomo yote kasoro 1,nk nk sababu zipo nyingi za hawa kusoma somo 1 tu.
hapa maana yake
1=100
20 x 100 = 2,000 (kwa siku)
2,000 x 30 = 60,000 (kwa mwezi)
Hapa tukija jumlisha 450,000 + 60,000 = 510,000 (tumevuka lengo letu),sasa hii 10k iliyozidi ina sababu zote za msingi kuzidi,haijazidi kimakosa maana yake ni kwamba ktk wale wanafunzi 20 ambao husoma somo 1 kwa siku,kuna wanafunzi 10 n waaminifu watakuja kila siku na kuna 10 ambao hawa leo atakuja kesho haji so hii 10 ita cover wale ma dodgers.
Kuna mtu nimemsikia huko akiuliza eti ntawapata wapi hawa wanafunzi 70 kwa mkupuo? aisee hamnaga biashara inaanza na wateja siku ya kwanza tu kwahyo kubali kuanza chini taratibu na kwakutumia hao hao unaowafundsha watakuletea wenzao wengi zaidi.
Faida za kutoza sh.100 kwa somo
- Ni rahisi kulipika kwa mzazi yeyote yule
- Ni rahisi kwa mtoto mwenyewe kujilipia hata kama mzazi hana hela
Unaweza kuona hawa wanafunzi 70 ni wengi sana,ila nataka ufahamu wanafunzi 70 kwa primary ni wachache sana,mliosoma kayumba international school mtakubaliana namimi kuwa darasani kwenu number ilikua inasoma ngapi.
Ushauri:
Hii project usiichukulie poa ukasema utaimudu peke ako ukajiona una fit nataka nikwambie kwa kuanza kweli unaweza imudu peke ako ila kama wazzi wataona matunda chanya ya ubora wa elimu unayowapa watoto wao nakuhakikishia utalemewa,tafuta Mwenzako muwe team ya watu wawili tu kisha changanyeni idea then ingieni mashuleni tangazeni kuwa mnafundisha tuition,Tafuteni posho kidogo ya kumpa MWALIMU MKUU wa kila shule mnayoenda kuomba mzunguke kutangaza huduma yenu.
mkizunguka shule 3 tu kuanzia darasa la 1 mpk la 7 sidhani kama mtaweza kukosa wanafunzi chini ya 200 kwa siku ya kwanza tu mmeanza hii huduma,si rahisi ila inawezekana mkiamua.HII NI PESA WAJOMBA (natamani mwenzenu ningekua mwalimu hamjui tu bahati mliyonayo).
Vilio za kukosa Ajira waachieni madaktari bana na ma pilot,hivi umesomea u pilot unaanzaje kujiajiri? labda ukajirushe juu ya dabo deka hadi chini sijui utajilipaje hapo,ACHENI BANA NYIE WALIMU shida yenu ni moja tu na wengi wenu hii ndio inawamaliza na mkiendekeza hili neno la "nitaonekanaje/watanichukuliaje/Aibu" mtakufa maskini.
Nawatakia utekelezaji mwema,namalizia kama nilivyoanza Mimi sio mwalimu na nimeleta hili kama story tu,tuambiane Je inawezekana au haiwezekani,msiniulize swali lolote kuhusu hiki nilichoandika,ninachoweza tu kuwajibu kama mtaniuliza ni hili swali?
Umeshawahi kuona mtu anafanya hivyo?
Jibu : Ndio nimewahi kuona tena ana Kijiji cha wanafunzi,sasa hivi ana Shule kabisa.