Mimi kwa sasa ni mtu mzima, Nimewahi kutaka kufulishwa nguo za watoto
Wengine wakiwa wamejikojolea. Nilikuwa hapo kwa mjomba wakati nikiwa
masomoni, shangazi aliniambia "Fua wa kusoma utakuwa wewe, we hapa ni yaya tu"
alikuwa ananiona mpole sana lakini siku hiyo nilimkata bonge la Ngwala ya Tanganyika jeki.
Baada ya kumnasa vibao viwili vitatu akaenda polisi kunishitaki. Mama mmoja jirani alifurahi
sana akanificha Temeke kwa Kaka yake. Mpaka namaliza nilikuwa naishi kwa huyo mzee.
Mwaka huu nimemnunulia Pikipiki kama shukurani.