Kwenu vijana mnaokula na kulala kwenu

Saguda47

JF-Expert Member
May 1, 2016
10,766
18,620
Assalam wanajamvi,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu,

Napenda kuwaongelea vijana/wanaume wanaoishi kwa wazazi, walezi, au ndugu yeyote.

Katika maisha Mara nyingi sisi wanadamu huwa ni watu wa kutotosheka ama kudhani kuna ofa fulani tunazostahili lakini hatupewi na wazazi, walezi ama ndugu zetu.

Hali hii hujenga dhana ya kulalamikia au kuwabeza wazazi, walezi au ndugu wanaotulea.

Kuna tabia zifuatazo ni mbaya sana kuzionyesha iwapo unaishi kwa ndugu zako au wazazi:-

1. Kulalamikia aina ya chakula.
Hapa utakuta wewe kijana unakaa kwenu au kwa ndugu zako unalalamika kuhusu chakula, Mara kila siku dagaa tumechoka ilihali hujui hata bei ya bamia gengeni. Elewa kuwa kulisha familia ni mzigo kwa mtoa matumizi, usilalamike iwapo wewe hutoi hata pesa ya unga.

2. Kugomea kazi, unakuta wewe umetoka kijijini ukaenda mjini kwa brother ako au mjomba kukaa, mama mjomba ako anakupa hata kazi ya kusafisha banda la kuku hutaki, kulima nyasi hutaki, unataka kushinda kwenye TV unaangalia series za wakorea tena zilizotafsriwa kiswahili.
Elewa kuwa upo kwa watu sio kwako fuata masharti, ukijenga mji wako utafanya huo uzembe wako uone utakavyokufa maskini.

3. Kuwa wa mwisho kurudi nyumbani, utakuta wewe ndio wa mwisho kufika nyumbani usiku, unaanza kuita watu waje kukufungulia geti kana kwamba we ndo baba mwenye familia, matokeo yake mjomba ako au shemeji yako anakuja kukufungulia geti/mlango, kama ni mstaarabu atakwambia jitahidi shemeji uwe unawahi ( hapo jiongeze).

4. Kutaka haki sawa na watoto wazawa wa familia.
Utakuta wewe upo tu nyumbani, ukitumwa kwenda sehemu unataka uende kwa gari, ukinyimwa unaanza kulalamika mbona Ali ( kijana mzawa wa familia) huwa anaendesha. Hapo jua upo for granted maana yake uwepo wapo ni gharama kwa familia husika, usijilinganishe na wenye haki katika familia hiyo.

5. Uvaaji,
Hapa utakuta kijana unakatiza sebuleni ukiwa na boksa tena bila wasiwasi, huu ni upumbavu wa hali ya juu, ukosefu wa staha ni dharau kubwa sana. Vaa vizuri bila kukwaza watu.

Nimalizie kwa kusema kuwa, maisha ni magumu sana ila kama unakaa kwenu huwezi jua hii shida, anayeijua ni yule anayehakikisha kila siku mnaenda chooni, usijifanye nunda kwenye kaya za watu fuata masharti na uwe mcheshi ujitume hakika utapendwa na kupewa vingi.
 
Ukitoka mkoa alafu unataka kuja dar dah afadhali fungasha nataka za kutosha fikia Gheto kwa mshikaji wako ila sio kwa ndugu aisee

Mbaya zaid ndugu yako ktk nyumba awe baba wa nyumba na sio mama wa nyumba HAKIKA UTAISOMA KIEBRABIA
 
Noma sana mkuu, bora ubaki kijijini tu ambako fursa zipo njenje mjini mambo yote yako budgeted
 
pole kwa wageni wa aina hiyo mkuu,atleast umetema nyongo,utaishi kwa amani sasa..
Hii mkuu ni tahadhari kwa vijana au wanaume wanaokimbilia mjini kwa ndugu zao bila kufuata shughuli maalumu.
 
1. Kama atakuwa anapika mlenda kila siku nitalalamika lakini moyoni.

2.Hata kama nimetoka kijijini ndo unipe kukuna nazi wakati kuna mabinti kibaooooooo!!!!?
3.Mimi nimetoka Mbinga, Njombe kwa Joto hili la Dar lazima niwe wa mwisho kuingia ndani.

4. Hapo sasa umezidi yaani nitoke kijijini nililie gari wakati siwezi kuendesha Acha dharau
ndugu.
5.Acha kujifanya mjuaji mkuu, hivi ni nani amewahi kukatiza hapo sebuleni kwako akiwa
amevaa boksa tu!? au unamaanisha hata ndani asivae? We sema tu hutaki wageni
kwenye nyumba ya baba yako.
 
Assalam wanajamvi

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu, napenda kuwaongelea vijana/wanaume wanaoishi kwa wazazi, walezi, au ndugu yeyote.
Katika maisha Mara nyingi sisi wanadamu huwa ni watu wa kutotosheka ama kudhani kuna ofa Fulani tunazostahili lakini hatupewi na wazazi, walezi ama ndugu zetu.
Hali hii hujenga dhana ya kulalamikia au kuwabeza wazazi, walezi au ndugu wanaotulea. Kuna tabia zifuatazo ni mbaya sana kuzionyesha iwapo unaishi kwa ndugu zako au wazazi:-

1. Kulalamikia aina ya chakula .
Hapa utakuta wewe kijana unakaa kwenu au kwa ndugu zako unalalamika kuhusu chakula, Mara kila siku dagaa tumechoka ilihali hujui hata bei ya bamia gengeni. Elewa kuwa kulisha familia ni mzigo kwa mtoa matumizi, usilalamike iwapo wewe hutoi hata pesa ya unga.

2. Kugomea kazi, unakuta wewe umetoka kijijini ukaenda mjini kwa brother ako au mjomba kukaa, mama mjomba ako anakupa hata kazi ya kusafisha banda la kuku hutaki, kulima nyasi hutaki, unataka kushinda kwenye TV unaangalia series za wakorea tena zilizotafsriwa kiswahili.
Elewa kuwa upo kwa watu sio kwako fuata masharti, ukijenga mji wako utafanya huo uzembe wako uone utakavyokufa maskini.

3. Kuwa wa mwisho kurudi nyumbani, utakuta wewe ndio wa mwisho kufika nyumbani usiku, unaanza kuita watu waje kukufungulia geti kana kwamba we ndo baba mwenye familia, matokeo yake mjomba ako au shemeji yako anakuja kukufungulia geti/mlango, kama ni mstaarabu atakwambia jitahidi shemeji uwe unawahi ( hapo jiongeze).

4. Kutaka haki sawa na watoto wazawa wa familia.
Utakuta we upo tu nyumbani, ukitumwa kwenda sehemu unataka uende kwa gari, ukinyimwa unaanza kulalamika mbona Ali ( kijana mzawa wa familia) huwa anaendesha. Hapo jua upo for granted maana yake uwepo wapo ni gharama kwa familia husika, usijilinganishe na wenye haki katika familia hiyo.

5. Uvaaji,
Hapa utakuta kijana unakatiza sebuleni ukiwa na boksa tena bila wasiwasi, huu ni upumbavu wa hali ya juu, ukosefu wa staha ni dharau kubwa sana. Vaa vizuri bila kukwaza watu.

Nimalizie kwa kusema kuwa, maisha ni magumu sana ila kama unakaa kwenu huwezi jua hii shida, anayeijua ni yule anayehakikisha kila siku mwaenda chooni, usijifanye nunda kwenye kaya za watu fuata masharti na uwe mcheshi ujitume hakika utapendwa na kupewa vingi.
wacha kunyanyasa ndugu kisa umesogea kidogo km hutak hao ndug zako waje wewe wambie,sio unakuja kuleta mipasho jf....kwahiyo mwanao ale favour bt ndugu umnyanyase.
poverty is problematic in Africa.
 
Hivi kuna mtu wa namna hii, yaani utake haki sawa na wazawa wa familia. itakua ajabu sana
Kuna vilaza wanadhani kuwa wana haki sawa na watoto wa wajomba zao au ndugu zao, wanataka haki sawa na ofa sawa.
 
Noma sana mkuu, bora ubaki kijijini tu ambako fursa zipo njenje mjini mambo yote yako budgeted
Sure mkuu

NAKUMBUKA first time natia mguu town nilipo chaguliwa advance huko

Kwanza nilikuwa nalala sitting room asubuh house girl anawai kudek ***** unabd na wewe uamke na pia kulala mpk WOTE walale..pale AZANIA NILISOMA WK MOJA NIKAHAMIA IYUNGA. Yaan tea asubuh ni vile vipandd viwili vya mkate wao wanashiba mie ilikuwa utab aisee

Nilipo kuwa nakuja tena kwa kuanza chuo nilikuwa nmejifunza..

WATU WA DAR WANAISHI MAISHA YA DHIKI KINOMA
.ALAFU SIFA ALIZO ZITAJA MKALI NI FACT

USIOMBEE NDUGU AWE MLOKOLE AU WA SWALA TANO
 
Hapo kwenye no 5 mkuu mimi huwaga sina habari yaani kukaa na boksa home au kwenda kusalimia ndugu waliojirani hapa kifua wazi
 
1. Kama atakuwa anapika mlenda kila siku nitalalamika lakini moyoni.

2.Hata kama nimetoka kijijini ndo unipe kukuna nazi wakati kuna mabinti kibaooooooo!!!!?
3.Mimi nimetoka Mbinga, Njombe kwa Joto hili la Dar lazima niwe wa mwisho kuingia ndani.

4. Hapo sasa umezidi yaani nitoke kijijini nililie gari wakati siwezi kuendesha Acha dharau
ndugu.
5.Acha kujifanya mjuaji mkuu, hivi ni nani amewahi kukatiza hapo sebuleni kwako akiwa
amevaa boksa tu!? au unamaanisha hata ndani asivae? We sema tu hutaki wageni
kwenye nyumba ya baba yako.
Naona jiwe la gizani limekufika mkuu, elewa kuwa sijaandika ili nijibizane na mtu, usitetee maana unayoona hayakuhusu wewe wapo yanaowalenga.
 
wacha kunyanyasa ndugu kisa umesogea kidogo km hutak hao ndug zako waje wewe wambie,sio unakuja kuleta mipasho jf....kwajiyo mwanao ale favour bt ndugu umnyanyase.
poverty is problematic in Africa.
Nazidi kujifunza as to why Tanzanians are probably poorest people in East Africa, yaani MTU kumhimiza afanye mema ni kumnyanyasa?
Bad mentality.
 
Back
Top Bottom