Kwenu mawifi, wake wa kaka zetu

Kwenu mawifi, wake wa kaka zetu

Hujui "wamekuoa"?????

Ila mie naona nimevunja rekodi ukweni

Naamka zangu saa mbili (na baridi la kule sasa)

Nikishapika na kula cha mchana narudi kulala (si nimepika na kuosha vyombo jamani????? )

Ila mama mkwe wangu bonge la mzungu.... aishi miaka mingi loh
Mi naamka saa mbili, napika uji wa watoto, nafua nguo zao, napika, jioni nawasha kuni napika aaah siku imeisha
 
Mawifi si hatuwachukii.Haya yote nadhani yanaletwa na kutojituma ipasavyo ili kujikwamua kiuchumi.Ukikuta kaka yao ametoka kimaisha basi wote wanataka kaka awasaidie.Atajigawaje jamani.
Ikitokea kaka amekwama oo wifi hataki tusaidiwe,kaka ana majukumu yake na yeye.
Afu mkumbuke watu wakishaoana wanakua mwili mmoja sio wawili tena mkituchukia mawifi basi mjue na kaka zenu hamuwapendi.
Huko vijijini tukija tukalala hadi sa nne na kwenyewe mnaona wivu.Basi mtuvumilie kwani hatukai mwaka mzima.
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Tatizo nyie mawifi zetu...

Kabla hamjaolewa...mnakuja tunawafahamu

Mnaonyesha upendo kumbe wa uongo

Mnafua

Mnapika

Mnashiriki kazi kupita kiasi

Mnamhudumia mama mkwe hadi anakuombea heri

Mkiolewa mnageuka miba

Kwa nini baadhi yenu ni miba kwenye familia mnazowakuta???

Hatuwakatazi kuvaa kunywa ni nyumba yako na mumeo

Tunahitaji ule upendo wa mwanzo uendelee

Baadhi yenu mnaingia kwenye familia kwa kujihami na attitudes

Vibaya hivyo
 
Mawifi mna tabu hivyo kumbe....kweli wanawake sio wa mchezomchezo akili zenu mnazijua wenyewe
 
Hahaha
Kila mwanamke mwenye kaka lazima awe wifi ake mtu...

Tuanze kujiangalia sisi kwanza maana hata sie tuna mawifi!!!!

Kwangu mie mawifi wananipenda hasa Emmyta, sijui ndo karibu mgeni.... Ila mke wa Kakangu nampenda ingawa twakutana mara chache sana hasa siku za siku Kuu tu nafikiri hili nalo huwa lasaidia pia

Hizo tabia zina wenyewe my wi tena walio wengi ni wale ambao macho na masikio yao yote yapo kwa kaka zao.

Hivyo kula ushibe my wi hii sio karibu mgeni ndio tulivyo siee. [emoji2] [emoji2].

Mi niko busy nahangaika na wa upande wa huku kwangu mana niliowapata sio wa mchezo mchezo.
 
Koh koh espy Nalendwa Evelyn Salt sijui na nyie mna meno au ndo vigego teh

Ukiwa na mawifi waswahili wasio na kazi, kazi kupiga umbea tu na kufuatilia maisha ya wifi yao na kaka yao basi wafwaaaa!!!

Kaka yako akishaoa utambue majukumu yameongezeka kwake na ana kazi ya kujenga kwake pia, mtasaidiwa lakini si kama mnavyotaka, bali kwa nafasi inayopatikana. Mkishatambua hilo basi walaa hakuna taabu. Kuna mawifi hawana jema, hata ufanyeje wataongea, weka nta masikioni fanya yaliyo ya msingi.
 
Mawifi na nyie si muolewe tu,msituonee wivu bwana,kumbukeni hata sisi tuna ma wifi wake za kaka zetu,ila kwa vile tupo busy na kulea ndoa na wanetu hatuna time.Ushauri oleweni ili msiwe na time ya kufuatilia wake za kaka zenu.
[emoji12] [emoji12] [emoji12] kweli dear waolewe na wao kila mtu awe na hamsini zake.
 
Nashukuru sina mawifi, mamaangu mkwe alizaa madume tupu. Yaan mashemeji wana raha nyie acheni tu, tena usipate wasomi mbona ndoa itaiona tamu
Ahahahaaaaaa hapo lazma unenepe, sasa usiombe ukutane na wasomi lazima uumie kichwa maa " ze ze kibao u know ooh mzungu kala mafenesi [emoji42][emoji42] argument kibao kuumizana kichwa tuu [emoji28][emoji28][emoji28]
 
Mawifi na nyie si muolewe tu,msituonee wivu bwana,kumbukeni hata sisi tuna ma wifi wake za kaka zetu,ila kwa vile tupo busy na kulea ndoa na wanetu hatuna time.Ushauri oleweni ili msiwe na time ya kufuatilia wake za kaka zenu.

Hahaa. Msg sent hiyo. Ila huwa wanakera hata uwabebe vipi hawabebeki lazima watakupa hila.
 
Ahahahaaaaaa hapo lazma unenepe, sasa usiombe ukutane na wasomi lazima uumie kichwa maa " ze ze kibao u know ooh mzungu kala mafenesi [emoji42][emoji42] argument kibao kuumizana kichwa tuu [emoji28][emoji28][emoji28]
We Ney wewe mbavu zangu mieee [emoji23] [emoji23]
 
Hizo tabia zina wenyewe my wi tena walio wengi ni wale ambao macho na masikio yao yote yapo kwa kaka zao.

Hivyo kula ushibe my wi hii sio karibu mgeni ndio tulivyo siee. [emoji2] [emoji2].

Mi niko busy nahangaika na wa upande wa huku kwangu mana niliowapata sio wa mchezo mchezo.
Hahaha
Pole my wii kazi unayo
 
Tatizo nyie mawifi zetu...

Kabla hamjaolewa...mnakuja tunawafahamu

Mnaonyesha upendo kumbe wa uongo

Mnafua

Mnapika

Mnashiriki kazi kupita kiasi

Mnamhudumia mama mkwe hadi anakuombea heri

Mkiolewa mnageuka miba

Kwa nini baadhi yenu ni miba kwenye familia mnazowakuta???

Hatuwakatazi kuvaa kunywa ni nyumba yako na mumeo

Tunahitaji ule upendo wa mwanzo uendelee

Baadhi yenu mnaingia kwenye familia kwa kujihami na attitudes

Vibaya hivyo
Sio kwamba tukiolewa tunakuwa miba hapana, hizo kazi nilizifanya kwa upendo lakini ndio isiwe sehemu ya kibarua changu nyumbani kwenu, mambo yamebadilika wifi yangu sasahivi nipo kwangu hizo kazi nitazifanya nyumbani kwangu nikija ukweni tutasaidiana tuu sio ndio mniachie kazi zote utadhan mimi ni mjakazi wenu hapana aiseeh, tuheshimiane mawifi zangu maana hata ninavyoishi na kakayenu ni kibarua tosha [emoji39][emoji39]
 
Back
Top Bottom