Kwenu mawifi, wake wa kaka zetu

Kwenu mawifi, wake wa kaka zetu

Na ukianza mazoea ndo tabu huanzia hapooo....
Ni kukaa mbali nao kwa kweeli
Kabisa, ukaribu nilishaupinga toka nakua kwakuona familia za watu wanavyosumbuana kisa huo uwifi, mawifi pande zote mbili ni tatizo katika familia. Either wewe ni mke au ni dada wa mume kifupi ni kuwa mbali na hao wifi zako, mkutane kwasababu maalum tuu unless otherwise utajuta kwanini uliolewa au kwanini kakaako alioa pale.
 
Mawifi si hatuwachukii.Haya yote nadhani yanaletwa na kutojituma ipasavyo ili kujikwamua kiuchumi.Ukikuta kaka yao ametoka kimaisha basi wote wanataka kaka awasaidie.Atajigawaje jamani.
Ikitokea kaka amekwama oo wifi hataki tusaidiwe,kaka ana majukumu yake na yeye.
Afu mkumbuke watu wakishaoana wanakua mwili mmoja sio wawili tena mkituchukia mawifi basi mjue na kaka zenu hamuwapendi.
Huko vijijini tukija tukalala hadi sa nne na kwenyewe mnaona wivu.Basi mtuvumilie kwani hatukai mwaka mzima.
 
Kakako akio jua Wifi wewe ni mtu wa kupita tu maana nawe ujiandae kua na mji wako badala ya kukaa na kubinanyana mapaja na kakako kwenye kochi kwa mbanano, mawifi mtulie muache meno ya Mbele kung'ata ng'ata ndoa za kaka zenu maana ufanyalo nawe utafanyiwa muda wako ukifika!! Ninachoshukuru wifi yangu ni kigego
[emoji6] [emoji6] [emoji6] [emoji6] [emoji6]
 
Ila sio wote wengine mawifi ni marafiki balaa

yote tisa nikorofishane na wengine lakini sio mzazi wa mme wangu. Maneno nengine ya mawifi porojo.
 
Mawifi na nyie si muolewe tu,msituonee wivu bwana,kumbukeni hata sisi tuna ma wifi wake za kaka zetu,ila kwa vile tupo busy na kulea ndoa na wanetu hatuna time.Ushauri oleweni ili msiwe na time ya kufuatilia wake za kaka zenu.
Ukweli mtupu
 
Halafu unaachaje kutafuta maisha yako,ukitegemea mtu mmoja awatoe umasikini au akusaidie na weww umekaa tu,anaetafuta anangalia watoto wake na uzee wake.
Hatulogwi ila tunaangalia utaokuwa uzee wetu.
Jukumu lipo kwa wazazi wasiojipanga tu,kwakuwa hawana nguvu.
Akina dada na wao wakachague wanaume wanaowafaa,siyo mizoga halafu shida tupate kina KAKA.
[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
Hua najiuliza sana wanaokaa kwa kaka zao,mie nna wifi 6 lakini kuonana nadra sana na hua mimi na Dada zangu hatuna tabia zakuwatembelea makwao wao ndio wanakuja nyumba ya Family ndio hua tunawaona sana ni watoto wa kaka zetu ndio most of the time tuko nao karibu na hiyo pia nadhani inasaidia kuepusha kelele,visafari vya kwa kaka kutwa,au ukakae miezi kwa kaka,mda wote unasubiria nini? mwenye nyumba anataka kuvaa kanga moja wewe wifi uko hapo wanataka kukaa waangalie TV na mumewe wewe ndio umejibweteka kwenye sofa tafran kwa watu sio sawa,ma wifi na nyie tulieni makwenuuuu,subiria ndoa zenu..
 
Mimi wifi asinitanie kwakweli ataita maji mma, kila nyumba inataratibu zake, kwa wakwe zangu wanataratibu zao na nyumbani kwetu wana taratibu zao hivyo hivyo na nyumbani kwangu na mume wangu tutakuwa na taratibu zetu, heshima itafuata mkondo wake, kwa atakayeona sifai kuwa mke wa kakaake aje anisaidie.
[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
Mi ni mke wa kaka bana sio mke wa familia
Hujui "wamekuoa"?????


Ila mie naona nimevunja rekodi ukweni

Naamka zangu saa mbili (na baridi la kule sasa)

Nikishapika na kula cha mchana narudi kulala (si nimepika na kuosha vyombo jamani????? )

Ila mama mkwe wangu bonge la mzungu.... aishi miaka mingi loh
 
Wanao walaumu wifi zao hawana shughuli za kufanya hivi niache kuwa bize na mishe zangu nibaki kila siku wifi sijui kafanyaje, tufanye kazi lawama hazijengi.
 
Mimi wifi asinitanie kwakweli ataita maji mma, kila nyumba inataratibu zake, kwa wakwe zangu wanataratibu zao na nyumbani kwetu wana taratibu zao hivyo hivyo na nyumbani kwangu na mume wangu tutakuwa na taratibu zetu, heshima itafuata mkondo wake, kwa atakayeona sifai kuwa mke wa kakaake aje anisaidie.
Toba walahi
 
Mawifi wengi ( ndugu upande wa wanaume) wanaboa.
Unakuta wifi anataka anyenyekewe kama vile yeye ndiyo Mume.
Pia kumridhisha binadamu ni kazi sana maana mazuri 1000 hufutwa na baya moja.
Nyie hamjui kaka yenu akishaoa majukumu yanaongezeka? Mnataka mchote tuu hela tusiwe na maendeleo ? Mwishowe mseme mwanamke nuksi?
Binafsi mawifi huwa nawachukulia watu wa kawaida sana.

Umeolewa?!
 
Back
Top Bottom