Kwenu Kina Baba........................! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwenu Kina Baba........................!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MwanajamiiOne, Sep 26, 2011.

 1. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #1
  Sep 26, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Wapendwa
  Ni matumaini yangu mlikuwa na weekend yenye Baraka.

  Mimi wiki hii MwanajamiiOne nimeianza kwa uchungu huku machozi yakinitiririka barabarani asubuhi wakati nakuja kibaruani. Kwenye taarifa ya habari iliyotangazwa kupitia Radio One. Mama mmoja huko Morogoro aliyekamatwa kwa kosa la kumpiga vibaya Mtoto wa Mume wake (Mtoto wa kambo). Taarifa hiyo ambayo ilisema mtoto huyo mwenye umri wa miaka 3 inasemekana amepigwa hadi kuvunjwa mkono na mguu huku akiachiwa majeraha sehemu za kichwa baada ya kupigwa mateke, kuangushwa chini huku akijipigiza sakafuni na kung'atwa kwa meno mwilini.

  Taarifa ilisema mtoto huyo (kwa mujibu wa majirani) amekuwa akichezea matezo hayo karibia kila siku pamoja na kufanyishwa kazi ngumu (Mtoto wa miaka 3??!!). Aliambulia kupigwa (tena kwa kuchangiwa na mama huyo na mwanae) pale anapotumwa kitu mfano mwiko akakosea (Mtoto wa Miaka 3!!).

  Sitaki kusema mengi lakini kwa kifupi, kina Baba ambao mna watoto wenu ambao hamuishi na mama zao, NINAWAOMBA muwe japo na kajitabia ka kusoma alama za nyakati. Ni kweli kuwa si mama wote wa kambo ni wabaya lakini you never know just take time kuchungua mazingira.

  Ningetamani kweli kujua namna ya kufanya hili liwe kweli lakini sijui, yaani nashuindwa kuwaza kabisa.
  KUWENI tu MAKINI.

  MBARIKIWE SANA KINA BABA NA MAMA WAZAZI/WALEZI WENYE MIOYO YA UPENDO KWA WATOTO WAO HATA KAMA HAWAJAWAZAA WAO.
   
 2. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,095
  Likes Received: 24,107
  Trophy Points: 280
  Ahsante sana mjukuu mtiifu

  Tutalifanyia kazi.

  Na nyie wanawake acheni "ROHO MBAYA". Mtoto wa mwanamke mwenzio ni MWANAO - Mpende akupende!
   
 3. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,753
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Pole sana kwa uchungu Mj1,na sisi wababa tumeuchukua ushauri wako kwa uzito mkubwa_lakn ni bora zaidi pia unge wa adress wamama kwani wao ndio wafanyaji wakubwa wa vitendo hivi vya kinyama,...wewe kama mama mwenzao ungechukua nafasi hii kuwaomba waache kuwatesa watoto ambao hawaja wazaa,....ila inasikitisha na kuuma sana
   
 4. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  oh my oh my !!

  huu ukatili sijui utaisha lini, na sijui kwanini majirani ambao wako karibu hawaripoti vitendo hivyo, mtoto wa miaka 3 tena si wako unampigia nini jamani ? kwanini usimshawishi mumeo amrudishe kwa mama yake ?

  yaani kila kukicha namshukuru Mungu kunipa uhai ili niendelee kuwaangalia wanangu, napata shida nikiwaza kuna mwanamke mwingine atawaangalia kama mimi ( yaani sio wanawake wote wabaya lakini haya mambo ya udhalilishaji yanavyoongezeka inatisha )

  mwanajamii one, it has always been my intention to fund causes for abused children and housegirls, when we have time out of our busy schedule we can contribute back to the society, niPM au any interested party can PM me...tuangalie tu hata tukisaidia mmoja si haba
   
 5. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #5
  Sep 26, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Babu na Mjomba IGWE nimewaelewa lakini lengo na madhumuni yangu kuwalenga nyie nina maana kuwa mwanamke mwenye roho ya kishetwani kama huyu hata nikimwambia nitakuwa ninampigia mbuzi gitaa na isitoshe threads nyingi za jambo hili zilikuwa zinawalenga wao so nimejiona kama vile sina jipya la kuwaeleza wanawake wenzangu niwageukie kina Baba.

  Imagine huyu alikuwa anakanywa na majirani na mashosti zake kuwa utamwuua mtoto wa watu anawajibu kama mna uchungu naye mchukueni mkamlee ninyi!! (Mtoto wa miaka 3?!!) jamani. Kitendo hiki kusema ukweli kimenifanya kwa mara ya kwanza maishani mwangu nione aibu kuzaliwa mwanamke (Sijuti). ............ Hivi kweli nawezapita kifua mbele kuwa mie ni mwanamke ilihali kuna wanawake wenye roho za kikatili kuliko wanyama?

  Wewe baba mwenye mtoto wako anayeishi na mama mwingine, huwa unachukua jukumu gani kuhakikisha kuwa anapata huduma, malezi na upendo kutoka kwa mama yake wa kambo? au unaamini tu kuwa analelewa vizuri kwa kuwa tu ukirudi unamkuta/ona mama huyo anamchekea au kujifanya anamkumbatia? ni mbinu gani mtu anawezatumia ili kulijua hili??
   
 6. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #6
  Sep 26, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  3yrs old anapigwa na watu wawili. Majirani wanajua, wanashndwa kuchukua hatua!!!. Kina mama punguzeni roho mbaya kwani huyo naye ni mtoto sawa na wako.
   
 7. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135

  Igwe ni kweli kabisa,

  kwanza nakushukuru kwa kuacknowledge kuwa you have a part to play, zaidi sana akina mama wa jinsi hii sidhani hata kama hapa JF wanapitapita, lakini nina uhakika wanaume wengi walio hapa ( baadhi ) wana watoto 'wa ujanani' etc kama wewe ni mwanaume unasoma hapa, na unakaa na mwanao, naomba umwangalie vizuri ama kama sote tunajua ukatili unapofanyika tujitahidi kuripoti na kuminimize situation

  juzi wakati nakuja kazini asubuhi nimepita njia panya za mwananyamala huko katikati, kukwepa foleni, njiani nikakuta mwanamke amefunga kanga moja anamtandika mtoto mdogo sana kwa kosa la kupoteza shs 200, kwavile tulikuwa tumesimama muda mrefu nikawa naangalia tu kama wengine, lakini akina mama wanaochoma mihogo hapo pembeni wakawa wanasema, 'ndio hivyo tena mtoto anapewa kipigo kwa vile si wake wakati wezi ni wanae' kwakweli sikuvumilia zaidi nilimpatia huyo mama shs 1,000 nikamwambia mwache mtoto aende shule jamani ni asubuhi unamchapa sasa hivi atachapwa tena kuchelewa, ok huyo mama aliichukua kwa kubetua midomo akaingia ndani akamwambia na uende shule mwana laana we!! kinanisikitisha kuwa majirani wanaona na watu hatuchukui hatua najua akirudi shule pengine atachapwa zaidi kwa kumdhalilisha mama mbele za watu hata sijui ?
   
 8. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #8
  Sep 26, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kinamama hebu acheni ukatili wa aina hii.
  OTIS.
   
 9. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #9
  Sep 26, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mara nyingi familia km hiyo baba huwa amekaliwa na mama (mama ndo kila kitu ndani ya nyumba na wamama hao huwa ni jst house wives.......... Thats my experience and point of view though......... Mtoto anaweza pigwa hata mbele ya baba na kunyimwa hata chakula.....
   
 10. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #10
  Sep 26, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,753
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Good woman,...Mungu atakuzidishia mara saba sabini
   
 11. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #11
  Sep 26, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
   
 12. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #12
  Sep 26, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,753
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  True_kwa sisi wafuasi wa morden and balanced mfumo dume ni nadra sana kufanyiwa vitendo vya kifedhuri kama hivyo,...tatizo lipo kwenu mliosoma ng'ambo hizo masters zenu
   
 13. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #13
  Sep 26, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  MJ1 thanks for such a positive take.......ni ushauri mzuri sana kwetu

  Hili kimsingi linaashiria sisi wakina baba kujitenga pembeni na kutokuwa na wakati na watoto wetu na wakati mwingine kuwa wapuuziaji wa mambo ya msingi. Nasema hivi kwa sababu sidhani kama huyu baba hakuwa na taarifa ya kuteswa kwa mtoto wake awali 9kama majirani wanavyosema kuwa ni jambo lenye kutokea mara kwa mara) na hii inamaanisha alikuwa mpuuziaji lakini inaonekana pia mdhaifu kuchukua maamuzi yenye manufaa....

  Inaumiza hasa tena kwa mtoto wa miaka mitatu
   
 14. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #14
  Sep 26, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  Dah!.......
   
 15. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #15
  Sep 26, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,095
  Likes Received: 24,107
  Trophy Points: 280
  Nimejikuta nimemkumbuka Chetuntu ghafla......... sijui kale ka handsome kake katalelewa na mama wa kambo?

  Inauma sana aisee!

  RIP Chetuntu.
   
 16. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #16
  Sep 26, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mbaya sana hii.
  Najiuliza kuhusu authenticity ya hii habari, maana ni ngumu hata kumeza!...Inawezekana kweli kuna viumbe katili hivyo?
  Mbona mtoto ni mtoto tu jamani?...
  Nimeboreka sana, na siku yangu kuharibika!
   
 17. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #17
  Sep 26, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,276
  Trophy Points: 280
  Una watoto wangapi??wewe
   
 18. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #18
  Sep 26, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Na mimi siku yangu ishaharibiwa na hii thread ya kusikitisha.
  Wababa wajitahidi kupata muda wa kuzungumza na watoto wenu muone kama mambo yapo sawa.
   
 19. Kabakabana

  Kabakabana JF-Expert Member

  #19
  Sep 26, 2011
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 5,559
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  too sad wanawake wengine bhana hivi hambebi mimba na nyinyi?imagine angekuwa ni mwanao kafanyiwa hivyo how would u feel?
   
 20. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #20
  Sep 26, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mwanangu ndio katimiza miaka mitatu mwaka huu, kwa umri huo kweli anaweza kufanya kazi, labda kama ni wa kike lakini wa kwangu sijaona kama anamudu kufanya kazi zaidi ya kubadilisha channel za TV tu.
  Jambo hili sio kwa mama wa kambo tu, hata mama wazazi huwatesa sana watoto zao utadhani hawakutoka mkatika matumbo, mie kule Kibaha nimeshuhudi mtoto alipoteza shilingi mia moja! lakini alichomwa mikono yote miwili kwa moto baada ya kufungwa na nailoni na kumwagiwa mafuta ya taa, yule mtoto alipoteza vidole vyake vyote, ilikuwa ni kwenye miaka ya mwanzoni mwa 90. jambo lile mpaka leo linaisumbua akili yangu.
   
Loading...