Kwendeni zenu huko 'Wanafiki' wakubwa nyie, Dk. Kimei yuko sahihi tena 100%

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Kauli ya Mbunge wa Vunjo, Dk Charles Kimei kuwa wachaga wanapenda biashara ya magendo inaonekana kuchafua hali ya hewa ambapo kikundi cha wazee kutoka jimboni humo kimejitokeza na kutoa tamko kali dhidi yake.

Katika tamko hilo, wazee hao wa kichaga wamelaani kauli hiyo na kwamba wanachukulia kauli hiyo kama matusi kwao na kumtaka Dk Kimei ajitokeza hadharani na kufuta kauli hiyo katika kumbukumbu rasmi za Bunge.

Taarifa: mwananchi_official

KEROZENE ninaungana tena kwa 100%.
 
Huyu Dr Kimei ana shida aisee, majuzi mbele ya Mhe SSH ametoa kauli ya ajabu eti watu wsruhusiwe kufanya shughuli za kibinadamu kwenye half mile strip kule juu Kilimanjaro NP, Mhe rais akampinga hadharani na kumkumbusha kwamba hali huko juu milimani ni mbaya na mabarafu yanaisha. Pia Dr Shoo akamshangaa mbunge huyo!! Pia amejichanganya kwenye issue ya Moshi kuwa jiji yeye anazungumzia sijui kupata Halmashauri nyingine. Atulie akipange mazee..
 
Nilikua namuona yuko smart,kumbe ni empty
 
Hizi habari za kutaja makabila siyo njema kwa mtu mwenye elimu, wanaofanya biashara Kilimanjaro siyo wachaga peke yao, wapo makabila mengine pia, habari za makabila karne hii zisihusishwe na siasa wala ustawi wa watanzania, tuwaache watanzania tusitafute gia za kuwagawa for political gains, hatutafika tuendako
 
watu wote wanaoishi maeneo ya mipakani hufanya magendo.....inawezekana hata babake au mmoja wa nduguze alipitia huko.....kwa maana hiyo anawashitakia polisi........polisi wote waanaoishi kanda hizo.....holili, taveta, mkuu -- mpaka tarakea - kamwanga...ni matajir na vijitambi vya magendo......wengi wakihamishwa vituo wanaacha kazi........anyway YEYE KESHASHIBA.......
 
Wazee wamesara kwa kuharibiwa dili zao..yaani Dr Kimei wanammind kwa kuwa mkuda.
 
Hata km atakuwa sahihi. Unafikiri ndiyo maisha yako yatakuwa mazuri?
Unaanzaje kulipa kodi kwa nchi yenye umeme na maji ya mgao?

Back
Top Bottom