Kwenda Mpirani au kutembelea mafuriko?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,739
Likes
7,521
Points
280

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,739 7,521 280
KUVUSHWA%2BMTONI.JPG


DARAJA%2BKUBOMOKA.JPGWakati wananchi wake hapo juu wanahangaika pa kula, kulala na afya zao!...

Kikwete%2Bna%2Bwachezaji%2Bna%2Bvioongozi%2Bwa%2Btimu%2Bya%2BIvory%2BCoast.JPG

(Picha zote toka kwa Michuzi)

Hoja imejengwa humu na watetezi wa "majanga ya kitaifa hayazuii Rais kwenda kuburudika" na kuwa tukiwa na matatizo makubwa haina maana Rais hafanyi shughuli muhimu 'za' kitaifa. Watetezi hawa wametetea kwa nguvu mno kuwa ilimlazimu Rais Kikwete kwenda mpirani ili kuonesha uongozi na kuwa ilikuwa ni sehemu ya kazi yake!

Katika hili ninawaita hawa ni watetezi wa uzembe na mazingaombwe ya siasa na ulaghai wa uongozi kwa sababu ningewaita vingine ingekuwa ni heshima wasiyostahili!

Nilikuwa mtu wa kwanza kutoa taarifa ya mafuriko makubwa siku ya Krismasi na kusema wazi kuwa "maafa yahofiwa". Nililiamsha tena taifa langu na kuliasa kujiandaa kama nilivyofanya zaidi ya mwaka mmoja uliopita katika makala ya "taifa lisiliojiandaa kwa majanga limejiandaa kwa maafa". Nilitegemea labda wangeamka!

Wakati watu wetu wanakosa pa kula na kulala, wakati watu wamekufa, wakati reli ya kati imechomolewa na usafiri kwenda bara kwa njia hiyo unakomeshwa kwa kiasi kikubwa hadi Aprili, watawala wetu wamekaa na kupiga picha na kina Ivory Coast katika kampeni ya "kulitangaza taifa".

Zaidi ya wiki mbili zinapita sasa Rais Kikwete hata kwenda kuwajulia hali wananchi wake huko Kilosa, Kongwa, Ruvuma n.k hajafanya hivyo kwa sababu yuko katika shughuli muhimu ya kitaifa!

Cha kushangaza (kama ilivyokuwa wakati akifunga 200 kwenye hotuba yake ya kuuaga mwaka 2009 hakuzungumzia lolote juu ya mafuriko na hali ya ndugu zetu hawa. Leo hii Msalaba Mwekundu wanahitaji karibu miliooni 300 kupeleka msaada; Leo hii Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa serikali imeionyoshea kidole Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuwa wazembe kila maafa yanapotokea!

Niiteni mlalamishi lakini sababu za yeye kutokugombea tena zinazidi kuongezeka.

Yaani wiki mbili zinapita...na anamuda wa kwenda mpirani, kuandaa dina, na bila ya shaka kufanya mambo mengine "muhimu".. it reminds me of another president in another country during a hurricane named Katrina!

Mwenyewe anaridhika baada ya kutoa statement hii kupitia kina Salva;

Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,ametuma salamu za pole kwa wakuu wa mikoa minne ambayo imekumbwa na maafa yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.
Aidha, Rais Kikwete amepongeza jitihada zinazofanywa na uongozi katika mikoa hiyo kukabiliana na maafa yanayosababishwa na mvua hizo.


Rais Kikwete ametuma salamu hizo za pole leo (jana) Jumanne, Desemba 29, 2009, kwa wakuu wa Mikoa ya Dodoma, Morogoro, Ruvuma na Rukwa.


Katika mikoa hiyo, baadhi ya watu wamepoteza maisha kutokana na mafuriko, wengine wamejeruhiwa kutokana na radi, na kumekuwepo na upotevu wa mali, na mamia ya watu kukosa mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kuezuliwa na upepo ulioambatana na mvua kubwa.

Katika salamu hizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhandisi Dkt. James Alex Msekela, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Luteni Kanali (mst) Issa Saleh Machibya, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mheshimiwa Christine G Ishengoma, na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mheshimiwa Daniel Ole Njoolay, Rais Kikwete amesema kuwa amesikitishwa na upotevu wa maisha, upotevu wa mali na hasara ya watu kuezuliwa nyumba zao.

“Nimesikitishwa na kuhuzunishwa na maafa ambayo yameambatana na mvua zinazoendelea kunyesha katika Mkoa wako. Nakupa salamu za pole wewe binafsi Mkuu wa Mkoa, na kupitia kwako, natoa mkono wa pole kwa watu wote waliopatwa na maafa kutokana na mvua hizo,” amesema Rais Kikwete katika sehemu ya salamu zake kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kanali Machibya.
Rais ametuma salamu zenye ujumbe kama huo kwa Mhandisi Dkt. Msekela, Mheshimiwa Ishengoma na Mheshimiwa Njoolay.


Katika Wilaya ya Kongwa ya Mkoa wa Dodoma watu 220 hawana mahali pa kuishi wakati idadi ya wasiokuwa na mahali pa kuishi katika Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro imefikia 2, 152 kufuatia nyumba zao kuezuliwa ama kuharibiwa na upepo ama mafuriko. Katika wilaya hiyo hiyo ya Kilosa, nyumba 922 zimefurika maji.

Katika Mkoa wa Rukwa, watu 27 wamelazwa katika Kituo cha Afya cha Kakese baada ya kuwa wamepigwa na radi katika tukio ambako mtu mmoja amepoteza maisha.

Katika salamu zake, Rais Kikwete amewaelekeza wakuu hao wa mikoa kuendelea kuchukua hatua za dharura kukabiliana na maafa yanayotokana na mvua hizo na kuahidi kuwa Serikali yake iko pamoja na wananchi waliopatwa na maafa katika mikoa hiyo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
29 Desemba, 2009

 

Recta

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2006
Messages
854
Likes
3
Points
35

Recta

JF-Expert Member
Joined Dec 8, 2006
854 3 35
Mkuu, kwakuwa alishafika uwanjani, mwache tu amalizie na kupiga picha.

Wiki mbili hajachukua hatua? Duh, labda kinachosubiriwa ni watu kusahau.

Hii inanikumbusha idadi ya celebrities ambao wanalitangaza Taifa. Steven Sieger, .... na sasa Didier Drogba. We are getting somewhere.
 

Kakalende

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2006
Messages
3,256
Likes
40
Points
135

Kakalende

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2006
3,256 40 135
Mkuu Mwanakijiji, kwa taarifa yako wapenzi wa kandanda tupo wengi sana humo na ajenda ya kumsakama mkulu kuhusu kabumbu haitaungwa mkono.

Mbona skandali ziko nyingi tu, si mtafute hoja nyingine?
 

MtazamoWangu

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2009
Messages
313
Likes
6
Points
35

MtazamoWangu

JF-Expert Member
Joined Apr 25, 2009
313 6 35
Hoja ipo Hapa, mi nadhani huyu jamaa hana washauri wenye busara, hata wakati wa milipuko ya mbagara ilimchukua muda mpaka kutembelea au kutoa tamko, na bila hata bunge kustka.....
lazima JK ajue anatakiwa ajijenge sana ndani sio nje...hiyo kazi aliyofanya inawenyewe....au hajui kazi yake????
 

nguvumali

JF Bronze Member
Joined
Sep 3, 2009
Messages
4,891
Likes
181
Points
160

nguvumali

JF Bronze Member
Joined Sep 3, 2009
4,891 181 160
Rais JK hana washauri viona mbali, hana vipaumbele, kwake yeye kujitafutia umashuhuri kwa vitu vya hovyohovyo na rahisi rahisi ndio apendavyo.
kweli inafikirisha sana , nnchi ipo kwenye mahangaiko kule Kilosa,Dodoma na LINDI lakini inaonekana kama si tatizo zito, Train imekwama, barabara zimesambaratishwa kweli vipaumbele vya raisi wetu ni viini macho na ujiko wa hovyohovyo.
 

Utingo

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Messages
7,197
Likes
260
Points
180

Utingo

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2009
7,197 260 180
NIWAKUMBUSHE KUWA hATA MWINYI ALIKWENDA KILIMANJARO HOTEL KUMWONA TSHALLA MWANA WAKATI MADAKTARI WALIKUWA WAMEGOMA PALE MUHIMBILI NA WALA HAKUJALI. IT IS A PRESIDENTIAL TRADITION HAPA BONGO. INGEKUWA NCHI NYINGINE INGESHATANGAZWA MBIU YA HALI YA HATARI NA MAJESHI YANGESHAPELEKWA KUSAIDIA.
SIJUI HATA MBUNGE WA HUKO (MKULO) KAMA AMESHAFIKA ENEO LA MAAFA.
 

Kidatu

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2008
Messages
1,494
Likes
23
Points
145

Kidatu

JF-Expert Member
Joined Jun 11, 2008
1,494 23 145
Uzalendo na mapenzi kwa nchi yetu ni jukumu la kila moja wetu na wala si JK pekee yake. Wewe MMJ umefika huko Kilosa kuwapa pole wahusika?, au umepeleka kitu chochote cha kuweza kuwasaidia wahusika?.
Serikali ya JK imepeleka misaada na watu mbalimbali ili kuweza kuwasaidia waliokumbwa na maafa hayo. Jamani JK ana wasaidizi katika kila fani, hawezi kufanya kila kitu yeye mwenyewe. Ametuma ujumbe wa watu mbalimbali huko Kilosa, amepeleka misaada ya kuanzia na mingine mingi iko njiani kwenda huko. Nilikuwa nategemea MMJ ungehamasisha wana JF kutoa michango ya kuweza kuwasaidia wana kilosa na wewe mwenyewe ungefika huko na kuwapatia michango hiyo, labda kuanzia hapo ungeweza kupata jukwaa la kumtupia lawama JK lakini si vinginevyo.
 
Joined
Nov 11, 2008
Messages
782
Likes
8
Points
0
Joined Nov 11, 2008
782 8 0
Wewe ndio umejichokea
Rais JK hana washauri viona mbali, hana vipaumbele, kwake yeye kujitafutia umashuhuri kwa vitu vya hovyohovyo na rahisi rahisi ndio apendavyo. HIVYO NDIVYO VIPAUMBELE VYAKE


kweli inafikirisha sana , nnchi ipo kwenye mahangaiko kule Kilosa,Dodoma na LINDI lakini inaonekana kama si tatizo zito, Train imekwama, barabara zimesambaratishwa kweli vipaumbele vya raisi wetu ni viini macho na ujiko wa hovyohovyo.
YAANI nyie mjinome na DRODBA yeye aende kwenye matope THUBUTU YENU
 

Masaki

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
3,468
Likes
177
Points
160

Masaki

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
3,468 177 160
Rais JK hana washauri viona mbali, hana vipaumbele, kwake yeye kujitafutia umashuhuri kwa vitu vya hovyohovyo na rahisi rahisi ndio apendavyo.
kweli inafikirisha sana , nnchi ipo kwenye mahangaiko kule Kilosa,Dodoma na LINDI lakini inaonekana kama si tatizo zito, Train imekwama, barabara zimesambaratishwa kweli vipaumbele vya raisi wetu ni viini macho na ujiko wa hovyohovyo.
Hivi kwanini kila akikosea mnakimbilia kulaumu washauri wake badala ya yeye mwenyewe! Hivi ukimshauri jambo bosi wako halafu akaenda kinyume na ushauri wako utafanyaje? Utamfokea? Ina maana yeye mwenyewe hana busara ya kutosha kupambanua mambo?

Kula lanchi na wachezaji ni sehemu tu ya kazi zake za kila siku. Huu ni mwaka wa tano sasa anamalizia ngwe yake ya kwanza. Kikubwa alichofanya ni kuwaruhusu mseme mpaka mchoke!!! Uhuru wa kutoa maoni!!
 

Kidatu

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2008
Messages
1,494
Likes
23
Points
145

Kidatu

JF-Expert Member
Joined Jun 11, 2008
1,494 23 145
Rais JK hana washauri viona mbali, hana vipaumbele, kwake yeye kujitafutia umashuhuri kwa vitu vya hovyohovyo na rahisi rahisi ndio apendavyo.
kweli inafikirisha sana , nnchi ipo kwenye mahangaiko kule Kilosa,Dodoma na LINDI lakini inaonekana kama si tatizo zito, Train imekwama, barabara zimesambaratishwa kweli vipaumbele vya raisi wetu ni viini macho na ujiko wa hovyohovyo.
Raisi hatembelei sehemu kwa kukurupuka. Kuna utaratibu maalumu. Usalama wa Raisi ni kitu muhimu, hivyo kuna watu wanatumwa mapema kuangalia na kuandaa usalama wa Raisi kabla hajatembelea sehemu. Na ndiyo maana unaona mara nyingi Raisi anakuwa wa mwisho kufika sehemu kama hizo.
 

nguvumali

JF Bronze Member
Joined
Sep 3, 2009
Messages
4,891
Likes
181
Points
160

nguvumali

JF Bronze Member
Joined Sep 3, 2009
4,891 181 160
Hivi kwanini kila akikosea mnakimbilia kulaumu washauri wake badala ya yeye mwenyewe! Hivi ukimshauri jambo bosi wako halafu akaenda kinyume na ushauri wako utafanyaje? Utamfokea? Ina maana yeye mwenyewe hana busara ya kutosha kupambanua mambo?

Kula lanchi na wachezaji ni sehemu tu ya kazi zake za kila siku. Huu ni mwaka wa tano sasa anamalizia ngwe yake ya kwanza. Kikubwa alichofanya ni kuwaruhusu mseme mpaka mchoke!!! Uhuru wa kutoa maoni!!
Unajua Urais ni taasisi, JK tunaelewa sikuhizi kiwango chake cha kufikiri, na tuliambiwa alipoenda kule visiwani akipita hadi kwenye mabembea ya JAMAIKA alipimwa akili....rejea mazungumzo yake na waandishi wahabari pale airport .."! sasa tangu hapo tumegundua kua Mheshimiwa upstairs..........lipo tatizo. sasa jukumu la kuendesha nchi kwamba mkuu afanye nini na nini tunaamini wasaidizi watamshauri na kinachoshangaza kua kama hatilii maanani ushauri wao kwanini hawaachii ngazi /????? lipo tatizo la mkuu kufikiri na kutenda mambo katika wakati wake.
Haki ya kuzungumza ama kujieleza ni haki yetu ya kuzaliwa hakuna wakuchukua japo wanaweza kutudhulu ila ukweli hauzuiwi kwa mtutu wa bunduki na hata ukiukimbia daima utakutana nao mbele unakusubiri kwa hamu.
 

SMU

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2008
Messages
8,139
Likes
2,495
Points
280

SMU

JF-Expert Member
Joined Feb 14, 2008
8,139 2,495 280
Mzee Mwanakijiji,

Katika kipindi cha maombolezo ya kitaifa Rais hufanya kazi muhimu na za lazima tu na zenye manufaa kwa taifa (kama mpira nk). Hawezi kwenda kuangalia (kuona kwenye kwenye TV inatosha!) maafa na kuwapa pole wahanga wa mafuriko katika kipindi hiki ambapo taifa lipo katika maombolezo ya msiba mzito (kama alivyotangaza) wa mpigania uhuru na simba wa vita Mzee RMK!

Huko kwenye mafuriko ametuma wawakilishi kwa sasa. Maombolezo yanaisha leo (kama hesabu hazijanitupa mkono!), hivyo tutegemee kuanzia kesho pengine ataanza kujishughulisha na majukumu ambayo sio muhimu sana kwa taifa likiwemo hili la mafuriko.
 

Forum statistics

Threads 1,189,736
Members 450,798
Posts 27,645,707