Kweli Yanga mnamuacha Kiiza?

kuna tetesi kuwa niyonzima kapewa $50,000 ndo maana kiiza naye anatikisa kiberiti kutaka kiasi hicho!

hata mimi nina mtizamo kama wako mkuu, hizo $35,000 alizotengewa bado ni nyingi mno, angepewa tu 25,000, akikataa waachane naye. akikaa kule ngasa na huku msuva then katikati tegete na bahanuzi huku wakilishwa na niyonzima mbona fowadi nzuri tu hiyo
Bahanuzi ni mchezaji wa kagame cup tu
 
Nasikia kashasaini mpaka 2017..

Hivi Tanzania kuna mchezaji alishawahi kusaini mkataba wa miaka minne kweli? Huwa naona wengi ni miaka miwili na wachache sana miaka mitatu, kama ni kweli kasaini hadi 2017 anaweza kuwa wa kwanza kusaini miaka minne lakini nadhani hii itakuwa biashara tu ya magazeti tena leo siku yenyewe jmosi washabiki wengi wa Ndala mpo nyumbani lazima mnunue sana hilo gazeti kumbe hata hajasaini, unacheza na waandishi wa bongo wewe hasa wa michezo hawana tofauti na wa Shigongo.
 
Maskhara hayo kaka.............
 
Kiiza nani bwana!toa huko profeshno uchwara sasa kina msuva,javu,kondo na wengineo tutawaonea wapi?ndio maana timu letu la taifa linakuwa kama TAHITI tuwape nafasi wachezaji wa ndani bwana
 
Kiiza nani bwana!toa huko profeshno uchwara sasa kina msuva,javu,kondo na wengineo tutawaonea wapi?ndio maana timu letu la taifa linakuwa kama TAHITI tuwape nafasi wachezaji wa ndani bwana

Kashasaini Jangwani, na alimtungua Juma K.Juma.
 
Kiiza aachwe, siyo tishio kama ilivyokuwa kwa Okwi. Mimi Yanga damu nikisikia Okwi yumo nilikuwa nakosa amani, tangu aondoke ni raha tupu. Hebu tuwe wakweli ni Wanasimba wangapi wanakumbwa na hofu wakimwona Kiiza yuko uwanjani? Hana hadhi ya kuichezea Yanga, kiwango kimeshuka, ni heri ya Ssentongo kuliko Kiiza.
Kiiza ni mchezaji wa misifa sana.................................ukweli aliousema Maximo ni dhahiri alikua mvivu sana na anaonekana anapenda totoz ndio maana hajitumi uwanjani, namsikitikia sana Tambwe kuondoka Simba
 
SIKU chache baada ya Yanga kumtema, Hamis Kiiza na nafasi yake kupewa Mliberia Kpah Sherman, mchezaji huyo raia wa Uganda ameibuka na kusema ipo siku timu hiyo itaukumbuka mchango wake kikosini.

Kwa muda mrefu Kiiza hakuwa na maisha mzuri ndani ya kikosi cha Yanga chini ya Kocha Marcio Maximo akikosa nafasi kikosi cha kwanza na awali alinusurika kutemwa mwanzoni mwa usajili, lakini akaachwa siku chache kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa.

Hata hivyo, Maximo naye amesitishiwa mkataba wake pamoja na msaidizi wake Leonardo Neiva na kiungo raia wa Brazil, Emerson Roque ambaye amempisha Amissi Tambwe.

Kiiza ambaye kwa sasa anatajwa kujiunga na URA ya Uganda, aliliambia Mwanaspoti kuwa ipo siku Yanga itaukumbuka mchango wake katika timu na itakuwa imechelewa kumrejesha kwani atakuwa amepiga hatua nyingine kisoka kwani anaamini ana kiwango kizuri cha kuendelea kucheza soka kwa mafanikio.

“Bado naamini nina uwezo mkubwa, nimekaa Yanga kwa kipindi kirefu na niliweza kuisadia japo kwa sasa muda umefika wameniacha, mimi ni mchezaji na soka ndiyo kipaji na ajira yangu, hivyo naamini nyota yangu ya soka ilipotea chini ya Maximo, bado nina imani kwamba kuna siku nitakumbukwa kwa mchango wangu Yanga,” alisema.

“Hatua waliyochukuwa inaweza kuwa ni sahihi kwao, Yanga ni timu kubwa na bado ina wachezaji wazuri, siyo kwamba kuondoka kwangu kutaifanya Yanga iyumbe, hapana, kuendelea kuwepo ama kuachwa ni moja ya maisha ya soka kwa mchezaji.”

Yanga sasa imebaki na wageni watano ambao ni Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima kutoka Rwanda, Sherman (Liberia), Tambwe (Burundi) na Andrey Coutinho wa Brazil.
 
Sijutii kwa kiiza kuondoka,sherman ni msumbufu kwa mabeki na anafanya timu iende mbele hata kama hafungi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom