Kweli wabongo tumetoka mbali!

Ralphryder

JF-Expert Member
Nov 16, 2011
4,933
1,294
Nakumbuka vioja vingi mfano, tukicheza mpira mtaani ukivaa njumu wenzio wanagoma kucheza na wewe maana timu nzima haina viatu! Ukienda disco bila kungfu shoes hupati mchumba! Enzi hizo shuleni kiatu ni safariboot! Na kiwanda ni Bora! Na wewe weka unayokumbuka....
 
UNavaa Chachacha ndio mjanja sana shule au kiatu kimeandikwa Zamoyoni Mogela sijui kama wachezaji walikuwa wanapata hata senti kutokana na viatu vile!
 
hahahahaha...mie nilkua na mpira wasiponipanga tu nilikua naondoka nao nyumbani

Teh teh teh umenichekesha sana! Mi nilikuwa kila siku nakula bakora home kwa kusahau viatu ktk uwanja wa mpira maana magoli hayakuwapo ilibidi upande mmoja mtu avue viatu ndo viwe magoli! Nikiondoka nasahau!
 
UNavaa Chachacha ndio mjanja sana shule au kiatu kimeandikwa Zamoyoni Mogela sijui kama wachezaji walikuwa wanapata hata senti kutokana na viatu vile!

ha ha ha! Chachacha ulikuwa ni mparo wa kutnkea! Kina Zamoyoni hawakufaidi chochote maskini!
 
enzi hizo ukitembea kifua wazi unaitwa gangwe..watoto wakikoromeana kidogo unawahi kuchota michanga na kuwageukia mmoja mmoja"puta,tia dole,vuka mstari"anayegoma kuputa kaogopa na ugomvi unaisha hapo hapo...
mnapinga bong'oa ukiinama unachukua bonge la shuti la ******..
unanyimwa namba mpirani ukicheza kilazima watu utawasikia"nyama huyo"hapo ukigusa mpira unastukia tama chini...
 
Kitaani tulikuwa na gari la kamba kuubwa hilo, mie nilikuwa napenda kuwa konda,

ilikuwa nikitoka kucheza mpira na kuskia kuwa mdingi karudi home najifuta miguu kwa mate kuepuka mboko...
 
Unapigwa dochi!
 
Kitaani tulikuwa na gari la kamba kuubwa hilo, mie nilikuwa napenda kuwa konda,

ilikuwa nikitoka kucheza mpira na kuskia kuwa mdingi karudi home najifuta miguu kwa mate kuepuka mboko...

enzi hizo madingi hawaopopi mtoto! Unakula mboko kwa kwenda mbele! Ndo maana tulifaulu shule!
 
Kulikuwa na mgao wa sukari,unga,mchele, n.k kwa kaya! Unawahi duka la ushirika au NMC kupanga foleni kwa kuweka jiwe,bila kujua leo muuzaji atauza nini! Unaganda masaa kibao akifungua anasema leo nauza chumvi tu! Hadi raha! Kuna jamaa walilikimbiza gari la NMC toka kinondoni hadi Ilala wakidhani kuna unga kumbe bosi kabebea chokaa!
 
...kuweka 'bluu' shati la shule...
...nilipaka kiwi raba zangu baada ya kuona zimepoteza rangi yake ya awali....duh...maradona
...wakinichezea rafu kwenye mpira na mpira kama ni wakwangu, nasepa nao,..mechi inakatishwa mpaka wanibembeleze
...tecnolojia ya simu ya mabox ya viberiti...unafunga waya...haloo, haloo unajaribu kuita
 
mhhh hapa stori zote nilizozisoma ni za miaka ya 90 chachacha, maradona,mabuti
 
Mnaikumbuka Raizon ngazi mbili, ngazi 3 ?
- Raba mtoni, pia nyumba Radio cassete National memory Q , ilionekana haina maendeleo.
- ikitambulika kijana anafanya kazi RTC au NMC na anataka kuoa basi wasichana mtaa mzima humtaka na anagombaniwa.
- ikifika saa 2 kasorobo usiku mnajikusanya kusikiliza RTD michezo mtangazaji Abdul Masoud (RIP) Taarifa habari Abdul Ngarawa, Jacob Tesha, Sekioni Kitojo. (wakati huo hapakuepo mwanamke mtangazaji aliyethubutu kusoma taarifa ya habari)
 
Mie nakumbuka baba alienda nairobi wakati fulan akaniletea ndala za sky way nekundu lol!
Nilijenga heshiam mtaan acha kbs,nakumbuka kuna shosti wangu mama yake alikuwa mwalimu aliponiona nazo akaniomba kuzijaribu wakati yy mtu mzima,hahahahha hii huwa siisahau aisee!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom