1. Long tym ukidundwa na wenzako unakimbilia kuita mabro wako wakamrudishie au kumkamata mbaya wako nawe umrudishie,,
2.Nakumbuka ugomvi wa mtaa kwa mtaa mara nyingi chanzo mpira au kuchukuliana mademu
3. Nakumbuka tulitawaliwa na michezo zaidi mf. Soka, kuendesha matairi mabovu ya magari au ringi za baiskeli kitumbo wazi shati umelichomeka kwa nyuma kwenye kibukta
4. Sisi wa dar tushakula fimbo sana baada ya kutoroka kwenda kuogelea baharini tulikuwa tunalambwa chumvi, michanga kichwani au chupi zilikuwa zina kamfuko kwa mbele basi laazma mchanga ukutwe humo/no boxers them days
5. Mwalimu mnoko ilikuwa kudundwa a madenti kawaida enzi hizo watu wanamaliza la saba wakubwaaa sio siku hizi
6.Kindumbwedumbwe kila weekend mtaani
7. Kwenda kuangalia tv au movies kwa jirani mwenye nayo tena unakuwa mnyenyekevu kwenye hiyo nyumba.. Na ilikuwa watoto ambao kwao kuna tv wanaogopewa eti watakupa mapigo ya wakali wa muvi wa enzi hizo chuck noris,bruce lee, van dame na wengine
8. Tobo bao bwanaaaa dah
9. Shati la shule kulipiga pasi vyumbavyumba kama kashata kwa mgongoni obviously pasi ya mkaa ilihusika
10. Ukivaa viatu vya DH/ zile njumu za kitambaa shuleni ilikuwa unataniwa hadi ukome.