Companero
Platinum Member
- Jul 12, 2008
- 5,604
- 1,704
Baada ya kufikiria kwa kina nimegundua kumbe ni kweli waafrika ndivyo tulivyo. Pamoja na jitihada zote za Chika Onyeani, Mtunzi wa Capitalist Nigger (Bepari Jeusi) kujaribu kutusaidia tuwe na tabia hizo za 'kukata shingo' (cut-throat) za Kibepari ili tupate maendeleo ya kibepari kama Ulaya na Marikani tumeshindwa na tunazidi kushindwa. Kwa nini? Kwa sababu sisi sio Wabepari. HIyo sio asili yetu. Naam ndio tulivyo - Wajamaa!