Kweli Tanzania tumefikia hapa?

Kweli Tanzania tumefikia hapa?

Mtoa mada anahoja sema tu amekerwa na yaliyomkuta. Mimi naona kweli kuna sehemu ukienda unapata huduma vizuri kwa card za NHIF na kuna sehemu ukienda na card hizi unwekwa kando kiaina flani hivi. Lakini kusema kweli NHIF imesaidia sana katika kuokoa wale ambao si kila mara unahela mfukoni.
 
usawa wa kulia
Hyo hela unayokatwa ni kiasi gani?nenda ukawaambie wakupe hela yako mkononi afu upigwe na stroke we au mzazi wako afu uende hospitalini uandikiwe kipimo cha MRI au ct scan ndo utakapoona kuwa ulikuwa mjinga kudai hela yako na baada ya wiki moja mkeo au mumeo apate ugonjwa unaohitaji upasuaji na baada ya siku tati mwanao alazwe hats kwa malaria ndo utakapojua umuhimu Wa kadi ya nhif na utaacha kuropoka ovyo
 
tatizo nyie mnaenda kwenye vijidispensari eti unategemea upate dawa..hebu nenda kwny mahospitali ya maana kama vile regency,tmj, uone huduma utakazopewa kwa hiyohiyo bima nadhani utakuja kubadilisha mada hapa

Mkuu me nimefanya kazi hospitali moja kubwa tu mjini DSM,nafahamu ni jinsi gani hao wagonjwa wa bima ya afya wanavyonyanyaswa,kwanzia ktk kupewa huduma hadi dawa. labda wenye green card ndio wana nafuu kidogo.
 
Siamini mlalamikaji amekuja na baseless claims, NHIF wanahitaji kuboresha huduma zao.
 
yupo sahihi kulalamika, wafanyakaz wanakatwa hela kila mwez lkn ukienda hospital wanakwambia hakuna, wanakuandikia then wanasema ukanunue, huu ni uonevu mkubwa.

Kama dawa hakuna hospitalini kwann usiende maduka ya dawa yanayotumia bima za NHIF??? au na kwenyewe ukienda unaambiwa utoe pesa??
 
usawa wa kulia

Labda nielezee kidogo kuhusiana na upande wa dawa( famasi ).

Kwanini mara nyingi wagonjwa wa bima hukosa dawa walizoandikiwa na madaktari, eiher iwe katika vituo vya afya au hata katika hospitali kubwa??.

Si kweli kwamba dawa hizo hivyo vituo vya afya au hizo hospitali wanakuwa hawana, bali ni kutokana na viwango vidogo vya bei vya dawa hizo serikali ilizozipanga.
Ifahamike ni serikali ndio inayopanga bei za dawa.
Na most of the time, kama si mara zote unakuta hazilipi. Kiukweli bei zao walizopanga haziendani na bei halisi za dawa sokoni. Mbaya zaidi hizo price list zao huwa inachukuwa muda mrefu kuzi update.

Na kama ujuavyo haina maana kwa mgonjwa kuja hospital kumwona daktari, kufanyiwa vipimo, na mwisho wa siku kukosa hata dawa moja aliyoandikiwa, na badala yake mgonjwa huyo huyo anaanza kuzunguka akitafuta dawa. Kwa kweli huu ni USUMBUFU MKUBWA SANA hasa kwa hawa wafanyakazi wanokatwa mishahara yao kila mwezi kwa ajili ya huduma za afya.
 
Last edited by a moderator:
Mdau pole sana, me ni mwanachama wa NHIF sijawah kutana na kadhia yeyote ila nakushauri kama una ushahidi peleka mahala husika, au kwa mkono au kwa njia yeyote ile, wewe ni mteja wake. But also huwezi jitibia bhana, acha masikhara mdau, usiangalie matibabu ya malaria
 
Hyo hela unayokatwa ni kiasi gani?nenda ukawaambie wakupe hela yako mkononi afu upigwe na stroke we au mzazi wako afu uende hospitalini uandikiwe kipimo cha MRI au ct scan ndo utakapoona kuwa ulikuwa mjinga kudai hela yako na baada ya wiki moja mkeo au mumeo apate ugonjwa unaohitaji upasuaji na baada ya siku tati mwanao alazwe hats kwa malaria ndo utakapojua umuhimu Wa kadi ya nhif na utaacha kuropoka ovyo

Kama dawa hakuna hospitalini kwann usiende maduka ya dawa yanayotumia bima za NHIF??? au na kwenyewe ukienda unaambiwa utoe pesa??

Mdau pole sana, me ni mwanachama wa NHIF sijawah kutana na kadhia yeyote ila nakushauri kama una ushahidi peleka mahala husika, au kwa mkono au kwa njia yeyote ile, wewe ni mteja wake. But also huwezi jitibia bhana, acha masikhara mdau, usiangalie matibabu ya malaria

ila NHIF kwa level za bongo wanajitahidi sana..

Kuna watu ni wabishi! Eti unakatwa 45,000/=Tshs sijui 54,000/=Tshs then unakuja kujitamba upewe hela mkononi, tena bila staha na matusi juu. Kuna watu watu wana majibu mepesi kwa maswali magumu.Nenda NHIF ujitoe basi tuone huduma hiyo "bora" utakayopata if you can afford at that same price!
 
Hapana, unasema uongo mweupe, mimi natibiwa Hindu mandali hawana huo mchezo kabiiisa, pale wagonjwa wa bima ndio wateja wao kwa 80% wana tujali saaana. Tafadhali sema vingine Tiba na pia hawaishiwi dawa.
 
Kuna siku nimeumwa usiku nikatibiwa kwa bima, ila dawa nilizopewa hazikunsaidia kwani nilizidiwa zaidi. Nilivyorudi tena hospital nikaambiwa nisitumie bima, ninunue dawa kwani haiwezekani kutumia bima mfululizo.
 
Ni kweli huduma ni mbovu, lakini ndugu kumpa mtu hela mkononi akajitibu yafuatayo yatatokea:

1. Hukana mtu atakuwa na hela hiyo wakati husika.. We waza ADA za mashule utadhani zinakujaga ghafla.

2. Vifo vitakavyosababishwa na kukosa hela ya matibabu. Hakuna Mtanzania anayeweka akiba ya matibabu. We jaribu kufikiri kama ingekuwa hata NSSF/ PPF etc. tungekuwa tunalipwa halafu tuzipeleke...

3. Watu wote wangechagua the lowest class ya matibabu, hasa kwa kuona huwa anaumwa nini na kwa mara ngapi kwa mwaka.

Ngalikihinja, sasa mbona wengne bima wakitusumbua tunajitibu na hela zetu za bank. Si kila mtu hawezi kutunza hela ndugu, ila bora wakupe hata ule kwasababu unakatwa hela yako bure tu kila mwezi na ukiumwa ujilipie tena?
 
Last edited by a moderator:
Mtoa mada anahoja sema tu amekerwa na yaliyomkuta. Mimi naona kweli kuna sehemu ukienda unapata huduma vizuri kwa card za NHIF na kuna sehemu ukienda na card hizi unwekwa kando kiaina flani hivi. Lakini kusema kweli NHIF imesaidia sana katika kuokoa wale ambao si kila mara unahela mfukoni.
Ni kweli mdau,binafs sijawai kutana na usumbufu kabisa
 
Hapana, unasema uongo mweupe, mimi natibiwa Hindu mandali hawana huo mchezo kabiiisa, pale wagonjwa wa bima ndio wateja wao kwa 80% wana tujali saaana. Tafadhali sema vingine Tiba na pia hawaishiwi dawa.

Mkuu nimesema hawakubali kutibu wafanyakazi wa serikali lakini wafanyakazi wa mashirika kama TANESCO na NSSF, PPF n.k wanapata huduma kama kawaida. Hii nimeishuhudia kwa macho yangu.

Tiba
 
Back
Top Bottom