Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 17,032
- 63,173
Yaani nchi yetu imekuwa ya ajabu mno siku hizi. Kila mwezi wanakata malaki ya hela kutoka kwenye mishahara ya watu kwa ajili ya bima ya Afya ya NHIF. Lakini ukienda hospitali kwa ajili ya huduma ya afya kama vile uzazi hospitali zinataka ulipie gharama za uzazi. Hili jambo halikuwepo zamani lakini siku hizi imegeuka ada. Na kibaya zaidi hizi hospitali hazitangazi rasmi au wazi ili watu wajue (nadhani ili kuogopa backlash ya kisiasa na hasira ya umma kwa serikali), lakini ndiyo imekuwa utaratibu siku hizi.
Wananchi tumekuwa tukiilalamikia serikali kuwa hayo mamikopo ya nje mnayokopa bila kujali kuwa kuna kesho madhara yake ndiyo haya, mnabana haki za msingi za raia ili kulipa madeni yenu, na ili mmentain extravagant life style zenu za mamisafara makubwa, mamishahara kwa wake/waume wa viongozi, maposho kedekede kwa wabunge lakini at the same time mnafanya quality ya maisha ya wananchi inazidi kuwa mbaya kila siku.
Sasa kuna haja gani mnakata mahela yote hayo kwenye mishahara ya watu kwa ajili ya bima ya afya ya NHIF halafu serikali inagoma kutoa hela kwa hospitali ili kucover magonjwa ambayo bima inacover?