Mtumiabusara
JF-Expert Member
- Nov 18, 2009
- 473
- 40
Huyu ni kuku kuku au kuku wa sumbawangaaaaaa mpandaaaa?
Pinda na yeye aache kupindisha mambo. Amekuwa serikalini akilipwa mshahara kwa zaidi ya miaka thelathini.Mshahara wake kwa kujinyima tu anasa angeweza kuwajengea wazazi wake nyumba nzuri tu na ambayo ni sawa na hadhi ya mshahara wake. Kuna waalimu tena wa shule za msingi wana nyumba bora na wanalima na kufuga kwa njia ya kisasa. Sitegemei kuona waziri asiye badilisha hali ya wazazi wake pamoja na jamaa zake kwa kuwahamasisha kubadili mtindo wa maisha eti tu kwa kuogopa kuonekana jajiri. Kama umeumbwa kutokukubali mabadiliko hata ukiwa rais, bado hutobadilika. Si tegemei mimi niteuliwe kuwa waziri mkuu, nikiwa na wazazi wangu wote nishindwe kuwanunulia nguo nzuri tena za kuvutia eti kwa kuogopa mimi kuonekana tajiri.
inategemea wazee wengine wabishi ukitaka kuwajengea nyumba nzuri na kubadilisha maisha yao hawataki kabisa, unawanunulia nguo nzuri wanagoma kuzivaa - unawaacha kama walivyo. you never know.
Pinda na yeye aache kupindisha mambo. Amekuwa serikalini akilipwa mshahara kwa zaidi ya miaka thelathini.Mshahara wake kwa kujinyima tu anasa angeweza kuwajengea wazazi wake nyumba nzuri tu na ambayo ni sawa na hadhi ya mshahara wake. Kuna waalimu tena wa shule za msingi wana nyumba bora na wanalima na kufuga kwa njia ya kisasa. Sitegemei kuona waziri asiye badilisha hali ya wazazi wake pamoja na jamaa zake kwa kuwahamasisha kubadili mtindo wa maisha eti tu kwa kuogopa kuonekana jajiri. Kama umeumbwa kutokukubali mabadiliko hata ukiwa rais, bado hutobadilika. Si tegemei mimi niteuliwe kuwa waziri mkuu, nikiwa na wazazi wangu wote nishindwe kuwanunulia nguo nzuri tena za kuvutia eti kwa kuogopa mimi kuonekana tajiri.
Pinda....changamka..hao wazee wanatakiwa wakae nyumba yenye hadhi kidogo...mimi kabwela wazee wangu nimewajengea kagorofa kamoja kule bush.....walikuwa wabishi lakini wakati ukawazidi ikabidi wahame.....kwa syle hii hata mungu hapendi,atakulaani
Pinda ni product ya Nyerere, hivyo amekuwa mfuasi mkubwa wa siasa za Nyerere. Pinda amefanya kazi ikulu miaka mingi toka enzi za Nyerere. Amekuwa katika vitengo vyeti sana pale ikulu. Ni mtu mwaminifu na wala si mla rushwa. Ameishi kwa mshahara wake tu hivyo wazazi wake kuwa katika nyumba kama hiyo si jambo la ajabu bali huo ni ukweli wenyewe. Bila shaka utakumbuka Nyerere naye wakati anastafu alikuwa hana mali alizojiwekea na pia alikuwa na nyumba ya kawaida kabisa pale kijijini kwake Butiama mpaka Serikali ilipoamua kuchukua uamuzi wa kumjengea nyumba ya kisasa.
Ni kuku wa Mpandaaaa!Huyu ni kuku kuku au kuku wa sumbawangaaaaaa mpandaaaa?
Kwapani acha fix..kuku wa kienyeji hufugwa hata na Mafisadi wakubwa huku town