Kweli Pinda mtoto wa mkulima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli Pinda mtoto wa mkulima

Discussion in 'Jamii Photos' started by Kapwani, Jun 20, 2010.

 1. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Pichani ni wazazi wa waziri mkuu Mizengo Pinda walipotembelewa na rais nyumbani kwao mpanda. Mimi nimeipenda nyie mnasemaje wakuu

  Mix with yours
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Umependa nini sasa? Nyumba ya wazazi wa Waziri Mkuu ilivyochoka?

  Halafu katika nchi yenye watu 90% wakulima kuwa mtoto wa mkulima ni distinction gani? Ni kama vile unasema "Pinda ni mtoto wa Watanzania" what kind of distinction is that among Tanzanians? Kama anataka kutuambia yeye ni mtu wa kawaida na hana distinction then hawezi kuongoza, ataongozaje na yeye mtu wa kawaida tu asiye na distinction wala merit, distinction yake eti "mtoto wa wakulima" of all things.
   
 3. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante mkuu kwa mchango wako! nadhani sikufafanua vema unisamehe sana...mie nimependa kuwa waziri mkuu ni mkweli alisema yeye ni mtoto wa mkulima na picha inaonyesha kweli mama yake ameshika kuku...kuku wa kienyeji ni zao la kawaida kwa mkulima wa tz
  Kwamba nyumba imechoka sikuwaza hilo kwani nyumba hiyo ni nzuri sana niki ikompea na yetu ....ata ivyo sina maadili ya kubeza mali za watu...sijatoa chochote kuwasaidia kwa iyo wao kuwa na bangalow au nyumba gani nadhani hainihusu
  Nilikuwa nimeoananisha maneno ya pinda na zawadi aliyoshika mama yake kumpa rais na si vinginevyo ...
  Mix with yours
   
 4. Tindikali

  Tindikali JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 766
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 180

  Kwa hiyo?

  Na mimi nasema ukweli kwamba mimi ni mtoto wa mfanyakazi, nimesema ukweli, kwa hiyo? Nipewe kitumbua? Wakati Pinda anazaliwa nchi ilikuwa kwenye minyonyoro ya wakoloni, kuwa mtoto wa mkulima sio ajabu. Unaelewa? Kizazi cha Pinda hakukuwa na watoto wa matajiri!

  Ulichokiona hapo kinaitwa fursa ya picha.

  Kwenye siasa, fursa ya picha ni tabia ya kiongozi kujitegesha, kukaa mkao wa picha itakayomjengea taswira ya kupendeza. Mara nyingi hutumika kujionyesha unajali kitu ama watu fulani. Hapo juu Rais anasafisha taswira, ya Pinda wake, na serikali yake kwa ujumla, kujifanya watu wa watu. Anauza sura.

  Sasa, Rais anatembea na wapiga picha wakati wote, na kila analofanya linaweza kupigwa picha laiti ni nje ya msalani. Unaweza kusema yeye hawezi kuepuka fursa za picha. Lakini wananchi wa jamii zilizopevuka kisiasa, picha yeyote ya Rais ya kuuza sura inachukiliwa kwa punje ya chumvi, kwa tahadhari, kwa sababu tunajua anaweza kuwa anatafuta ujiko, awe amejitegesha au hajajitegesha. Haziheshimiki.

  Na kibaya zaidi Kikwete mwenyewe anazikosea hizo fursa za picha. Anaenda kwenye misiba ya wake wa matajiri na mabalozi wastaafu. Anapiga picha akimpa mtoto peremende lakini yuko ndani ya Shangingi la Rais, hashuki. Muafrika humrushii chakula kwa mbali. Anapiga picha akipokea kuku nyumbani kwao Waziri Mkuu.

  Wazazi wa Waziri mkuu sio wakulima wa kawaida tena! Tanzania ndugu za viongozi wanahudumiwa kiholela holela, hata hawa usikute ni mimi ndio nawatunza na kodi yangu. Wake watatu wa Rais, sheria zinasema nini kuhusu huduma kwa wake wengi, hata haijulikani. Si ajabu hiyo nyumba ya kwao na Pinda inapata ma Land Cruiser ya kuku na mchele kila siku, ma Fuso ya ma Simtank ya maji kila siku, na ma Defender ya FFU.

  Ni rahisi sana kuwa kiongozi Tanzania, Afrika. Eti bado fursa za picha zinachota watu.
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Thanks kamanda

  ni yaleyale ya kumsifia simply kwasababu hajaiba sana hivyo nyumba yake ni chovu!!! kuwa mtoto wa kulima inakua abused these days wakati asilimia mia ya watanzania wana link ya moja-kwa-moja na wakulima

  ni ufisadi tu ndio unasumbua

  tuliulize sasa huko kuku kweli aliliwa na JK au ndio yale ya kuse pa mitego?
   
 6. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Wakati Mkuu wetu wa kaya anapokea zawadi ya kuku wa kienyeji, akina Al Gore wako bize maofisini kwa tija ya nchi yao...Halafu kesho tunakwenda kuomba misaada!

  [​IMG]
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa Mkuu nakuunga mguu tutakuwa omba omba mpaka lini?ikiwa Mkuu wetu anatembela Wazazi wa Waziri mkuu je kweli huko offisini kwake nani atafanya kazi? Au ndio kumefungwa mpaka arudi mkuu wetu toka Ziara ya Mikowa?kazi kweli na bongo yetu WAFRIKA BWANA NDIVYO WALIVYO EHHH
   
 8. Q

  Qadhi JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2010
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Al Gore yuko BIZE sana bana,,,yaani kaacha hadi mke?it's too much
   
 9. Iteitei Lya Kitee

  Iteitei Lya Kitee JF-Expert Member

  #9
  Jun 21, 2010
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 589
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Huyu ni kuku kuku au kuku wa sumbawangaaaaaa mpandaaaa?
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  Jun 21, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Dah hapa no comment:A S 103:
   
 11. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #11
  Jun 21, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nadhani inafaa tuwe na viongozi wa aina ya Pinda kwa maana ya watu waliokulia maisha ya kawaida (wanaozitambua kwa undani changamoto anazopambana nazo mtanzania wa kawaida) lakini waadilifu wanaotaka kuitoa nchi hii kutoka kwenye umasikini kwa kutumia rasilimali zetu vizuri, siyo kwenda tunajipendekeza na kujidhalilisha kwa wazungu kuomba misaada.
  Mpaka pale tutakapoacha kulaumu vita vya ukombozi wa Afrika kwa umasikini wetu, ukosefu wa pesa za kuwasaidia watu wetu, na visingizio vingine tunavyo-manufacture ili mradi ku-justify umasikini wetu ndipo tutaondokana na umasikini.
  Binafsi sioni umhimu wa rais wetu kuwa kila sehemu kila siku akihudhulia uzinduzi wa maabara (tuliyojengewa kwa msaada), akipokea zawadi ya kuku (sijui ya kufuga?) akihudhulia matamasha ya mziki na akina Boys II Men, akirandaranda huku na kule kututafutia misaada. Halafu kesho yake anatudanganya kuwa ahadi zote alizotoa wakati akiomba kura 2005 zitatekelezwa na kuwa ndani ya miaka miwili kila mwalimu wa Tanzania atakuwa na laptop, wakati hata mshahara wake tumeshindwa kuuongeza ili awe motivated zaidi.... no priority, no direction, no brains, no nothing, just smiles and empty words. Hatutaki!
   
 12. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #12
  Jun 21, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  mama? baba? weka wazi watu watangaze nia? soroff topic
   
 13. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #13
  Jun 21, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  nadhani message yako hujaiweka vizuri hivyo ujumbe wako haujatufikia vizuri, lakini kuna maana sana kubwa sana kwa viongozi wa sasa wa Tanzania na familia zao zinavyohishi, ukilinganisha na hiyo picha
   
 14. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #14
  Jun 21, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante mkuu kama umenielewa kidogo hebu nisaidie kufanunua vema kwa wana jf ...will be helpful
  Mix with yours
   
 15. j

  jamadary Member

  #15
  Jun 21, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata mi nimekubali Waziri Mkuu wetu kweli ni Mkulima namuunga mkono kwani tuko wengi hata mi najivunia hilo kwa wazazi wangu ni wakulima wakubwa tangu kitambo sana
   
 16. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #16
  Jun 21, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Rais wetu anakazi nyingi sana ofisini kwake lakini kila leo yeye ni kiguu na njia; mifano mchache tu inatosha kudhihilisha haya niandikayo, hivi sasa kuna mashirika na taasisi nyingi ambazo hazina bodi wala wenyeviti na yeye ndiye mwenye mamlaka ya kuteua wenyeviti na mawaziri ngwe yao ni kuteua wajumbe lakini mpaka hivi sasa mashirika kama TCAA na Air Tanzania hayana bodi; kwahiyo yanaendeshwa kiholele!! Anangojea mpaka baada ya uchaguzi awape zawadi wapambe wake, kweli nchi hii kazi tunayo.
   
 17. k

  kaiya Member

  #17
  Jun 21, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaacha au wameachana??
   
 18. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #18
  Jun 21, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Yeye ni mtoto wa mkulima, mimi ni mkulima mwenyewe
   
 19. JAMIETZN

  JAMIETZN Member

  #19
  Jun 21, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu nimecheka sana. Kama ulishaishi karibu na nyumba za hawa waheshimiwa utakubaliana na maneno red, Nakumbuka jirani yangu alikuwa wa kwanza kuletewa misamaki ile mikubwa na mboga mboga toka kwa wakulima wafungwa kwenye magereza.

  Hiyo nyumba huenda ni banda la nguruwe na kuku tu, Nyumba ya Pinda na wazazi wake ipo mfukoni mwa Pinda, Any time atakayo feel kuitoa mfukoni ndio mtaitambua vizuri. Hizi picha ni za kusafishana safishana machoni mwa watanzania. Hatukatai utendaji wake lakini pia hatukubali kumwagiwa changa la macho.
   
 20. JAMIETZN

  JAMIETZN Member

  #20
  Jun 21, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawezi kumla huyo kuku kabla wataalam hawajampigia kisomo !!
   
Loading...