Kweli mdomo huumba, ni laana au?

Kweli mdomo huumba, ni laana au?

Aunty kemmy

Member
Joined
Dec 13, 2013
Posts
46
Reaction score
23
Katika familia yetu mimi ni wa mwisho na ni mtoto wa nje ya ndoa. Wazazi wote wamefariki. Tukiwa katika pilikapilika za mambo ya urithi mambo mengi yalitokea, kuna dada yangu mmoja alithubutu kuninyanyasa kwa kusema mimi ni mtoto wa nje sistahili kurithi mali.

Kiukweli alikuwa hanipendi, iliniuma sana na kila siku nilikuwa nalalamika juu yake vioja alivokuwa ananifanyia katika hiyo nyumba tulokuwa tunaishi ya urithi. Nilikuwa natamani niondoke home lakini nitaenda wapi, bahati nzuri nikapata kazi mkoa mwingine nikafurahi, nikaenda huo mkoa nikaanza kazi.

Nikasahau yote ya nyuma nikiwa huko baada ya miezi kama nikapata taarifa kuwa dada yako ameuliwa ndani ya ile nyumba mliokuwa mnakaa amekutwa kaoza. Nilishtuka nikakumbuka maneno nilowahi kutamka nikiwa nanungunika juu yake, inshort kifo chake jinsi kilivotokea niliwahi kukitamka kwa mdomo wangu.

Kweli mdomo huumba jamani nilikuwa naongea tu kwa hasira kumbe imekuja kutokea kweli.

Mpaka leo najiuliza ni nini hiki!
 
Hata watu wakutende mabaya kiasi gani ama wakuumize kiasi gani usipende kunena mabaya juu yao, wasamehe na waombee kwa Mungu awabadilishe Shetani huwa anayasikia tunayoyanena na kuyafanyia kazi.
 
Hakuna kitu cha uhalisia kinachoitwa laana.

Hiyo inayoitwa laana ni jambo la kufikirika tu ambapo watu huunganishia matukio mabaya na hiyo dhana kwa sababu ya ukosefu wa uelewa juu ya jambo au mambo fulani.
Kwa mara ya kwanza nakupinga Mkuu iko kitu kipo kwa wenye kuamini haswa washika dini...
Kauli huwa tendo na tendo uwa kauli..
Ndio maana tunafundishwa kukaa kimya au kufikiri kabla ya kusema...
 
Hata watu wakutende mabaya kiasi gani ama wakuumize kiasi gani usipende kunena mabaya juu yao, wasamehe na waombee kwa Mungu awabadilishe Shetani huwa anayasikia tunayoyanena na kuyafanyia kazi.
Sio siri shetani huwa hana mchezo ktk hili.
 
Laana ni neno la kufikilika ingekuwepo mimi ningeshakufa siku nyingi, kwa nature ya kazi yangu Mara kadhaa nimekuwa nikipewa laana na muda mwingine nilikuwa natishika kabisa ila miaka inaenda na bado nadunda town
 
mshana jr naomba uandae somo LA Laana mbalimbali naona Monkey Ngabu kuna kitu anajisahaulisha

Nishatoa fursa kwa wachawi wote waliopo JF waniroge ili wanithibitishie kuwa uchawi upo lakini wapi, miaka kadhaa ishapita sasa na bado ninadunda tu kama kawa.
 
Omba toba kwaajili ya uko wako yaani tangu mababu, baba yako, mama yako na nduguzako wote, ndipo mungu ataifuta hiyo laana ama sivyo itaendelea kuwaandama.
 
Laana ni neno la kufikilika ingekuwepo mimi ningeshakufa siku nyingi, kwa nature ya kazi yangu Mara kadhaa nimekuwa nikipewa laana na muda mwingine nilikuwa natishika kabisa ila miaka inaenda na bado nadunda town
kaz gani mkuu
 
Back
Top Bottom