Ukiangalia kwenye Jumuiya tunazoishi utagundua Nyumba za Urithi ni tatizo kubwa sana.
Na utakuta Ndugu wenyewe kwa wenyewe wanawekeana Bifu.
Hasa,
Hawa Wajomba, Shangazi, Baba Mkubwa, Baba Mdogo, Mama Mkubwa, Mama Mdogo.
Cha ajabu unaweza kuta mmoja wa niliowataja hapo juu Watoto wa Mdogo wake au Kaka yake, au Dada yake wa tumbo moja, anataka wapunguzwe kwenye mgao, ili mgao umpitie yeye na Familia yake.
Jamani, Watu hawana huruma.
Nimeshuhudia migogoro mingi sana ya Mirathi, na siku zote kwa uchunguzi wangu nimegundua Mashangazi kwenye Mirathi sio watu wazuri hata kidogo.
Wanaweza kumuwekea hata Sumu Mtoto wa Marehemu kumpunguza, ili mgao wanufaike nao wao na Watoto zao.
Na wao siku zote wanakuwa kimbelembele sana linapokuja suala la Mirathi