Kweli mafuriko sio ushindi

Kweli mafuriko sio ushindi

sheiza

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2010
Posts
7,634
Reaction score
11,691
IMG_20150828_224822.jpg IMG_20150828_224935.jpg IMG_20150829_071603.jpg IMG_20150829_071703.jpg IMG_20150828_225130.jpg
Kweli nimeamini mpira ni mpaka filimbi ya mwisho ipigwe ndio muda mzuri wa kushangilia na kutamba.. Nakumbuka 2010 jinsi Dr Silaa alivyokuwa anakusanya mafuriko kwenye mikutano ya kampeni..huku e-polls zote za kwenye mitandao zikionyesha amemuacha mbali JK..Hapa mtu atakuambia watu hawakujiandikisha lakini hao hao watu ndio walifanikisha kupitisha wabunge wa chadema kwa uwingi wao..

Kikubwa hapa hususani kwa hiki kizazi kipya cha siasa msidanganyike na wingi wa watu kwenye mikutano ya Lowasa mkadhani ushindi tayari..hakuna kitu kama hicho..Kwa nchi za kiafrika matokeo ya mwisho ndio hutoa mshindi wa urais.. Kwa hiyo msitegemee ushindi kwa kutumia hicho kinaitwa mafuriko kwenye mikutano.

Labda kuna mtu atasema kuchakachua lakini nani kathibisha..tunarudi palepale kwamba matokeo ya mwisho ndio hutoa mshindi wa urais..
 
Dallai lama unadhihirisha umkapa wako..
 
Mbona CCM nanyi manajivunia mafuriko ya Magufuli huko anakozunguka. Ukiona mafuriko ni dlili nzuri ya mapenzi ya UKAWA na wapiga kura wake. Hizo siyo picha za kuunga kama alivyosema mnayemfahamu ni picha halisi. Mumlaumu mwenyekiti wenu ndo amewafikisha wana CCM hapo mlipo. POLENI SANA.
 
Naweza kubaliana na hoja yako kwa upande mmoja, lakini jua hili, kila siku influence ya kisiasa huongezeka kwa watu hivyo ilivyotokea 2010 haimaanishi kuwa itajirudia na 2015 tena. Kila kinachotokea kwa jirani huwa na impact kwako, kwa kupenda au lah, haya unayoona yakitokea nchi za jiran kwa wapinzani huleta mwamsho kwa watanzania, na hutia hamasa zaid kwa hiki kizazi cha vijana.
Mwisho nikutake ujiandae kukubaliana na matokeo yatakayotokea hata km yatakuwa tofauti na utabiri/ matarajio yako.
 
Tungoje BALOT BOX INASEMAJE !
Kwenye mafuriko wanakuwepo hata darasa la kwanza!
 
Ni kweli ulivyosema hata mby Magufuli amejaza watu kumbe ni mbwembwe tu za akina Dymond
 
View attachment 281518View attachment 281519View attachment 281520View attachment 281521View attachment 281522
Kweli nimeamini mpira ni mpaka filimbi ya mwisho ipigwe ndio muda mzuri wa kushangilia na kutamba.. Nakumbuka 2010 jinsi Dr Silaa alivyokuwa anakusanya mafuriko kwenye mikutano ya kampeni..huku e-polls zote za kwenye mitandao zikionyesha amemuacha mbali JK..Hapa mtu atakuambia watu hawakujiandikisha lakini hao hao watu ndio walifanikisha kupitisha wabunge wa chadema kwa uwingi wao..

Kikubwa hapa hususani kwa hiki kizazi kipya cha siasa msidanganyike na wingi wa watu kwenye mikutano ya Lowasa mkadhani ushindi tayari..hakuna kitu kama hicho..Kwa nchi za kiafrika matokeo ya mwisho ndio hutoa mshindi wa urais.. Kwa hiyo msitegemee ushindi kwa kutumia hicho kinaitwa mafuriko kwenye mikutano.

Labda kuna mtu atasema kuchakachua lakini nani kathibisha..tunarudi palepale kwamba matokeo ya mwisho ndio hutoa mshindi wa urais..

Wizi wa kura ndio tatizo kubwa sana.
Aliyekua mwenyekiti wa tume ya uchaguzi mwaka 2010 aliahidi kutoa takwimu sahihi za matokeo ya kura za urais wa mwaka 2010.
Mpaka anafariki hakuweza kutoa.
Kaenda na siri ya ushindi wa CCM.

Hata mwaka huu wizi umeshaanza...
Refer to Nape Nnauye na kauli zake za CCM lazima kushinda hata kwa 'goli (bao) la mkono'

Soma kidogo hapa...

https://www.jamiiforums.com/uchaguz...ha-namba-za-vitambulisho-vya-wapiga-kura.html
 
ccm ni majizi haswa ......kama sasa hivi wakat kampeni zinaendelea wao kuna kamati ya "fitna" au maarufu kama "kitengo" wao wakiamka tu kazi ni moja tu ni kuwaza namna ya kuiba kura ilikushinda mfano:
1.Kutengeneza kadi feki..........hizi baadhi tayari zimekamatwa tumeona hata kwenye vyombo vya habari.
2. kuandikisha majina na namba za vitambulisho kwakudanyanya kua wanataka kuanzisha fursa ya kiuchumi.....haya tumeyaona kwenye vyombo vya habari jana.
3. Lakini pia kuna habari kua wadauwaowamejiandikisha mara nyingi....tumeyaona kupitia vyombo vya habari kupitia viongozi wa NEC.
4.Tetesi 😛eni za kutikia mgombea uliye mchagua ukiweka tiki baada ya sekunde chache inafutika iliwao baadae waweke tiki kwa peni nyingine kwa mgombea wao.
5. kujaza watu kwa malory toka mikoa ya jirani na vijijini ili baadae wasema wao pia walikua na watu wengi hivyo wameshinda wao.
6. kucheza na kalenda ya wanafunzi wa elimu ya juu ili wasipige kura.
7. watu walio jiandikisha kukuta majina yao hayapo hivyo kukosa fursa muhimu ya kupiga kura.

Na wizi mwingine mwingi bado hauja gundulika.......maccm ni majizi yaliyo pitiliza. Mwaka huu UKAWA ni lazima wawe macho kuliko kawaida maana hata 2010 walishinda lakini maccm majizi haya yaliiba kwa kishindo. UKAWA nguvu ya umma.
 
2010 walifunga goli la mkono wanadai na mwaka huu hivyo hivyo tena refa atapigwa chenga la macho
 
Je unajua mwaka 2010 wapiga kura 42% ndio wanadaiwa kupiga kura?. Je ni kweli 58% ya wapiga kura hakwenda vituoni siku hiyo? Na unapozungumzia mafuriko usiigemee chama
 
Back
Top Bottom