Kweli leo nimekoma

Mkuu.. mlima Kilimanjaro unaonekana Asubuhi mda wa saa 11 mpaka saa moja. Baada ya hapo unafunikwa na mawingu. Unaweza pia kubahatisha kuuona mchana lakini ni mara chache na tena ni mda wa kiangazi tu. Ukifanikiwa kuuona unapendeza sana



Hapa ni maeneo ya marangu.. Mda ilikua ni saa moja asubuhi
 
Nenda Kibosho maeneo ya Umbwe utauona vizuri hadi ufurahie
 
Nimekaa Moshi siku tatu lakini sikufanikiwa kuuona mlima, siku ya mwisho nikaambiwa natakiwa kuwahi kuamka saa 12 asubuh ndio naweza kuuona
 
Kutoka malangu mpka moshi mjin ni sh ngapi hata mm napanga siku moja nitembelee huko nikaone mlima
 
Kabla ya kurudi Arusha Kunywa mbege kwanza mlima utauona
 
Mlima uko picha karibu zote, just google Mt. Kilimanjaro
 
Ukisimama pale KNCU unauona, Ukiwa Mweka pale Chuoni unauona, ukiwa TPC kule unauona, Ukiwa Mile Sita pale Weruweru unauona.
 
Njoo kesho shuka Tengeru saa 10 jioni yani unauona live kama vile upo hapo mbele tu
 
Hata ukiwa KIA mbona huwa unaonekana vizuri tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…