Kweli kuishi na Mwanamke kunahitaji hekima

politicians

Senior Member
Apr 8, 2018
154
124
TUISHI NAO KWA HEKIMA SANA NDIVYO VITABU VYA MUNGU VILIVYOTUAGIZA

Jamaa kaamka asubuhi, kavaa track suit na kumuamsha mkewe!

MUME: Amka twende jogging mke wangu?
MKE: Alaaa kwa hiyo una maana mi tipwatipwa? (Mnene)

MUME: Hapana si hivyo jogging ni nzuri kwa afya yako mke wangu
MKE: Kwa hiyo una maana mi mgonjwa?

MUME: Basi yaishe endelea kulala
MKE: Kwa hiyo unaniona mi mvivu sana sio?

MUME: Hujanielewa mpenzi wangu sikuwa na maana hiyo baby
MKE: Kwa hiyo mie mjinga mpaka nashindwa kukuelewa?

MUME: Jamani mi sijasema hilo
MKE: Kwa hiyo mie muongo?

MUME: Chonde tusiendeleze haya asubuhi namna hii
MKE: Kwa hiyo mie ndio naendeleza ugomvi?

MUME: Sikia we lala mie naenda jogging.
MKE: Ndio zako hizo mambo yote unafanya peke yako hunishirikishi"

MUME: Unajua nimeanza kusikia kizunguzungu
MKE: Unaona nikiongea kidogo unakimbilia kuumwa, mbinafsi sana wewe...

MUME: Basi ngoja tu nilale siendi jogging
Mke: Kwahiyo ulikua unanijaribu?

WANAWAKE MUNGU ANAWAONA MUJUE
 
Hapo mke kaibuka mshindi mme kakosa msimamo,

Jamani ifahamike Hawa wanawake wa siku hizi ukienda nao kibabybaby kila siku utalialia mpaka mtoto was yusufu anarudi

Kwa kizazi hiki cha mwanamke wa Android usieleweke ,
mida mingine kuwa leo kuwa kondoo kesho kuwa chui

Mchana msikilize jion jifanye ulisahau
Wiki hii unajifanya yuda kidogo wiki ijayo unakuwa Ibrahim
Leo unarudi mapema hadi unaangalia nao tamthilia kesho unatimba night kali,
Mara nyingi huwa wanapenda kututingisha kwa vitu vidogo tu halafu ukiteteleka kidogo wanajisemea kimoyomoyo Bora ningekuoa

Mwanaume hakikisha huweki ligi yoyote nyumbani ukiona dalili ya ligi unaweka hitimisho tu unabaki na msimamo wako

Kazi njema
 
Director kuna hiki kipande kime miss hapo kukamilisha convo

MUME: Basi samahani naomba uchukue ATM card hapo mezani twende shoping nikakununulie zile nguo zako unazozipenda
 
Muda wa kujibishana yote hayo mnautoaga wapi? Pengine ndo mana nipo single mpka leo kifupi huwa si entartain ujinga.
 
Ukimaliza kukisoma iki kitabu,utakua umewajua wanawake,
JamiiForums-204902884.jpg
JamiiForums308654683.jpg
 
TUISHI NAO KWA HEKIMA SANA NDIVYO VITABU VYA MUNGU VILIVYOTUAGIZA

Jamaa kaamka asubuhi, kavaa track suit na kumuamsha mkewe!

MUME: Amka twende jogging mke wangu?
MKE: Alaaa kwa hiyo una maana mi tipwatipwa? (Mnene)

MUME: Hapana si hivyo jogging ni nzuri kwa afya yako mke wangu
MKE: Kwa hiyo una maana mi mgonjwa?

MUME: Basi yaishe endelea kulala
MKE: Kwa hiyo unaniona mi mvivu sana sio?

MUME: Hujanielewa mpenzi wangu sikuwa na maana hiyo baby
MKE: Kwa hiyo mie mjinga mpaka nashindwa kukuelewa?

MUME: Jamani mi sijasema hilo
MKE: Kwa hiyo mie muongo?

MUME: Chonde tusiendeleze haya asubuhi namna hii
MKE: Kwa hiyo mie ndio naendeleza ugomvi?

MUME: Sikia we lala mie naenda jogging.
MKE: Ndio zako hizo mambo yote unafanya peke yako hunishirikishi"

MUME: Unajua nimeanza kusikia kizunguzungu
MKE: Unaona nikiongea kidogo unakimbilia kuumwa, mbinafsi sana wewe...

MUME: Basi ngoja tu nilale siendi jogging
Mke: Kwahiyo ulikua unanijaribu?

WANAWAKE MUNGU ANAWAONA MUJUE
Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; maana wao pia ni warithi wa neema ya uzima, ili maombi yenu yasizuiliwe na chochote.
1 Petro 3:7
 
Director kuna hiki kipande kime miss hapo kukamilisha convo

MUME: Basi samahani naomba uchukue ATM card hapo mezani twende shoping nikakununulie zile nguo zako unazozipenda
kwahiyo umeona mi masikini sana naongea vya maana unanituliza na hela? we mwanaume una dharau sana ushaona najiuza sio? hawajawahi ishiwa maneno.
 
Nyingine hii apa

Mume katoka kazini......

Siku ya kwanza
Mke: uoge kwanza ndo upumzike

Mume: aaagh... Niko safi mke wangu, kwa uchovu huu hebu nipumzike kwanza, ntaoga baadae.

Mke: Twende nkakuogeshe

Mume: Dah wewe nae.... Sawa, acha nkaoge mwenyewe.

Siku ya pili
Mume: Nimechoka sana mke wangu, ntaoga baadae ngj nipumzke.

Mke: Ushaanza habari zako, Twende nkakuogeshe, maana kila siku hadi tupigizane makelele.

Mume; Sawaaaaa, naoga.... andaa tu chakula mke wangu

Siku ya tatu
Mume katoka zake kazini akiwa na furaha ya mshahara kuingia,
Kimoyomoyo kajisemea "leo nikienda naoga bila kupigiwa kelele na mke wangu".

Kufika tu, mke yuko bize kuandaa chakula, jamaa kapitiliza bafuni, kapiga maji safi kabisa, then katoka.............

Mke: Aaaaaaaagh! kwanini umeoga??!!!

Mume: khaaa, swali gan hlo mke wangu

Mke: Huko ukipotoka umetoka kufanya nn hadi uje uanze kuoga?. Kwanza toka lini umetoka kazini ukaja kuoga kabla hatujapigizana kelele. Ko umeamua kunisaliti mchana kweupe.....

Mume kachoka.
 
Back
Top Bottom