Dada aolewa na kibaka! Mlishaonywa na kufundishwa kusali kwakuwa Mungu si kiziwi

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,793
Maneno ya Mungu yanasema hivi..Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.

Dada mmoja usiku mwingi kukiwa tulivu kabisa akaanza akaanza maombi ya kuomba kupata mume.. Hili halikuwa tatizo kabisa, maana maombi ndio njia kuu ya kuwasiliana na Mungu..
Dada alichokosea ni kuomba kwa kupiga kelele na kupayuka kwa sauti ya juu

Alianza kwa kumshukuru Mungu kwa kumpa elimu nzuri
Kisha akamshukuru kwa kumpa kazi mzuri
Akaendelea kwa sauti ya juu kushukuru kwa mshahara mkubwa na masilahi mazuri kiasi cha kujiwekea hakiba ya kutosha sana ndani ya muda mfupi

Sasa akaingia hatua muhimu ya maombi.. Akiomba Mungu ampatie mume atakayempenda kumjali, kumtunuku na lumpatia vyote alivyonavyo ama chochote atakachohitaji..

Kumbe kipindi chote hiki cha maombi haya ya nguvu kwa sauti ya juu kuna kibaka alikuwa kajibanza dirishani akisubiri maombi yaishe mwombaji alale jamaa afanye yake
Ni kwenye kipengele hicho cha kupata mume ndio kibaka akapata wazo jipya na kuahirisha kuiba na kuondoka
Kesho yake asubuhi na mapema kibaka akaibukia nyumbani kwa yule dada na kugonga mlango kwa bashasha sana

Dada alipofungua mlango Jamaa akasema kwa sauti ya furaha sana ... Halelujah maombi yangu yamejibiwa.. Nimeongozwa na roho kuja hapa kukutana na mke wangu mtarajiwa..

Maskini dada wa watu bila kujua anaingizwa kingi, akampokea jamaa na kufurahi maombi yake kujibiwa kwa muda mfupi sana
Alichokuja kukuta nacho kwenye hiyo ndoa mpaka anakuja kuujua ukweli wote kilimpa fundisho kubwa sana hasa kwenye kipengele cha maombi
 
Eeeh kazi kweli kweli
Screenshots_2023-04-22-21-13-35.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom