Kweli Kifo habari nyingine

Richbanks

Member
Joined
Apr 25, 2019
Messages
13
Points
45

Richbanks

Member
Joined Apr 25, 2019
13 45
Kweli kifo habari nyingine uuuuwiSikia Hii kali ya leo

Familia moja walifurahi sana kupata mtoto, lakini majonzi yalianza pale walipogundua siku zinaenda lakini mtoto hawezi kutamka neno lolote. Mtoto alizaliwa bubu. Siku moja ghafla wakasikia anasema bibi bibi, wote wakafurahi na kujua kuwa labda kaanza kuongea. Furaha yao iliisha baada ya muda mfupi, bibi wa mtoto akafariki.

Baada ya hapo mtoto akaendelea kuwa bubu. Mwezi baada ya msiba mtoto akaamka anatamka mjomba mjomba, wakafurahi tena ila furaha yao ikaisha mjomba alipofariki masaa machache baadaye.

Sasa ikawa wasiwasi. Wanaogopa mtoto asifungue mdomo. Lakini asubuhi moja mtoto akasema Baba baba, basi mzee mwenye nyumba furaha ikamuishia akanyong'onyea akisubiri kifo. Usiku hakulala. Mkewe akamuonea huruma na kumwambia "Mume wangu samahani kwa ntakalokwambia, kiukweli mtoto huyu si wako nilichepuka na baba yake amefariki masaa mawili yaliyopita"

Jamaa aliamka na kumkumbatia mkewe kwa furaha na kumsifu, "Asante mke wangu leo ndio nimejua unanipenda kwa dhati".


Usicheke peke yako share na marafiki zako.
 

Forum statistics

Threads 1,381,428
Members 526,090
Posts 33,799,933
Top