Kweli hii ni shida!

Kweli hii ni shida!

mlivoachana kwani mlisema ham,tajihusisha tena na mapenzi? kuachana ni kwamba kila mtu aangalie mtu mwingine wa kuendana nae .wewe unamuogopa nini? au hapo ni kwake?
Mkwala tu, si unajua tena!
 
Pole mwayaa, hana wivu ila roho inaumaaaa
 
Jamani waungwana

Leo baada ya kutoka kanisani, nimemkaribisha nyumbani dada mmoja ambaye ni rafiki yangu na tunaheshimiana sana, kwa hiyo tumeongozana naye mpaka nyumbani. Nikawatambulisha mgeni aliyetutembelea. Tukapata chakula cha mchana pamoja na familia yangu iliyopo hapo nyumbani, baada ya hapo akatuaga na kuondoka.

Kutokana na wingi wa kazi ofisini kwangu, nikaona ni jambo jema angalau niende nikapunguze baadhi ya kazi.

Naishi na wanangu wawili, wote wa kike hapo nyumbani, mama yao hatupo pamoja nae aliniacha kwa muda mrefu na anaishi mkoa mwingine.

Baada ya kutoka nyumbani, watoto waliongea na mama yao na mara nyingi huwa ana kawaida ya kuwapigia simu siku ya jumapili ambayo huwa wapo nyumbani, sasa kumbe akawa anawadadisi na wamemweleza kuhusu mgeni aliyefika hapo nyumbani.

Niko ofisini, nasikia mlio wa msg inaingia. Kusoma, hakuna cha salam, kaandika "usiwafundishe watoto tabia mbaya, we ma.....ya, huna akili, huwezi leta mwanamke ndani ya nyumba mbele ya watoto, unawajengea tabia mbaya" Nikafikiri sana kwa kweli kaniondolea amani ndani ya moyo wangu kwa siku ya leo.
Moyo ungekua unaazimwa ningekuazima umtie adabu,huwezi kosa amani kwa mtu na kauli za kitoto hzo.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji3] mzazi mwenzio ana point kubwa kusema usiwafundishe watoto tabia mbaya ,

Ila kwa upande mwingine ana kosa, vizur angeanza kukuuliza kwanza.

Nisaidie namba ya mzazi mwenzio nijaribu kumuelekeza[emoji23][emoji23]
Unaingia kwa gia nzuri sana mkuu
 
kwanza nianze na hao watoto,inaonekana hao watoto na Maza yao hua wanakuongea sana pili mkuu jitahidi uwe makin na huyo mzazi mwenzio atakuharibia watoto kuna sumu anawapandikiza juu yako,watoto watakua wanakuwekea hira moyoni juu ya kuachana na mama yao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom