Kweli akutukanaye hakuchagulii tusi

double R

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
2,398
2,538
Nimesikitishwa sana hadi nimetoa machozi kwa hiki kilichokuwa kinaendelea kwenye uzi wa Wanawake wanajiuza.

Wanaume mnataka nini? Mmekosa hata staha kwa hao wachache mnaowajali mkabaki mnashabikia haya. Najua watakuwepo wa rika mbali mbali na mmeonyesha ushirikiano mzuri kweli. Mmeona mnayowafanyia humo vyumbani haitoshi mpaka mje kuanika u.p.u.m.b.a.f.u wenu hapa.
Haikutosha kutoa fedheha hizi kwenye vijiwe vyenu ambavyo sisi hatupo mkatuhabarisha na kutuweka katika madaraja.

Kuna mwanamke anakuwepo kwenye vikao vya kupanga mahari?
Kuna mwanamke anapenda yaliyomkuta yeye yamkute na bintiye?
Kuna kahaba anayefundisha mwanae wa kike kazi?
Ni wanawake wangapi wanalea watoto bila baba zao?
Wanajiuza ehh?

Mnatutukana nyumbani, vijiweni na humu pia.
Mnaendelea kushirikiana kudhalilisha utu wa wanawake.
Eti wanawake wanajiuza!

Si ni nyie kwa u.m.a.l.a.y.a wenu mnaoenda mnatafuta mabikra wachanga na kuwahadaa na vijimali vyenu, leo hawawezi sahau siku waliyotoa utu wao kwa wanaume waliodhani wanaheshimu. Mnasimama kusema wanajiuza.

Si ni nyie mmewazalisha wake zenu,mkisisitiza watoto waitwe kwa majina yenu hamjali familia zenu mnaondoka mnapeleka pesa kwa makahaba wawafanyie mnayotaka. Leo mnasema wanawake wanajiuza.

Si ni nyie mnaozalisha mabinti wa watu kwa hila za ahadi za ndoa halafu mnatelekeza watoto, mnadai siyo “wife material”. Kabla alikuwa malkia huyu, leo anajiuza.

Si ni nyie mnaita wake zenu m.a.l.a.y.a na pengine kuwapiga ngumi mkijificha kwenye sura ya “kichwa cha familia” halafu baadaye mkiwaletea watoto wa matunda ya ufuska wenu mkitaka wawalee, leo mnasema wanajiuza.

Si ni nyie mlio maofisini na vyuoni mnawajaribu wanawake waliobahatika kusoma mkitaka mlale nao ndo mwape stahili yao. Hao nao hujiuza!

Si ni nyie mnaogongana na watoto wenu mkishindana kuwatumia “mahousegirl” kama vyombo vya kujistarehesha bila gharama. Hii ni part time ehh?

Si ni nyie mnawabaka watoto wadogo pengine watoto wa ndugu zenu bila haya wakipata mimba mnawalazimisha kutoa mimba wangali vigoli. Wanajiuza hawa ehh?

Si ni nyie mnasema mnapenda huduma ya kikahaba na kuwalazimisha pengine wake wenu kushiriki mkiwatumia kinyume cha maumbile kukidhi haja zenu, eti akulidhishe kimapenzi. Hawa wameliwa kwa kujiuza,eeeh!

Si ni nyie mnaowafuata watoto wanaolingana na watoto wenu mnabebwa kwenye vifua vya watoto hawa bila aibu. Wanajiuza?

Si ni nyie mnawalaghai mabinti wanapiga picha za ngono. Picha hizo sura za mabinti hawa tu zinaonekana za kwenu huwa mnaficha. Malipo ya kujiuza hayo ehh?

Si ni nyie kwa tamaa zenu mnabaka hadi viumbe vingine ili mridhishe hamu zenu. Hapa bei sokoni iko juu ehh?

Si ni nyie mnaokaa vijiweni kutathimini ya nani tamu ipi hajaguswa mnawekeana dau kumpata bikra. Mpango wa kupata bidhaa adimu ehh?

Jamani mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Kama wazazi mmetuita m.a.l.a.y.a tungali wadogo wakati hatujui mtu mme, tumeshuhudia mkiwanyanyasa mama zetu kwa tabia zenu mbaya huku mkitaka wawape heshima tumekua katika jamii ambayo mwanamke si mtu ni bidhaa, wengine mmewachagulia maisha mkiwanyima hata elimu achilia kina sie tusiojua sura za baba zetu. Mnataka nini?

Naandika haya baada ya moyo wangu kushindwa kuvumilia kuendelea kutukanwa namna hii. Nakataa udhalilishwaji huu.

Ole wenu! Ole wenu! Ole wenu mnaojipa moyo kuwa wanawake wanajiuza na kuendelea kuwafanyia maovu.
.
 
Hapa sijaelewa, naweza kuchangia, nikaishia kula makofi.Kuna mtu atakuwa amechokza hawa Mama zetu.Usiku mwema wapendwa
 
Somtyms huwa nikiona mtoto baba kamtekelza mtoto nahis labda may b it was a busines na mkataba ulishaisha!Tamaa mbaya sn
 
Dillish wa kwetu unashindwa kujua hata wale wanaojipanga buguruni ni mama,dada,bidi,shangazi zetu!Ila waogopwe kwa hayo
 
Last edited by a moderator:
Dah ni kweli yamenisikitisha,ndio mara yangu yabkwanza kuona status ambayo haina pingamizi hata kidogo,yalowemo yooote ni ukweli mtupu,maana kila mstari ninaousoma ni kweli tena kweli tupu,dah jamani wanawake ndio mama zetu tuwapunguzie kuwasakama na kuwasingizia wakati vyanzo ni wanaume
Pole sana tena pole jamani.
 
Mimi kidume ila wakati mwingine nawahurumia sana wanawake hasa mnapokutana na changamoto kama hizi. Kiukweli uzi huo unaouzungumzia niliuona nikawa sijavutiwa kuusoma baada ya kukaa na kutulia ilibidi niupitie kidogo. Kwakweli inasikitisha na inaumiza sana maana nahisi kama hata mama yangu mzazi dada na shangazi wote wametukanwa ila ilinibidi nipuuzie tu nikakosa cha kucomment pale. Kumbuka kila mtu ana akili zake na anaweza kuandika atakacho na wewe ulipopost uzi wako ingefaa sana ukajua kwamba si wote wanaafiki kitu kama hicho. Ila poleni sana kwa waliokereka.
 
Umeongea maneno mengi bi dada hebu kunywa maji kwanza.

MM-0016-09-MINALBA-25L.jpg



Nalog off
 
katika siku ambazo nimehisi tumbo la uzazi linauma ni leo.....nikimwangalia mwanangu sasa......baadae amekuwa ndo anakaa kijiweni na wenzake anashadadia kabisa KILA MWANAMKE ANAJIUZA wenzake .....wanamuuliza mpaka mama yako....anasema ndio ......dah kiukweli baada ya kufikilia hvyo nimejikuta nalia......na si kawaida yangu kuwa macho mida hii....

EE MUNGU MLINDE MWANANGU....KINYWA CHAKE KINENE MAZURI.....NA AWE NA BUSARA.....NA HESHIMA KWA WATU WOTE BILA KUJALI JINSIA.....AMEN
 
katika siku ambazo nimehisi tumbo la uzazi linauma ni leo.....nikimwangalia mwanangu sasa......baadae amekuwa ndo anakaa kijiweni na wenzake anashadadia kabisa KILA MWANAMKE ANAJIUZA wenzake .....wanamuuliza mpaka mama yako....anasema ndio ......dah kiukweli baada ya kufikilia hvyo nimejikuta nalia......na si kawaida yangu kuwa macho mida hii....

EE MUNGU MLINDE MWANANGU....KINYWA CHAKE KINENE MAZURI.....NA AWE NA BUSARA.....NA HESHIMA KWA WATU WOTE BILA KUJALI JINSIA.....AMEN

Pole sana , siku zote ukimya husaidia
 
Back
Top Bottom