Kigoma Region Tanzania
JF-Expert Member
- May 25, 2021
- 229
- 593
Kusafiri na reli ni zaidi ya safari, maana utapata fursa ya kuona mandhari nzuri ya nchi ya Tanzania, uoto wa asili, mbuga za wanyama, huduma bora za chakula katika mgahawa ndani ya treni pamoja na huduma za afya.
Usafiri umepangiliwa kwa kuzingatia ratiba zilizowekwa kwa mpangilio ukilinganisha na aina nyingine za usafiri.
Treni hii ya Ordinary inatoka Dar es salaam siku ya Jumapili saa 9:00 Alasiri na huwasili Mkoani Kigoma siku ya Jumanne saa 12:20 asubuhi.
Nauli
Daraja la 3 mtu mzima ni TZS 27,600, mtoto ni TZS 13,800
Daraja la 2 mtu mzima ni TZS 55,600, mtoto ni TZS 27,800
Daraja la 1 mtu mzima ni TZS 76,100, mtoto ni TZS 38,050
*Watoto wenye umri kati ya 0-3 hawalipiwi nauli
Nakukaribisha Kigoma, nitakupokea station.
Kigoma Railway station
Usafiri wa Train ya Kigoma (TRC) ni nafuu zaidi ukilinganisha na aina nyingine za usafiri kutokana na kuwepo kwa madaraja tofautii ambayo yanatoa fursa kwa watu wa vipato vya aina zote kusafiri.
Kazuramimba village
Unapokuwa kwenye mabehewa ya abiria unapata nafasi ya kuhama kutoka behewa moja kwenda behewa linginena kufurahia muonekano mzuri wa maeneo asilia na vivutio mbalimbali.
Njoo Kigoma utembee hata kwa siku mbili.
Karibu Kigoma
Treni hii ya Ordinary haina ubaguzi wa mizigo, unaweza kununua vitoweo ukasafiri navyo.
Mwanamke akiuza jogoo wake kwa mwanaume huyu kwa gharama ya shilingi 5,000
Jogoo wa 5000
Treni hii ya Ordinary ina Mabehewa ya Daraja la Kwanza Kulala, Daraja la Pili Kulala, Daraja la Pili Kukaa na Daraja la Tatu ikiwa na behewa maalum la Mgahawa kwa ajili ya Chakula na Vinywaji. Maisha ni rahisi sana.
Pata fursa ya kukutana na watu wapya ndani ya Treni ni furaha tupu.
Kigoma inapendeza.
Unaruhusiwa kununua chochote utakacho kwa bei nafuu kabisa, ukitaka Muhogo mbichi, ndizi mbivu, miwa n.k
Ukiwa ndani ya Behewa la Treni wewe ni Tajiri, lazima uletewe bidhaa za kununua.
.....................
Hili ndio jengo la station, wewe panda train ya Deluxe au Ordinary njoo Kigoma utembee, watu wa mji huu ni wenye ukarimu.
Kwenda sehemu sio lazima uwe na jambo maalumu, kuja kupaona Kigoma hilo ni jambo kubwa sana utakua umefanya maishani mwako. Kukanyaga ardhi hii maarufu ni jambo lenye historia kwako,
Njoo hapa Kigoma. Upate vitu vipya vya kufungua akili.