Njia ya msalaba
Sala mbele ya altare
Ee mkomboz wangu nimekuja leo kufuata njia ile uliyo shika siku ya kufa sadaka yetu,
Nimetubu dhambi zangu zote, nataka kugeuza mwenendo wangu, ninaomba kwako niwapatie roho za waamini marehemu waliomo toharani, rehema zote zilizotolewa na kanisa kwa njia ya msalaba nawe Maria bikira mtakatifu. Uliye fuata njia ile nyuma ya mwanao YESU KRISTO. Uniangalie kwa wema unitie moyo mkuu. Nisipende kazi tena nikivumilia kazi na usumbufu na mateso na matukano yatayo nipata AMINA