Kwanini Zitto nisikuite msaliti?

Kwanini Zitto nisikuite msaliti?

Sasa hivi anapango wa kumpa fisadi mkuu chama chake, bisheni tena harafu akimpa shangaeni tuuu
 
Tulieni dawa iingie. Tuliwaambia saccos ya CHADEMA ilijengwa na Zitto na Mbowe hamkutaka kuelewa. Sasa tupo Tabora na watu wengi utafikiri mji mzima umehamia hapa!
 
Mlipomfukuza mlitaka adharirike ili mseme chama ni zaidi ya zito.sasa nafikiri sasa mnaamini kwamba zito alikuwa ni zaidi ya chadema.wachaga naona hamuamini kilichotokea.

Mi nimewakumbusha tu wafuasi wa ZZK msiwe wapumbavu, alikataa amekiri nyinyi wafuasi mpo kama kupe hata ng'ombe kishachinjwa mpo tu kwenye ngozi.
 
Nataka kuweka kumbukumbu vizuri, wakati ule CDM inamwambia ZZK kuwa ameanzisha chama alikataaa na wafuasi wake ndani na nje ya JF walipinga, nataka niwakumbushe wafuasi wa ZZK wasiwe wapumbavu. Hii kauli aliitoa Nyerere akimwambia Kawawa asiwe mpumbavu kama Lowassa, wakati EL alitaka nyerere aende monduli kumpigia kampeni kusafisha hali ya hewa kwani kwa Mwalimu kumkataa EL kwa madai ya RIshwa na Ufisadi kwa maoni ya EL angehatarisha asipate hata UBUNGE.

Sasa jiorodhezesheni hapa wale ambao mlikuwa mnapost kupinga kuwa ZZK hajaanzisha chama.

Post zinaonesha kuwa nyinyi kweli mko tayari kusapoti msichokijua, sijui pia shida ni nini, tumbo? au magari hapa mjini? shida ni nini??? wafuasi wa ZZK je hawana uwezo wa hela na akili au? alikataa nanyi mkamuunga mkono kumbe intelegensia yetu Kubwa, haiwezi fanya makosa, jiorodhesheni kwa ajili ya kupata msaada wa ada mkaongeze maarifa. Maarifa madogo, huwezi ona jambo kabla halijatokea wewe ni sawa na mtoto mdogo wa miaka chini ya mitano, JF sio saizi yenu.

Nawasilisha
...huyu bwana zitto mimi nilikuwa mtu wake but nilikuja kumsikia anasema eti hiyo act alianzisha..basi nakamjua huyu bwana anatumika na anafanya kazi ya kuharibu mageuzi,yaani yeye amegeuza deal mageuzi wakati miaka 23 tunaangaikia...hafai.
 
...huyu bwana zitto mimi nilikuwa mtu wake but nilikuja kumsikia anasema eti hiyo act alianzisha..basi nakamjua huyu bwana anatumika na anafanya kazi ya kuharibu mageuzi,yaani yeye amegeuza deal mageuzi wakati miaka 23 tunaangaikia...hafai.

Wewe ni Kiboko, UNAKIRI na unasonga mbele, achana na kina simiyu yetu abubakar Shekua, hafai hafai ukielewa ukweli achana naye ni kama mchawi iwapo hajakuroga leo kesho atakuroga tu.
 
nataka kuweka kumbukumbu vizuri, wakati ule cdm inamwambia zzk kuwa ameanzisha chama alikataaa na wafuasi wake ndani na nje ya jf walipinga, nataka niwakumbushe wafuasi wa zzk wasiwe wapumbavu. Hii kauli aliitoa nyerere akimwambia kawawa asiwe mpumbavu kama lowassa, wakati el alitaka nyerere aende monduli kumpigia kampeni kusafisha hali ya hewa kwani kwa mwalimu kumkataa el kwa madai ya rishwa na ufisadi kwa maoni ya el angehatarisha asipate hata ubunge.

Sasa jiorodhezesheni hapa wale ambao mlikuwa mnapost kupinga kuwa zzk hajaanzisha chama.

Post zinaonesha kuwa nyinyi kweli mko tayari kusapoti msichokijua, sijui pia shida ni nini, tumbo? Au magari hapa mjini? Shida ni nini??? Wafuasi wa zzk je hawana uwezo wa hela na akili au? Alikataa nanyi mkamuunga mkono kumbe intelegensia yetu kubwa, haiwezi fanya makosa, jiorodhesheni kwa ajili ya kupata msaada wa ada mkaongeze maarifa. Maarifa madogo, huwezi ona jambo kabla halijatokea wewe ni sawa na mtoto mdogo wa miaka chini ya mitano, jf sio saizi yenu.

Nawasilisha

acha umbea mwanaume wakati act inaanzishwa zitto alikuwa chadema
 
...huyu bwana zitto mimi nilikuwa mtu wake but nilikuja kumsikia anasema eti hiyo act alianzisha..basi nakamjua huyu bwana anatumika na anafanya kazi ya kuharibu mageuzi,yaani yeye amegeuza deal mageuzi wakati miaka 23 tunaangaikia...hafai.

Huyo usaluti alofanya angeufanyia nxhi za wenzetu sijuu ......
 
Chadema hawafuatilii tena maendeleo ya saccos yao. Macho na Masikio yao yako kwa Zityo na ACT

Unataarifa kuwa huko kanda ya Pwani kuna mafunzo kwa viongozi wa cdm na timu nzima ya ushindi hapo October au unabwabwaja tu? CDM ni taasisi kubwa haiwezi kuhangaika na vidagaa badala ya sangara ccm
 
Ulishawahijuamiakayako?
- Sijawahi ona kokote siasa inakofanywa mwanachama wa chama kimoja kwa wakati huohuo ni mwanzilishi wa chama kingine cha siasa, sijawahi.

- Sijawahi kuona mtu anajiunga na chama fulani baada ya siku tano anapewa uongozi mkuu wa chama hicho, sijawahi

- Sijawahi kuona popote siasa inapofanywa, mwenyekiti wa chama yupo chini ya mtu fulani. Yahani kikatiba kabisa kuna mtu yupo juu ya mwenyekiti, hii pia sijawahi kuona.

- Sijawahi kuona popote pale chama cha upinzani kukipinga chama cha upinzani na si chama tawala. AGAINST CHADEMA TANZANIA(ACT). Kwa maneno au hata vitendo. Chama kinafanya sherehe kikipata wafuasi wa upinzani kuliko wa chama tawala.

- Sijawahi kuona chama cha upinzani kinafadhiliwa na chama tawala kiuchumi na kimikakati. Tumefanya uzinduzi wa chama chako Zuberi kwa gharama kubwa sana, air time ITV, chakula, ukumbi expensive, na mbwembwe nyingi. Lakini mbona hujawahi kuchangisha pesa toka kwa wanachama wako? Kama kuna mtu anachangia ni nani huyo? Mtamlipaje baadae?

- Sijawahi ona chama cha upinzani popote pale siasa inapofanywa, wafuasi wake ni wale wanachama na wafuasi wa chama tawala. Le mutuz, laki si pesa, musa alani n.k, hii nayo sijawahi ona.

Kwa yote hayo juu Zuberi kwa nini nisikuite kwamba wewe ni msaliti halisi wa demokrasia hapa nchini. Kama kweli wewe siyo msaliti mbona hujawahi kujitokeza na kukataa zile namba za simu walizozitoa chama chako cha zamani kuwa zilitumika katika ufisadi? Mbona sijasikia kuikana ile akaunti ya benki wa yule dada kule ujerumani?

UKINIJIBU HAYO KWA UFASHA WEWE KWELI SI MSALITI.
 
Wanajamvi heshima sana,

Ngongo wa JF ajiunga na ACT Wazalendo chama makini kinachoongozwa na Kiongozi Mkuu --------- Zitto Zuberi Kabwe.Zipo sababu nyingi zilizonifanya nijiunge na chama hiki makini leo nitazitaja sababu chache tu ila nikipata muda nitaongeza nyingine ambazo hata wewe zinaweza kukushawishi.

Mosi,Ngongo ni muumini wa siasa za kufuata watu usiniulize kwanini ndivyo nilivyozaliwa.Nimeamua kumfuata --------- Zitto kwasababu katika yeye nimeyaona matendo na misimamo yake isiyoyumba wala kutetereka.Ikumbukwe Zitto Kabwe katika nafasi ya naibu katibu mkuu alishiriki kuondoa minyukano ya kugombea madaraka,sikuwahi hata mara moja kumwona Zitto akitamani nafasi ya Mwenyekiti wa chama au kiongozi mkuu wa upinzani bungeni ndio maana hata alipojiunga na ACT alikataa katu katu nafasi ya Mwenyekiti wa chama cha ACT.Katika Hili Zitto kawazima na kuwaacha hoi bin taabani wale wote waliokuwa wakimpakazia kwamba yeye ni mwenye tamaa na uchuu wa madaraka.

Zitto ni mjamaa mwenye kufuata misingi ya Mwl Nyerere na Mimi ni mjamaa mwenye kufuata mkondo huo huo ni kwanini nisijiunge na ACT Wazalendo.Mimi Ngongo namiliki Nyumba 6,Mashamba makubwa 3,Magari 5 si ya kiafahari a) Land Cruiser VDJ 201 b) Ranger Rover 2015 c) Hammer d) Bugatti Veyron e) Lamborghini Roadster.Vimali vyote hivi nimevipata kupitia siasa za Tanzania ikiwa ni pamoja na kukataa posho,kukataa misamaa ya kodi wanayopewa wabunge wote wa bunge la muungano.Bahati nzuri Kiongozi Mkuu si mpenda mali wala madaraka wote tunafuata siasa za kijamaa ingawa katika dunia ya leo zimeshindwa sijui ni jinsi gani mimi na Zitto tutaweza kulifanikisha hili labda kwakuwa sisi tutakuwa mfano na wengine watatuiga.

Pili Ngongo kaamuwa kujiunga na ACT kwakuwa kiongozi mkuu ni mkweli kila anachokisema ndicho anachokifanya hajawahi hata mara moja kusema kitu asichokimaanisha.Endelea kunifuata taratibu nikuonyeshe Kiongozi mkuu alivyo mkweli daima.Zitto alinukuliwa na wanahabari akikanusha vikali

a) Kwamba yeye haijui ACT wala hausiki na uanzishwaji wake.

b) Kwamba yeye hawezi kuhama CDM atakuwa mtu wa mwisho kuhama CDM

c) Kwamba amejipanga kugombea urais mwaka 2015 huku akijua kakosa sifa ya kugombea (umri) hata katiba pendekezwa haimruhusu

d) Kwamba ni Zitto Kabwe aliyeliibua sakata la ESCROW akina Kafulila walidandia tu.

e) Hajui chochote wala hana mahusiano na Prof Kitila & Samson Mwigamba.Leo ni wamoja labda ni kwa bahati mbaya nakuachia wewe msomajo kutengua hiki kitendawili ingawa sikupi mji katu.

f) Kwamba angeachana na siasa baada ya kipindi chake cha ubunge kwisha mwaka 2015.Zitto leo ni kiongozi mkuu tena baada ya kufukuzwa ubunge aliwaaga wabunge angerejea mjengo tena.Hii inapingana na kauli yake kwamba angeecha siasa na kwenda kufundisha chuo kikuu.Hii tunaweza kumsamee kwakuwa nafasi ya kiongozi mkuu si nafasi ya kisiasa sanaa anaweza kugawa muda wa kufundisha chuo kikuu na muda mwingine wa kiongozi mkuu usishangae hizi ndio siasa za kitanzania nchi ya watu wasiopenda kufikiri sana ukiweza kubwa bwaja utawasomba wengi.Mbona Gwajima anafufua wafu hakuna anayehoji wala kuuliza makaburi yao kanunua chopa mnaanza wivu wenu wa kike.Nasema nimeamua kumfuata Zitto ACT ndio habari ya mjini mengine kelele ebooo.

Zitto ndio mkombozi wetu bwana wengine wote njaa,Zitto ni mwanasiasa pekee aliyekataa kupokea posho hata akifanya ziara za kikazi NSSF,TANAPA..... na mashirika mengine mengi ya umma hachukui hata senti tano.Kuna kipindi Zitto na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF walisafiri na timu yetu ya taifa Zitto alijilipia nauli na malazi mwenyewe hakuchukua ndururu ya NSSF.

Zitto kama mwenyekiti wa PAC kila mara amekuwa mfano bora wa kukataa posho za mashirika ya umma wanayoyakagua ingawa kuwana kipindi payment voucher za Ngorongoro Creater Area Authority zilionyesha Zitto alikuwa akilamba allowances hiyo haitoshi kumfanya Zitto fisadi labda hizo voucher ziligushiwa kumchafua kiongozi mkuu.

Naomba kuwasilisha kwa mjadala wa afya hoja kwa hoja na si viroja.

Hii Sana'a uliyopiga hapa kama ningekuwa mtoa tuzo ningekutunuku kwa kazi bora ya Sana'a 2015 hapa JF. Umemaliza kila kitu
 
Back
Top Bottom