Kwanini Zitto nisikuite msaliti?

Kwanini Zitto nisikuite msaliti?

mtakufa kwa pressure mwaka huu....unazuia watu kuja urambo una hati miliki ya nchi hii wewe.....ebooo!
 
Wanajamvi heshima sana,

Ngongo wa JF ajiunga na ACT Wazalendo chama makini kinachoongozwa na Kiongozi Mkuu --------- Zitto Zuberi Kabwe.Zipo sababu nyingi zilizonifanya nijiunge na chama hiki makini leo nitazitaja sababu chache tu ila nikipata muda nitaongeza nyingine ambazo hata wewe zinaweza kukushawishi.

Mosi,Ngongo ni muumini wa siasa za kufuata watu usiniulize kwanini ndivyo nilivyozaliwa.Nimeamua kumfuata --------- Zitto kwasababu katika yeye nimeyaona matendo na misimamo yake isiyoyumba wala kutetereka.Ikumbukwe Zitto Kabwe katika nafasi ya naibu katibu mkuu alishiriki kuondoa minyukano ya kugombea madaraka,sikuwahi hata mara moja kumwona Zitto akitamani nafasi ya Mwenyekiti wa chama au kiongozi mkuu wa upinzani bungeni ndio maana hata alipojiunga na ACT alikataa katu katu nafasi ya Mwenyekiti wa chama cha ACT.Katika Hili Zitto kawazima na kuwaacha hoi bin taabani wale wote waliokuwa wakimpakazia kwamba yeye ni mwenye tamaa na uchuu wa madaraka.

Zitto ni mjamaa mwenye kufuata misingi ya Mwl Nyerere na Mimi ni mjamaa mwenye kufuata mkondo huo huo ni kwanini nisijiunge na ACT Wazalendo.Mimi Ngongo namiliki Nyumba 6,Mashamba makubwa 3,Magari 5 si ya kiafahari a) Land Cruiser VDJ 201 b) Ranger Rover 2015 c) Hammer d) Bugatti Veyron e) Lamborghini Roadster.Vimali vyote hivi nimevipata kupitia siasa za Tanzania ikiwa ni pamoja na kukataa posho,kukataa misamaa ya kodi wanayopewa wabunge wote wa bunge la muungano.Bahati nzuri Kiongozi Mkuu si mpenda mali wala madaraka wote tunafuata siasa za kijamaa ingawa katika dunia ya leo zimeshindwa sijui ni jinsi gani mimi na Zitto tutaweza kulifanikisha hili labda kwakuwa sisi tutakuwa mfano na wengine watatuiga.

Pili Ngongo kaamuwa kujiunga na ACT kwakuwa kiongozi mkuu ni mkweli kila anachokisema ndicho anachokifanya hajawahi hata mara moja kusema kitu asichokimaanisha.Endelea kunifuata taratibu nikuonyeshe Kiongozi mkuu alivyo mkweli daima.Zitto alinukuliwa na wanahabari akikanusha vikali

a) Kwamba yeye haijui ACT wala hausiki na uanzishwaji wake.

b) Kwamba yeye hawezi kuhama CDM atakuwa mtu wa mwisho kuhama CDM

c) Kwamba amejipanga kugombea urais mwaka 2015 huku akijua kakosa sifa ya kugombea (umri) hata katiba pendekezwa haimruhusu

d) Kwamba ni Zitto Kabwe aliyeliibua sakata la ESCROW akina Kafulila walidandia tu.

e) Hajui chochote wala hana mahusiano na Prof Kitila & Samson Mwigamba.Leo ni wamoja labda ni kwa bahati mbaya nakuachia wewe msomajo kutengua hiki kitendawili ingawa sikupi mji katu.

f) Kwamba angeachana na siasa baada ya kipindi chake cha ubunge kwisha mwaka 2015.Zitto leo ni kiongozi mkuu tena baada ya kufukuzwa ubunge aliwaaga wabunge angerejea mjengo tena.Hii inapingana na kauli yake kwamba angeecha siasa na kwenda kufundisha chuo kikuu.Hii tunaweza kumsamee kwakuwa nafasi ya kiongozi mkuu si nafasi ya kisiasa sanaa anaweza kugawa muda wa kufundisha chuo kikuu na muda mwingine wa kiongozi mkuu usishangae hizi ndio siasa za kitanzania nchi ya watu wasiopenda kufikiri sana ukiweza kubwa bwaja utawasomba wengi.Mbona Gwajima anafufua wafu hakuna anayehoji wala kuuliza makaburi yao kanunua chopa mnaanza wivu wenu wa kike.Nasema nimeamua kumfuata Zitto ACT ndio habari ya mjini mengine kelele ebooo.

Zitto ndio mkombozi wetu bwana wengine wote njaa,Zitto ni mwanasiasa pekee aliyekataa kupokea posho hata akifanya ziara za kikazi NSSF,TANAPA..... na mashirika mengine mengi ya umma hachukui hata senti tano.Kuna kipindi Zitto na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF walisafiri na timu yetu ya taifa Zitto alijilipia nauli na malazi mwenyewe hakuchukua ndururu ya NSSF.

Zitto kama mwenyekiti wa PAC kila mara amekuwa mfano bora wa kukataa posho za mashirika ya umma wanayoyakagua ingawa kuwana kipindi payment voucher za Ngorongoro Creater Area Authority zilionyesha Zitto alikuwa akilamba allowances hiyo haitoshi kumfanya Zitto fisadi labda hizo voucher ziligushiwa kumchafua kiongozi mkuu.

Naomba kuwasilisha kwa mjadala wa afya hoja kwa hoja na si viroja.
 
Mhmmm we mtu wewe kweli unajua kuzunguka mbuyu.
Wavivu wa kusoma wengi hawata kuelewa.
 
hongera ngongo kwa kujiunga na chama chetu cha wazalendo na wapiga dili maarufu wa fedha za ccm...unakaribishwa mwaka ndio huu wa kupiga hela........kuna watu wanaweza kupotea maboya kwenye huu uzi
 
Duuh?! Na mimi najiunga na wewe Mr. Ngongo.. Tukamuunge ZZK kwenye chama chetu cha kizalendo na chenye kufuata mingi ya kijamaa.
 
ha ha ha - tangulia na mimi naiwinda kadi ya huyu mzalendo numberi one Tanzania. Unajua mtu kufikia hatua ya kukataa hata kiinua ngongo chake cha Ubunge basi huyu ni mzalendo na mjamaa wa kweli ukimwondoa Mwalimu.

Ngongo upo sahihi.
 
kesho naenda kuchukua kadi hiki ndio chama bwana sio vile vingine.....hivi ofisi zao zipo wapi hapa mwanza ? mwenye kujua anijuze humu
 
Hahahahahahah...............Gud...nimekupata mkuuu...Kimwili upo ACT lakini Kiroho upo Chademaa, ila hapa ili mtu akuelewe lazima asome neno kwa neno...
 
Mkuu Ngongo Hongera...

Hizo sehemu zimetokea dash unaweza kuandika cheo chake kingine cha CEO au Mfalme.
 
Last edited by a moderator:
sku izi ajira kweli njenje....unalipwa sh ngapi na CDM kwa kazi hii......hehehheehheh tutaona mengi mwaka huuu :shocked:
 
Back
Top Bottom