Kwanini Zitto nisikuite msaliti?

Kwanini Zitto nisikuite msaliti?

Unajua lini mikakati yake ya usaliti ilianza? Unajua lini alianza kuchukiwa na chama chake na chanzo kilikuwa nini? Kwa mawazo yake na mikakati ya chama chake ingeingilianaje na chama chake cha zamani? Ni lini alikuwa na maono ya kujenga chama cha 'ujamaa'? Wewe! Watch out....we are serious for our nation and its liberation for the second time.

Tatizo la wanamapinduzi wa tanzania na tunaojiita wanamapinduzi wa kweli;usaliti kwetu ni mtu anapopishana mawazo na ww;hata kama alianza mipango zamani wakati ule na wakina prof mkumbo na mwigamba kwa ninachokijua mm;ambacho kipo wazi na kwangu mm bado ule c usaliti ni mawazo tu ambapo wangekaa kama chama na kuyamaliza.

Baada ya hapo ndo zito akaona kabisa kiama chake hakipo mbali;ndo akajipanga strategically kukabiliana na hali halisi na mpaka sasa maisha yanaendelea.

Sitetei usaliti ila usaliti wa zito kwangu mm hadi sasa naona ni simba na yanga;ni mawazo yangu lakini na sio lazima yawe sahihi
 
Huna haja ya kuwa na hofu basi, maana wewe na mimi ndio wananchi hao, tulia kama ana makosa tutamhukumu tu na kama alionewa waliomuonea tutawahukumu pia.

Sina hofu chembe kaka, maana usaliti wake tumeufahamu bado wewe na ninaamini muda si mrefu utaziona rangi zote za zito kabwe
 
inasikitisha sana october ukawa wakiwa na vita mbili
1.dhidi ya ccm
2. dhidi ya act
 
Nimejaribu kufuatilia kwa utulivu juu ya mwenendo wa kiongozi mkuu wa ACT- Wazalendo Zitto Kabwe na kwa kweli sijaelewa dhamira yake ni nini hasa kisiasa.

Wapinzani wanaungana ili kung'oa kisiki kilichoshindikana kwa muda wa miaka takribani miaka 20 sasa.

Ninapofuatilia tabwe zake na mikakati yake ya kisiasa naona anakilenga sana chama chake cha CHADEMA na naona ni kama ametumwa na Watawala kuvuruga upinzani hapa nchini.

Ombi langu kwako ewe Zitto Kabwe kama kweli umedhamilia kuleta upinzani wa kweli katika Taifa letu ni vema ukawa na ajenda za kujenga upinzani imala kwa kueneza sera za chama chako na hasa dhidi ya chama Tawala ili basi Chama chako kisaidie kuondoa chama tawala na wananchi tuweze kupumua dhidi ya Rushwa na Ufisadi unaolitafuna Taifa letu la Tanzania.

Kuanzisha chama na kuanzisha mapambano dhidi ya vyama vya upinzani badala ya chama tawala ni kuleta mkanganyilko juu ya hasa malengo ya chama chako katika demokrasia ya nchi ni za namana gani?

Ni vizuri hata kama una chuki na vyama vingine ambavyo haviko madarakani ukaanzisha upinzani dhidi ya watunga sera na si wapinzani wenzako!

Najua ujumbe huu utausoma humu katika jukwaa letu la kijamii na niombe wadau wote msaidie katika kutoa ushauri wa kujenga na si kiushabiki zaidi.

Tujaribu kujenga kizazi chenye fikra pevu na zenye mashiko kwa manufaa ya Taifa na si kufanya mambo yanaooyesha wazi upuuzi wetu wa kihistoria.

ni vema tukajifunza kuvumiliana na si kukomoana na kulipiziana visasi kama anavyojaribu kufanya Zitto dhidi ya CHADEMA!

Na ukwelii ni kwamba akiendelea na mwenendo huu nakuhakikishia Zitto kuwa kwa Tanzania hii huwezi kwenda mbali na mwisho utakuja kurudi kwenye vyama hivi ulivyoviacha na kuanzisha chama chako kipya na huu ndiyo ubinafsi ambao uliuonesha ndani ya chama chako cha awali.

Nakutakia kila la heri!!
 
Wasiojua watafute magazeti ya Mwanahabari yaliyo na habari ya chama cha wazalendo watajua chama hicho kimeanzishwa na kina nani. Hatutaki chama kinachoanzia Lumumba alafu kinaitwa chama cha upinzani!
 
Hali sasa imegeuka kabisa ZZK hapambani na CHADEMA bali na upinzani wote kwani anajua kuwa kigoma ni ngome ya NCCR-MAGEUZI lakini yeye anataka iwe ngome ya ACT, Na amewataka wabunge wa kigoma kama wanataka kuendelea na majimbo hayo wajiunge na ACT, Aidha katibu wake Samsoni Mwigamba alinukuliwa kuwa ACT watahakikisha wanaisambaratisha CUF katika maeneo ya pwani. HIvyo dhumuni la ACT ni kudunisha nguvu ya UKAWA
 
Hao chadema ndo wanaeneza chuki kwa. Zito,mara msaliti sijui na yeye hajawajibu ila wafuasi wake lazima warespond sasa kuna kosa hapo
 
Zitto kila siku anaubomoa utawala wa Kikwete....na ameichachafya kweli Serikali......ona Jaji werema alivyofurahia kuona zitto ameshindwa kesi mahakamani.....ona ngeleja alivyojitetea kwenye baraza La maadili kwa kumchafua zitto......usipoipa akili yako ushabiki ni rahisi kugundua kuwa zitto ni mpinzani wa CCM na sio wa wapinzani
 
Zitto kila siku anaubomoa utawala wa Kikwete....na ameichachafya kweli Serikali......ona Jaji werema alivyofurahia kuona zitto ameshindwa kesi mahakamani.....ona ngeleja alivyojitetea kwenye baraza La maadili kwa kumchafua zitto......usipoipa akili yako ushabiki ni rahisi kugundua kuwa zitto ni mpinzani wa CCM na sio wa wapinzani

Zitto ni msaliti na mnafiki. Ubunge atausikia kwenye bomba.
 
Usishangae maana hata aliyekuwa malaika mkuu Lucifeli alimgeuka Mwenyezi Mungu. Zitto aliigeuka Chadema miaka mingi
 
Zitto yuko kazini tangu 2006 lakini timu imara ys usalama wa chama ilikuwa imara kufuatilia nyendo zake mpaka alipokamatwa kama mjusi kwenye mlango. Sasa kaanzisha chama cha kuvuruga Ukawa, umeshindwa ndani, utaweza ukitoka nje?
 
"Safari ya mbwa haijulikani" hawa watu wanaonesha wana fedha sana na waliwahi kuhaidi kuweka mapato na matumizi kila baada ya miezi tatu nyie ni mashaidi hakuna kitu kama hicho wamekula kona wote, wanasema ati wanachangishana kweli! hatari bado ni siasa za wizi, uongo, uzandiki, fitina unaa umalaya mdogomdogo na hujuma juu ya makabwera wenzetu. Tujue hakuna mtu mwenye akiri safi hasiyejua kuwa hii ni propaganda ya CCM kuendelea kutawala kiurahisi kupitia washenzi wachache kama ngome ya usaliti, we will fight!
 
Back
Top Bottom