The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,355
- 17,321
Ukikutana na kila mzazi leo anataka shule inayofaulisha, wazazi wako busy kuulizia ufaulishaji wa shule.
Juzi matokeo yalitoka kila mzazi ama mlezi anakata kujua shule hiyo division one ngapi, sijui nini.
Swali langu, kwa nini wazazi ama walezi wameshikwa sana na ufaulu wa watoto, division one, two na vitu kama hivyo?
Hii obsession ya ufaulu inafanya hata shule ama waalimu watafte namna ya kuiba mtihani ili waonekane wanafaulisha.
Kinachonisikitisha, wao wanaopata division one mbona hatuoni mchango wao wowote wa maana kwenye maisha yetu ya kila siku?
Kila mwaka nchi hii tuna division one za 7 zaidi ya 500, division one za 3 zaidi ya 200, hizo division zina mchango gani kwenye jamii?
Watoto wanaopata division one hizo mbona ni weupe sana vichwani?
Mimi kama mlezi, natamani kuona watoto wakiwa na uwezo wa kuhoji (questioning mind) kufikiri (reasoning skills), kutafakari na kuchambua (analytical skills), vitu ambavyo ndio Dunia ya sasa inachokitaka na sio huu utaratibu wa kukaririsha watoto ili wapate division one ama two.
Mbaya zaidi sioni kama wazazi ama walezi mnaona kama huu mfumo ni mbovu, mfumo wa kuwakaririsha watoto, mfumo wa kuwafanya wasifikirie, wasihoji.
Kuna mtoto wa kaka yangu hapa ana division one ya point 7 lakini nachokiona kichwani mwake ni mweupe kabisa, hata baba yake anauliza huyu amepataje hii one ya 7.
Natafta hela mtoto wangu asome Cambridge ama IB schools.