Kwanini Wazanzibar wanafanana majina????????

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2009
Posts
6,157
Reaction score
4,457
Wadau nimelazimika kuuliza hili swala kwasababu ni zaidi ya mara tatu nakutana na Wazanzibar wasiofahamiana ila wanafanana majina tena majina matatu, nina rafiki yangu wa Mtandaoni yeye yupo Zanzibar tulikutana mitandaoni enzi hizo za Secondary School tukiwa tunasaka marafiki kwenye Mitandao, huwa ananisaidia sana kunipa Kampani, ninapokwenda Kikazi Zanzibar namimi huwa nafanya hivyo hivyo anapokuja Dar.

Nitatumia majina yasiyo harisi kuepuka usumbufu, Huyu rafiki yangu anaitwa Arafa Suleiman Husein, siku moja nikiwa nafanya kiproject flani kilichoni nilazimu kutafuta vibarua watatu kwa ajiri ya kukusanya taarifa, nikajikuta nina kibarua mmoja anaitwa Arafa Suleiman Husein na hata nilipowakutanisha na rafiki yangu ni kwamba hakuna anayemfaham mwenzake, nikiwa huko huko Zanzibar nikakutana na Jamaa aitwaye Hamad Hassan Makame, hili jina lilinikumbusha jamaa mmoja Mzanzibar nimesoma naye Kozi moja mwaka 2007 aitwaye Hamad Hassan Makame, nilipouliza kama anamfaham nayeye akawa anashangaa tu.

Kitu kilichonifanya niandike hii thread, ni kwamba pale Tanga nimekutana na mtu mwingine ambaye anakuwa ni watatu sasa kufanana jina na rafiki yangu yaani anaitwa Arafa Suleiman Husein, na hata hafahamiani na rafiki yangu Arafa Suleiman Husein aishiye Zanzibar,naye huyu pia ni Mzanzibar lakini maisha yake kwasasa anayaendeshea Tanga.

Sasa wadau naombeni kujua ni kwanini hawa ndugu zetu wanafanana sana majina? Nauliza hivyo kwasababu kwa huku Bara ni vigumu sana kuwakuta watu wanafanana majina tena majina yote matatu.
 
Hii inatokana na udogo wa watu Wa znz na wanapeda kutumia majina ya mababu au mabibizao nilikutana na jamaa mmoja anaitwa haji Wa haji
 
Tatizo lingine la Wazanzibari ni kubadili majina bila kujua...mtu ataandika jina lake leo hii Mohamed; Kesho Mohamedi...au Fatma kesho Fatuma....inawasumbua sana likija swala la kukagua documents za mtu
 
Huko kutokujuana kwa watu wenye jina moja inawezekana sana.
...
Majina mengi ya kufanana mpaka mababu, mara nyingi wazee hufanya hivyo kwa kukusudia kabisa! na wakati mwengine hupanga hayo majina kwa kukusudia ndoa!!!!
 
Tatizo lingine la Wazanzibari ni kubadili majina bila kujua...mtu ataandika jina lake leo hii Mohamed; Kesho Mohamedi...au Fatma kesho Fatuma....inawasumbua sana likija swala la kukagua documents za mtu

Mmmh jamani nyiee...
 
Ndio zenu hizo hamuchelewi kusema tuache tupumueee
 
Kwa uhalali wa kizazi :- Sir/family name.......,
Fathers name..............,
Given name.............................,
 
Duh umenikumbusha kitu sijui Zanzibar kuna Makame wangapi kila mtaa lazima ukutane na Makame.
 
Wanyumbaniee Mvaa tai; Sasa nikujuze idadi yote ya kiswaniZNZ/PMB ni kama laki 8 hadi 9..!! Hayo majina siyo ya Ajabu!!
Wewe staajabia majina ya kichina !! idadi ya CHINA ni 1.5bilioni !! na wote ni rangi moja/lugha moja/kimo na hulka !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…