Kwanini watu wanapenda kuvaa milegezo?

Kwanini watu wanapenda kuvaa milegezo?

Acha kutetea vitu visivyofaa, inawezekana nawe ukawa miongoni ya hao wavaaji wa hiyo milegezo.

Hivi hao vijana kutuonyesha maboxer yao, wengine hawajayafua hadi wiki moja, kwako unaona imekaa sawa tu?!
Khaa!! Kila mtu kwa wakati hupitia haya mambo inategemea tu wakati. Sidhani kama boxer kuonekana ni uchi. Kama makalio yangeonekana hiyo ingekuwa habari nyingine. Hawajavunja sheria yeyote ya nchi. Tuwaache wafurahie uhuru wao. Siku wakipoteza nusu ya uhuru wao (kazi/ ndoa) wataacha tu.
" Kila kizazi na kitabu chake" - Mzee Ruksa
 
CHAULA RICH

Umeuliza swali zuri. Tatizo ni kwamba vijana wa siku hizi wanadhani kila kitu kinachofanywa na vijana wenzao nje ya nchi - majuu - kinafaa kuigwa. Huo ni ulimbukeni.

Asili ya uvaaji "mlegezo" ni kwenye jela za nchi za nje, ambapo uvaaji huu ulianzia nchini Uingereza.

Kwa vijana wanaoingia magerezani, walijifunza kwamba ukiwa pale - mfungwa - unapaswa kuwa na "bwana" wa kukulinda ili usiwe unapigwa na kuumizwa na wafungwa wenzako. Kwa hiyo ili upate "ulinzi" huo unapaswa kukubali kujihusisha na matendo ya usodoma. "Bwana" wako anakuwa ni mtu mzima, jabali, mwenye wafuasi wengi, ambao baada ya wewe kuwa "kundini" hakuna atakayekugusa mpaka akuchoke au ugombane naye na aamue kwamba huna faida naye tena.

"Ukishatemwa" kwenye kundi la "Bwana" hiyo inakubidi uvae "mlegezo" ili "bwana" mwingine ajue kwamba sasa "uko huru" na yeye anaweza "kukuchukua".

Mtindo huu ulienea kwa kasi sana kwenye magereza ya Uingereza hadi Marekani, na unaonekana kuwa jambo la kawaida.

Hivyo basi, uvaaji huu unahusika kabisa na vitendo vya kishoga, na mashoga wengi wa kiume ambao hawako jela huvaa suruali zao kwa namna hiyo ili kujitambulisha kwa mashoga wengine, haswa kwa vijana.

Swali ni, je, hawa WAJINGA wanaovaa mlegezo wanajua maana yake?

Jaribuni kuwaambia kwamba uvaaji huo ni wa kishoga, muone kitakachotokea.

Nimemaliza.


Asante kwa ufafanuzi mzuri sana Mwanahaki,samahan kwa kuchelewa kukujibu kwasababu nilikuwa mbali na mtandao kidogo kwa siku kadhaa.nitawaelimisha,japo wengi wao ni wagumu kuelewa na huwa wanadhani kuwa ni ujanja kumbe ni ulimbukeni usio na maana na ni ujinga.
 
Kuvaa milegezo ni kutangaza biashara ya 0713. Juzi kati nimekutana na askari FFU kalegeza suluali huku anadunda na buti zake!
 
Ni maumuzi ya mtu mwenyewe kutokana na muinekano wake katika vazi flani
 
Back
Top Bottom