Miongoni ya fasheni za hovyo kabisa kuvaliwa na vijana wa kizazi hiki, basi ni hii staili ya vijana wa sasa wanayoiita mlegezo aka kata K.
Huwa najaribu kuimagine hivi inawezekanaje kijana wa kiume avae huo mlegezo, halafu anapita mbele ya mama yake mzazi au mama mkwe wake bila wasiwasi wowote!
Huo ni mmomonyoko wa maadili uliopitiliza.
Vijana wetu waTz watambue kuwa siyo kila kitu kinachofanyika Marekani ni cha kuiga.
Nadhani umefika wakati, kama ambavyo imewahi kufanyika wakati fulani kwa wananchi kuwazomea waxiwazi wadada waliokuwa wanakatiza mitaani na vimini vya kutisha, hadi sasa wadada wengi wameacha kabisa kuvaa vimini vifupi sana, nadhani imefika wakati kwa watanzania wote tunaopenda Taifa letu liwe na maadili mema, tuanze sasa kuwazomea waziwazi vijana wote kila watakapokuwa wanapita, wakiwa wamevaa hayo mavazi yso ya kishenzi ya mlegezo.
Naamini ni kwa njia hiyo peke yake, tutaweza kulirejesha Taifa letu kwenye mstari, badala ya kuliacha liendelee kuangamia na mmonyoko huo wa maadili uliopitiliza.