Kwanini watu wananiogopa sana?

Kwanini watu wananiogopa sana?

Ushauri wangu jipeleleze kama sio ww basi mtafute mtu wako wa karibu ambae angalau mnafahamiana kwa muda mrefu.Kama mkiwa background ya kusoma nae pamoja inaweza ikawa nzuri zaid.Ongea nae na mwambie akusaidie kwa kuwa muwazi na mkwel juu yako na vile ulivyo kwa kadir anavyokufaham (Kama utampata mtu wa karibu itakusaidia kukufanya usihis anaku judge pindi anapokuambia ukwel).
Trust me ,unaweza ukajiona mzuri au handsome kama unavyoambiwa lakin your impression usoni mwako ina matter sana.Namna unavyojiweka ukiwa unaongea au unamsikiliza mtu pia TONE ya sauti yako iko vp bila kujali.Tone yko inaweza ikaleta message tofauti kabisa bila kujal unaongea kwa upole auu unaongea kitu Positive, kama tone ya saut yako hujaweza kuijua na kui master always watu wataku misunderstand tu.
Binafsi nina issue kama yako but aleast kuna mtu alikua na guts za kunambia ukwel, a close frnd.Shida yangu hasa ilikua Tone ya sauti.Kwamba imekaa kiu shari shari sana.Kila nachoongea naonekana kama na judge /nabishana/ nagombeza.
Naweza kuongea kitu kama ushaur lakin knaapokelewa kama Command au instructions.
Shida ya pil ni kuwa huwa ni mtu wa kutafakar sana kitu hata kama ni kidogo hivyo mtu akinambia kitu ikawa inaleta picha kana kwamba nachambua sana mawazo yao au sikubalian nao mara moja kumbe ninakua na mambo yangu tu.Sikua mtu mwenye haiba ya kucheka cheka sana kwahiyo ikawa inawaletea tafsir watu kuwa nina dharau + am judgmental + a commanding person.
Trust me kwa type hii ya personality watu hawawez kuwa interested na ww automatically.Ikawa inawafanya watu wa interect na mm only where necessary.
Na kitu hiki nikaanza kukiona hata kwa mwanangu wa kwanza.
Thanks God nilijulishwa ukwel na nikaufanyia kazi and am enjoying the power of interaction with people.
HUJACHELEWA
Aisee.... Asante boss!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuogopwa ni suala la kiroho, UNA ROHO YA KUTIA HOFU, hata zamani kabla ya ustaarabu wa kikoloni , wale machifu walikuwa na roho hizo.. mtu akikaa na wenzake inatokeaa tu anachoongea watu wanshindwa kubishia. viongozi wa wakati huo walipatikana kutokana na nguvu za kiroho , mtu anaogopwa tu. mi niliwahi kuambiwa hata machifu kuwa na wake wengi ilitokanan na wanawake kuwaogopa hao watu kiasi kwamba inakuwa ngumu kumkatalia.
uhh??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi huwa siamini kama kuna mtu anakosa rafiki wa kuendana nae, haijalishi ni mtaa mmoja au mwingine...
Halafu usijitahidi kujibadili maana hakuna namna utakuwa ambayo watu hawatokuangalia negatively ...

Kama hayo maisha hayakudhuru bhasi haina shida; japo kuzoeana na jirani mmoja au wawili ni muhimu kwa maana jirani wa karibu ni bora kuliko ndugu aliye mbali hasa ukipatwa na chochote kibaya kama ugonjwa wa ghafla..

Sent using Jamii Forums mobile app
Binafsi sina tatizo, lakini tatizo linakuja pale watu wanapoonyesha kunyong'onyea hususani nikiwa naongea nao!! Wanapapatika sana kiasi kwamba najiuliza shida nini! Sauti yangu naiweka chini na nakwepa kutizamana nao machoni lakini bado wanatetemeka!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi pia niko hivyo ,ila sioni shida sana,ni mkimya na nahisi watu wengi wanakosa kujiamini wanapokutana na watu wasioongea sana ndio maana wanakuwa kama wanakuogopa,ni mara chache kunikuta naongea sana,utani wangu pia una mipaka,sijilaumu kuwa hivi ila nimegundua pia kuna watu wanatamani kuwa kama mimi lakini kwakuwa ni swala la maumbile naona inakuwa vigumu kwao.Ninapokuwa na mke wangu au familia ni tofauti sana,ninaongea ninacheka na hata kutaniana ila nikiingia kazini au kwenye mchanganyiko wa watu hali inakuwa tofauti,sijui labda niko serious sana lakini naona ni kawaida..
 
Hata Magu kwa sura wala siyo ya kutisha mkuu..Ila anaogopesha sana watu..Matendo/nyendo/tabia yako mkuu ndiyo inatisha..

#Muungwana_John
Mimi ni mkimya na napenda kujifungia ndani muda mwingi! Kinachowaogopesha nini hasa maana hata mtu ninayekutana nae mara ya kwanza ananitetemekea!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani ukimwona mkuu was mkoa wa tabora kwa haraka haraka unaweza kusema huyu MTU katiri sana kutokana na sura ilivyo lakini mzee huyu nampenda sana ni mcheshi mzungumzaji mzuri ...kuogopwa sio sura

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je. Hii ni kwa wanao kufahamu tu ama hata ukikutana na mtu kwa Mara ya kwanza?

Je.unafanya mazoezi na mwili wako umetuna?

Unafanya kazi ya aina gani? Ulinzi ama za computers kwa maana ya kutumia?
Mwili wangu ni mwepesi tu (athletic) na hata urefu wangu ni wa kawaida kabisa saizi ya kati! Umbo langu halitishi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaweza ukawa upo poa lakini si mtu wa stori na watu. Ukiishi mazingira ya namna hiyo watu watakutafsiri upo serious sana. Matokeo yake asilimia kubwa ya watu watakuwa ni wenye kukuhofia/kukuogopa.

In short huchangamani na watu, ndipo tatizo lilipo.
uhh.. labda asee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasalaam...

Mimi ni Kijana wa early 30's, nina urefu saizi ya kati, rangi ya maji ya kunde. Kwa asili mimi ni mtu mkimya SANA.

Nimekuwa niki experience namna ambavyo watu wanajawa hofu wakiwa karibu yangu... aidha watanisalimia kwa woga na kutetemeka, au wataonyesha ishara ya kunyong'onyea.

Watoto wadogo na vijana ndio balaa kabisa, wakiniona wanatetemeka sana huku wananiamkia haraka haraka.

Hii hali inanitesa sana maana hata kazini watu wananiogopa na wakiniona wanajisikia inferior sana. Nikianza kuzungumza kila mtu anaitikia kwa hofu. Wakati mwingine najaribu kukaa mbali na watu ili wasijisikie duni!

Ni nini hiki? Sidhani kama sura yangu inatisha maana mke wangu na baadhi ya wanawake huniambia mimi ni handsome! Kwahiyo naamini sura yangu haitishi!

What is this?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nafanana na ww kwa hayo maelezo zaidi ya 80%. Mpaka wife anawezaje kuishi na mimi
 
Kama kwenye avatar, ww ni huyo wa katikati ,dah hata mimi napata hofu
 
Back
Top Bottom