Afrolink-Tz Consult Ltd
JF-Expert Member
- Feb 25, 2018
- 420
- 939
Habari zenu
Makala hii naileta ikiwa katika muundo wa swali ambalo kama jamii na wenye mamlaka pia wanapaswa kujiuliza na hatimaye kutafuta njia sahihi za kuifanya jamii ione na iamini ya kuwa kulipa kodi ya mapato ni wajibu wa kila anaestahili na si kwa watu wachache tu kama wafanyabiashara, wajasiriamali ,wafanyakazi na wadau wengineo.
Itambulike ya kwamba kodi ya Mapato ina umuhimu mkubwa sana kwa nchi yoyote duniani kwani ni chanzo kikuu cha mapato kwa serikali ambapo kupitia kodi hii basi maendeleo katika Nyanja mbali mbali kama vile za kielimu, kiafya, huduma na miundombinu hugharamiwa
Ama baada ya utangulizi huo, tukirejea katika Makala yetu ya leo fikirishi ya kwa nini hasaa jamii (si yote) hususani Tanzania haipendi kuwajibika katika ulipaji wa kodi. Hili husababishwa na mambo ambayo twaweza kugawanya katika maeneo makuu mawili
A. Jamii (wafanyabiashara, wajasiriamali, wafanyakazi, wakulima na wadau wengineo)
B. Mamlaka zinazohusika na ukusanyaji wa kodi
A: Jamii husika
Jamii kuu inayolipa kodi imegawanyika katika makundi ya wafanyabiashara, wajasiriamali, wafanyakazi, wakulima na wadau wengineo ambao uwajibikaji wao wa kulipa kodi ya mapato kwa hiyari ni mgumu japo sio wote. Changamoto hii huweza kutokana na:
1. Ukosefu wa elimu juu ya kodi ya mapato
Jamii yetu asilimia kubwa bado kuna changamoto kubwa sana juu ya elimu ya ulipaji wa kodi, kwa nini alipe kodi, namna gani ya ulipaji kodi, kipi kilipiwe kodi na kipi hakilipiwi kodi n.k. kutokuwa na elimu kunaifanya jamii hii kuona hakuna haja ya kulipa kodi. Jamii nyingi za watu waishio maeneo ya vijijini mathalani japo na mijini kuna changamoto hii hawana elimu ya msingi juu ya kodi hivyo kuleta uzito wa kuwajibika katika kulipa kodi.
2. Tabia za jamii (kasumba)
Jamii kuamini kuwa kama utakuwa muwazi katika mapato yako basi ukienda Mamlaka ya Mapato hutokubaliwa unachotaka kulipa bali utalipishwa kodi kwa matakwa ya mtu atakaekusikiliza. Kutokana na khofu hii hata kama jamii husika ikienda basi itatoa maelezo yasiyo sahihi ili tu kujihami dhidi ya kulazimishwa juu ya kiasi gani cha kulipa
3. Mfumo wa ulipaji kodi kuonekana kama una kificho kwa jamii
Hii pia ni kasumba iliyojengeka kwa jamii kuwa kuna mtego katika namna ya ukokotoaji wa kodi kwa kuwa jamii inaamini haupo wazi kwao. Kwa mfano labda kwa nini alipe kiasi fulani cha kodi ilhali biashara aliyofanya haikuzalisha kiasi hicho. Jamii inakuwa inaamini kuwa ukokotoaji wa kodi huwa ‘based on assumptions rather than the facts’ hivyo kusababisha kulipa kodi kubwa na kandamizi
4. Jamii kuwa na mtazamo hasi juu ya matokeo baada ya malipo ya kodi
Hili linatokana na jamii kuona matokeo baada ya kulipa kodi hayana uwiano na kinacholipwa. Maana yake ni kwamba jamii inaamini kulipa kodi basi ipate huduma bora kama za afya, elimu na maji. Sasa nongwa huja iwapo mwanajamii akienda hospitali akikosa tu dawa basi kuamini kodi inawanufaisha wachache
5. Watu wachache kuwajibika kulipa kodi
Hii inatokana na kuamni kuwa wanajamii wachache sana wanalipakodi hivyo kujikuta wanakuwa na kodi za viwango vikubwa ilhali kundi kubwa la jamii halilipi kodi moja kwa moja kama kundi dogo. Kutokana na hili linasababisha jamii kuchukia kulipa kodi ya mapato
Hizi ni baadhi tu ya sababu za jamii.
B: Mamlaka zinazohusika na ukusanyaji wa kodi
Mamlaka kwa ujumla zina sheria, kanuni na taratibu nzuri sana za ulipaji wa kodi kwa kila mwanajamii alie na sifa. Ila kunaweza kukawa na sababu hizi ndani yake ambazo zikasababisha utekelezaji kuwa na mapungufu
1. Watendaji
Hii inakuja pale mtendaji kufanya maamuzi kwa mujibu wa matakwa yake na si kwa mujibu wa sheria zinavyoelekezwa. Hili hupelekea kutoa upendeleo au kumkandamiza mlipaji kodi. Pia mtendaji kutumia ‘advantage’ ya mwanajamii kutokuwa na elimu ya kodi basi anamkandamiza ikiwa kwa nia ya kunufaika na tatizo la mlengwa au kumkandamiza
SULUHISHO
Kutokana na changamoto na kelele zinazozidi kila leo juu ya masuala ya kodi ya mapato, kuna haja serikali kuchukua hatua stahiki zifuatazo:

- Somo la kodi (basic) liwekwe kwenye mitaala ya elimu kuanzia ngazi za chini ikibidi shule za msingi ili kila mtoto anakuwa akiamini kulipakodi ni wajibu
- Mamlaka zinazohusika zijitahidi kuongeza idadi ya walipa kodi wa moja kwa moja (tax base) kwn hii itasaidia hata kupunguza kiwango cha kodi kuwa Rafiki zaidi
- Uadilifu kwa watendaji wa Mamlaka husika za ukusanyaji mapato. Watendaji kuamini ni wajibu wao kutoa elimu kwa mlipa kodi kwani bila kufanya hivyo kila leo kos litakuwa lenye kujirudia kwa mlipa kodi