Hapa utakuwa unaongelea watoto wa kishua na wenye pesa ambao ni wachache Tanzania kiuhalisia.
Nimeona hapo sijui gari, club na uhuru haya mambo ni mageni kwangu na kwa wengi waliokulia mazingira na uchumi wa kipato cha kati.
Watoto waliolelewa kwenye mazingira ya uchumi wa kawaida au wa kati kamwe hawawezi kuwa na uwezo au fikra za kuua mzazi.
Sababu tangu mtoto anakuwa anamuona mama ndio msaidizi na mtetezi wa kila kitu kwenye shida na nafuu na kama baba ni mjinga ndio kabisa.
Mama anakuwa rafiki na mshauri pia kunakuwa na mipaka vilevile, kutokana na ukaribu na mwanae mtoto anakuwa motivated kupambana kwa ajili ya mama no matter what na heshima kwa mama isiyoteteleka wala kuvunjika.
Hakuna kitu ninachokiheshimu duniani kama mzazi wa kike.
Hayo yote ni sababu ya malezi tu.
Lakini hawa jamaa wa kishua na pesa wazazi wao wanaishi kama wazungu.
Hakuna mipaka kati ya mzazi na mtoto, hii inapelekea kukosekana heshima.
Hakuna ukaribu kati ya mzazi na mtoto, hii inapelekea mtoto kutokujali kuhusu mzazi.
Na kutokana na malezi yao na tabia za wazazi, watoto wanakuwa hawajui wala hawaoni umuhimu wa mama kwenye maisha yao.
Anamuona kama mshikaji wake tu, matokeo ndio hayo.
Na hata hivyo hakuna sababu yoyote ya kuhalalisha mauaji ya mzazi hata kama makosa ni ya wote au upanda mmoja, lakini hii iwe fundisho kwa wazazi juu ya malezi ya watoto.
Mimi nipo tayari kufa kwa ajili ya mzazi, wengine wanawapiga mapanga.
Yote ni malezi tu.