Hoja kwa hoja; Ni kwanini wazazi kwasasa wamepoteza mvuto kwa watoto wao (BIRTH)

Palac

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2025
Posts
2,391
Reaction score
6,266
Hivi sasa kwa zama hizi wengi ni wazazi pengine kwa kutarajia kua na wengine hawakutarajia imetokea tu.

Kwasasa wazazi wanalalamika watoto wao kutowahudumia zaidi wanapofikia uzee lakini watoto hawa hawa unakuta mjini ana maisha ya kuweza kumtumza mzazi au wazazi wote wawili lakini kwa GenZ imekua tofauti sana kwa wazazi wao na hata wasio kua wazazi

Je ni nini hasa imepelekea ili swala limekua kubwa na linazidi kukua nafikiri ukizunguka mjini unakutana na wazee tofauti hali zao zinakua tofauti ila anakueleza ana mtoto pengine yupo vizuri ila hamhudumiii na wala swala la kuja kumsalimu imekua hadithi

Karibuni tujadili je ni wazazi ndio wamepoteza mvuto kwa watoto wao au nini hasa
 
Mahusiano kati ya watoto na wazazi hajyakujengwa vizuri hapo awali, pia majukumu yakizidi sana wkaati kufikia malengo ni jasho, mtu ana lose interest kwa kila kitu!
Kipindi nakua mzazi alikua anaheshimika sana kila jambo la mtoto lazima anahusika kwa 90% ata kama mtoto ashakua mtu mzima lakini kwasasa ni tofauti kabisa
 
Mahusiano kati ya watoto na wazazi hajyakujengwa vizuri hapo awali, pia majukumu yakizidi sana wkaati kufikia malengo ni jasho, mtu ana lose interest kwa kila kitu!
Upo sahihi! Wakati mwingine sisi wazazi tunasahau majukumu yetu hususan kwa wale tuliozalisha michepuko yetu. Michepuko ni pasua kichwa maana anakutandika kupitia kwa mtoto. Usipokuwa ngangari, utamsahau hata mwanao. Mtoto hayo hayajui, atabugia sumu toka kwa mama.

Mbinu tulizokuwa tunatumia, unahakikisha wakati wa kulipa shule, unakuwa na mtoto beneti nakumweleza hii hela nakulipia shule. Wakati mwingine hasa akiwa day, unaenda na pipi unampa na kumweleza kuwa baba yako mimi nakupenda. Unambeba mgongoni hata kama ni miaka 15. Ila unakuwa mwangalifu hata siku moja usimseme vibaya mama yake. Kila siku unamsifia, baadaye atagundua sumu. Mwenyewe atakuja kukueleza tu. Pili angali interest za mtoto etc. Ni ujanja tu
 
Hivi sasa kwa zama hizi wengi ni wazazi pengine kwa kutarajia kua na wengine hawakutarajia imetokea tu.

Kwasasa wazazi wanalalamika watoto wao kutowahudumia zaidi wanapofikia uzee lakini watoto hawa hawa unakuta mjini ana maisha ya kuweza kumtumza mzazi au wazazi wote wawili lakini kwa GenZ imekua tofauti sana kwa wazazi wao na hata wasio kua wazazi

Je ni nini hasa imepelekea ili swala limekua kubwa na linazidi kukua nafikiri ukizunguka mjini unakutana na wazee tofauti hali zao zinakua tofauti ila anakueleza ana mtoto pengine yupo vizuri ila hamhudumiii na wala swala la kuja kumsalimu imekua hadithi

Karibuni tujadili je ni wazazi ndio wamepoteza mvuto kwa watoto wao au nini hasa
waheshimu baba na mama yako ili upate miaka mingi na kheri duniani,
watoto wengi hawadumu maishani kwasababu hiyo, watoto wengi hawana heri za wazazi bali manung'uniko ya wazazi dhidi yao kwa kuwatelekeza.

ni muhimu sana kila moja kulitazama hili,
vinginevyo, ndio yale mazungumzo ya waombolezaji kwamba kaondoka akiwa bado mdogo sana

tuwaheshimu wazazi wetu :1Head:
 
Upo sahihi! Wakati mwingine sisi wazazi tunasahau majukumu yetu hususan kwa wale tuliozalisha michepuko yetu. Michepuko ni pasua kichwa maana anakutandika kupitia kwa mtoto. Usipokuwa ngangari, utamsahau hata mwanao. Mtoto hayo hayajui, atabugia sumu toka kwa mama.

Mbinu tulizokuwa tunatumia, unahakikisha wakati wa kulipa shule, unakuwa na mtoto beneti nakumweleza hii hela nakulipia shule. Wakati mwingine hasa akiwa day, unaenda na pipi unampa na kumweleza kuwa baba yako mimi nakupenda. Unambeba mgongoni hata kama ni miaka 15. Ila unakuwa mwangalifu hata siku moja usimseme vibaya mama yake. Kila siku unamsifia, baadaye atagundua sumu. Mwenyewe atakuja kukueleza tu. Pili angali interest za mtoto etc. Ni ujanja tu
Dahh sema mnakosea basi tu, hiki ndio chanzo cha familia nyingi kuvunjika, unashangaa unaishia kupendwa na mtoto wa mchepuko kwa kutia bidii zako halafu ndani unaangusha kila kitu! Ndio matokeo ya hilo kundi hapo juu la kuchukia au kuwapotezea kabisa wazazi!
 
Ni issue ya malezi,
Unakuta mzazi hakujenge emotion connection na mtoto wake,wanakua hawana bond kati yao,

Wazazi wengi hawajui kua kuhudumia na kulea ni vitu viwili tofauti kabisa,

Mfano mtoto mdogo anapelekwa boarding school,au mzazi hajipi muda wa kukaa home na familia yake ili kutengeneza bond na watoto wake,

Ni kweli maisha yanakimbiza ila jitahidi uwe unapata muda wa kukaa na wanao,au kua una cheza nao baadhi ya michezo,hivyo ndivyo vitu hukumbukwa zaidi na watoto kwenye makuzi yao,

Mtoto humkumbuka mtu aliyekua karibu nae zaidi kwenye makuzi yake.
 
Mtoto wa kwako uliyezaa na mchepuko. Ukishakuwa mzazi wa multiparty, wewe unafungamana na watoto. Wanawake achana nao. Hata ukifa hakuna mtu anataja wake ila anataja alifariki akiwa na watoto 15 wa kwanza ni... wapili na wa 15 ni... mchezo unaisha
 
Ni sahihi kwa mazingira ya sasa wazazi wamejikita kutafuta sana pesa ila uzao wao unalelewa na jamii tu
 
Haya mambo hesabu zake ni ngumu sana.
 
Mtoto wa kwako uliyezaa na mchepuko. Ukishakuwa mzazi wa multiparty, wewe unafungamana na watoto. Wanawake achana nao. Hata ukifa hakuna mtu anataja wake ila anataja alifariki akiwa na watoto 15 wa kwanza ni... wapili na wa 15 ni... mchezo unaisha
Hii tabia ipo kwa wasukuma, na baba yangu nahisi siku akifa tutakutana msururu wa watoto! We acha tu! Lakini tunampenda kweli mpole mno🥲
 
Hivi mtoto wa miaka 4-6 umuamshe saa kumi na moja alfajiri akalelewe na watu wengine huko kwa jina la elimu utegemee awe na upendo na wewe?

Upendo unajengwa kuanzia miaka 0-10 kabla mtoto hajabalehe. Akishaanza kubalehe anakuwa anahitaji marafiki kuliko wazazi
 
Ni sahihi kwa mazingira ya sasa wazazi wamejikita kutafuta sana pesa ila uzao wao unalelewa na jamii tu
Huo ni ujinga! Huwezi kukosa muda wa kuwa na watoto ulojizalia. Tatizo kubwa ni moja, mwanamke akikuchefua kawaida wanaume tunachafukwa na uzao wake wote. Hilo ni kosa la kipuuzi. Kila wakati mwanaume unabanana na watoto wako
 
Hela ni muhimu kwenye maisha hilo wala halipingiki ila kwenye haya maisha usipokua makini,unaweza kujikuta muda wako wote wa uhai wako uliutumia kukimbizana na hela tu na ukasahau kuishi.
Lakini bado kumekua na wimbi kama ukiwa na watoto wa nje ya ndoa siku ukitengana na mzazi mwenzako basi nao watoto hukutenga ili unalitazama vp
 
Back
Top Bottom