Kwanini Watanzania wengi hawafanikiwi kutokana na kazi zao?

Kwenye madini wengi wanaofanikiwa sio wachimbaji, ni wenye migodi na wanahisa. Vibarua wachimbaji wachache hubahatika mafanikio ila mafanikio yao huambatana na kelele nyingi sana.

Ngumi na soka ni michezo ambayo wenye vipaji wakaongeza bidii na usimamizi mzuri ndio hufanikiwa zaidi, wapo wengi katika hiyo michezo wana bidii kubwa ila kutokana na kukosa vipaji au fursa wanaishia kuwa wa kawaida tu na wengi pia hawafiki popote.
Freemason je?
 
Dr. John C. Maxwell ni Mwalimu mashuhuri wa uongozi duniani. Kabla ya kufika barani Afrika, aliamini yafuatayo kuhusu mafanikio, kwamba:

1. Mafanikio yanatokana na kufanya kazi kwa bidii.

2. Wamarekani wanaongoza kwa kufanya kazi kwa bidii.

Lakini baada ya kufika Afrika, alibadilisha mtazamo. Kwa mara ya kwanza maishani mwake alishuhudia watu wanaofanya kazi sana lakini bado hawana maendeleo.

Sijui "case study" yake ilikuwa nchi gani Afrika, lakini maadam ni Afrika, na Tanzania inahusika, na ni kweli kuwa kuna Watanzania wengi wanaofanya kazi kwa bidii lakini wangali wana hali ngumu kiuchumi.

Kwanini iko hivyo?
Kwani huyo dokta wako wa mchongo hajui kwamba Africa inakabiliwa na bottlenecks nyingi kiasi kwamba Tija ya kujituma haipo?
 
Ukiwa Marekani nadharia ya kufanya kazi kwa bidii na kufanikiwa ni sahihi sana kwa sababu kuna ukweli mkubwa kwamba US ni "land of equal opportunity" na watu wengi waliofanya kazi kwa bidii wamefikia American Dream katika siasa, sanaa, michezo, teknolojia n.k

Sehemu kubwa ya Africa hata ukiwa actor au mwanamziki mzuri sana hakuna wa kununua kazi zako,

Ukizaliwa na wazazi Immigrants kama Obama, hata uwe mzuri vipi Urais sahau.

Kuanzisha biashara vikwazo kibao, watawala mangimeza wanavuruga biashara na kazi za watu kwa sababu ya siasa tu.

Taaluma muhimu kama madaktari hazithaminiwi,

Haya ni baadhi ya mambo tu ambayo yanafanya hata walio na juhudi kubwa sana kubaki na maisha ya kubangaiza.
Viongozi wetu na matajiri wetu wa Afrika hawapati mafanikio kwa bidii ya kazi bali kwa mkato wa kuvunja sheria na Katiba ikiwemo ukwepaji kodi za serikali, sasa sisi raia tutafuata barabara ndeeefu ya mafanikio tuweze kweli?.
 
Mazingira yetu ni magumu mno tunaishi kislavery kwenye mfumo wa capitalism.

Mfano. Miaka 8 nyuma nimemaliza chuo nikapata kazi kwa muasia mmoja hapo posta kampuni kubwa tu mshahara laki 3.. na wote tulioajiriwa tulikuwa ni degree basi income kwa mwezi ile ofisi tunaiingizia almost bill 1.1 kila mwezi. Ila mshahara ndo huo na hapo unachungwa hatari usiibe tukajiorganize tukapeleka proposal kwa manager huyo muasia aongeze mshahara basi maana yy anajilipa million 30 kwa mwezi anaservice ya gari million 4 anakaa appartment ya million 2.5 kwa mwezi..

Basi huwezi hamini akatuita wote akasema hawezi kuongeza chochote maana huo mshahara tunaolipwa hapa africa ni mkubwa na tunaweza kusurvive vizuri alafu akaongeza kama mnaona vipi acheni kazi huku kwenu africa labour force ni cheap sana na watu kibao hawana kazi..na maneno ya shombo mengiii tukapewa..

Mm kwa majibu yale nikaacha kazi siku iliyofuata niliona nimedhalilika sana nchini kwangu tunadharauliwa vile..nimekaa miezi 5 nikasikia alifukuza wenzangu wote waliobaki akaajiri wapya.
Africa ni shida basi tu..
Ukifungua biashara utaelewa
 
Huyo Mr John Maxwell kuna kitabu chake kazungumzia haya mambo Kwa style hii

Maisha popote duniani unapozaliwa unabidi kufahamu kuwa maisha ni magumu Ila yataendelea Kuwait Magumu ikiwa utashindwa kuwa na ivi vitu

Effective thinking
Goals and being smarter


kama wewe unaelewa kuhusu Africa watu tunafanya Sana kazi Ila hatuna malengo wapi tunahitaji kufika na wapi tulipo tunapata pesa lakini pesa nyingi tunawekeza katika pombe na wanawake.


Mfano Mimi nalipwa 300k

Nikitoa 100k inatosha kununua Michele kg 20 na unga kg 10 na gas

Hivyo ikiwa sitaonga wala kunywa pombe basi ntakuwa na uwezo wa Ku save laki moja kila mwezi.

Sisi tunakwama katika Effective thinking na Goals and being smarter
Usipoonga utapata wap demu kutoa hamu zako alafu maisha sio strictly hivyo
 
Ukiwa Marekani nadharia ya kufanya kazi kwa bidii na kufanikiwa ni sahihi sana kwa sababu kuna ukweli mkubwa kwamba US ni "land of equal opportunity" na watu wengi waliofanya kazi kwa bidii wamefikia American Dream katika siasa, sanaa, michezo, teknolojia n.k

Sehemu kubwa ya Africa hata ukiwa actor au mwanamziki mzuri sana hakuna wa kununua kazi zako,

Ukizaliwa na wazazi Immigrants kama Obama, hata uwe mzuri vipi Urais sahau.

Kuanzisha biashara vikwazo kibao, watawala mangimeza wanavuruga biashara na kazi za watu kwa sababu ya siasa tu.

Taaluma muhimu kama madaktari hazithaminiwi,

Haya ni baadhi ya mambo tu ambayo yanafanya hata walio na juhudi kubwa sana kubaki na maisha ya kubangaiza.
Hata Samata angebakisha kipaji chake humu humu Afrika asingetoboa. Akina Sande Manara wangevuka bahari leo wangeacha ukwasi mkubwa wa kutisha.

Wafuatao wangecheza soka la kulipwa Afrika wasingekuwa matajiri:-
1. Diego Maradona.
2. Leonel Messi.
3. Ronaldo de Lema.
4. Ronaldinho Gaucho.
5. Christiano Ronaldo.
6. Neymar.
7. Hazard.
8. Paulo Dybala.
9. Lewandowski.
10. Sergio Aguero.
Nk nk.
 
Hilo neno "kutumiskisha" kama lina kaukakasi mkuu. Mimi nafikiri kazi nzuri ni ya "win win" baina ya mwajiri na mwajiriwa.

Kama inayokusaidia ni ya kwako hata kama inamilikiwa na mtu mwingine.

Mfanyakazi na mwjiri wake ni "partners" wa maendeleo ya kila mmoja.
Kama unataka mafanikio makubwa sahau kuajiriwa. Hakuna namna unaweza kutoboa maisha na kuishi utakavyo kwa kuajiriwa. Popote utakapokuwa umeajiriwa utalipwa asilimia 10 au hata chini ya asilimia 10 ya kile unachokiingiza kwenye kampuni
 
Sijafanya research ya kuweza kuhalalisha majibu yangu.

Ila nitatoa mfano.

Kesho unatakiwa kuukata mti.

Unajihimu Alfajiri na vitendea kazi, unafika pale na kuanza kukata mti. Unajitoa kweli kweli, unatumia msumeno, unatumia shoka na unatumia panga.

Lakini muda wote huo ulikua hauahangaiki kukata shina, ulikua unakata mizizi na matawi.

Kufika jioni mti haujakatika.

Kesho unarudi tena, na kwenda na routine ile ile.

Kwa maoni yangu WaTz wengi wanaoonekana wanafanya kazi angalia kama kazi yao inashughulikia tatizo. Utakuta ni inalizunguka tatizo.

Angalia wanasiasa, timu za mpira, hata maofisini n.k. ni wachache wanaaddress tatizo.

Ninaamini ndiyo sababu tunaonekana tunafanya kazi ila mafanikio hayaji au yanakuja kiduchu
Most people are busy with the wrong things

Tupo bize lakini bize kwenye mambo ambayo siyo sahihi
 
Back
Top Bottom