Kwanini Watanzania tuko tofauti na Waafrika wengine?

Kwanini Watanzania tuko tofauti na Waafrika wengine?

Ebu subiria comment za wengine
Panya je? Mikoa ya Rukwa ..Katavi ..Lindi na Mtwara ..panya ni kitoweo hadi funza wa kwenye magome ya miti aina ya miyombo ..Rukwa huwa ni kitoweo pia ..nyani mkoa wa Rukwa analiwa na kabila LA wanyika a.k.a kabila analotokea mbunge mstaafu ndg Mzindakaya ...tembea uone mkuu usifikiri kila unayoyaona mjini na vijijini ni hayo hayo..[/QUOTE]
Hao wa Mtwara wamefundishwa na wamakonde wa Msumbiji na wengine ukichimba asili yao ni huko. Tabia za tofauti unaweza kuziona mikoa iliopo mipakani
 
Rudi ukafanye utafiti wako vizuri, kwani hata Watanzania wapo naoakula nyani, mbwa, panya nk.....

Alafu ukisikia nchi fulani wanakula mfano sokwe usifikiri kwamba ni watu wote wanakula sokwe na kwamba utakuta nyama ya sokwe butchani , bali ni jamii ndogo ndogo tu ambao ndio wanakula hizo unazoita vyakula vya ajabu, nikama wenzetu wale wanaokula mbwa hapa tz lakini sio kwamba eti watanzania wanakula mbwa,
Nadhani umeelewa


Acha uongo hakuna Mtanzania anayekula Mbwa leo hii, hizo ni hadithi tu za zamani nimefika Iringa nimetembea huko kote sijawahi kuona Bucha inayouza nyama ya Mbwa au mtu akila nyama Mbwa bali wanakula nyama za kistaarabu kama Ng'ombe, Mbuzi, kuku n.k lkn Mbwa hakuna kitu kama hicho, ila hawo Waafrika wengine wa Kongo au AM ni kweli wanakula Sokwe na Nyani na ndiyo hasa chanzo cha Ebola, huko ukienda Kongo au Kameruni ni kawaida kabisa kukuta bucha inauza nyama ya Sokwe au Nyani, hapa Tanzania ni wapi kuna bucha imeandikwa inauza Nyama ya Mbwa au Panya?

Hiyo ni Bucha huko AM, ni wapi hapa kwetuTanZania kuna bucha au soko la hivi? Nitajie!
0822bushmeat03.jpg


Hii ni bucha ya Nyama ya Sokwe/Nyani Mji Mkuu wa Ivory Coast Abijani, nionyeshe wapi Tanzania kuna Bucha ya kuuza nyama ya Nyani?

2014-03-27t150847z_1007970001_lynxmpea2q032_rtroptp_2_ozatp-us-health-ebola-bushmeat.jpg
 
Panya je? Mikoa ya Rukwa ..Katavi ..Lindi na Mtwara ..panya ni kitoweo hadi funza wa kwenye magome ya miti aina ya miyombo ..Rukwa huwa ni kitoweo pia ..nyani mkoa wa Rukwa analiwa na kabila LA wanyika a.k.a kabila analotokea mbunge mstaafu ndg Mzindakaya ...tembea uone mkuu usifikiri kila unayoyaona mjini na vijijini ni hayo hayo..
Hao wa Mtwara wamefundishwa na wamakonde wa Msumbiji na wengine ukichimba asili yao ni huko. Tabia za tofauti unaweza kuziona mikoa iliopo mipakani[/QUOTE]
Kwn singida nao wanapakana na nchi gani ? maana punda kwao ni kitoweo
 
Kuhusu kula mizizi mie sioni tatizo kwani mizizi mingine ni dawa, kama haidhuru basi kula ruksa na wale isiwe kioja, MBONA VIAZI NI MIZIZI NA NDIO INAPENDWA SANA KAMA FAST FOOD kwenye majiji hasa Dar
 
Hao wa Mtwara wamefundishwa na wamakonde wa Msumbiji na wengine ukichimba asili yao ni huko. Tabia za tofauti unaweza kuziona mikoa iliopo mipakani
Kwn singida nao wanapakana na nchi gani ? maana punda kwao ni kitoweo[/QUOTE]
Wale ni hodari wa kupaa na ungo hawana haja ya kupakana na nchi
 
watanzani waajabu sana, yan uoga na akili kuwa na mtindio wa ubongo imekuwa ni ustaarabu!!? we have a long way to go.
 
" sijawahi kutishiwa wala kukabwa, huko kwingene Uhalifu ndiyo nyumbani..."
mkuu unaishi wapi masaki? hata knyama wanakabana cku hizi, wanawasingizia wtt wa tandale.
 
ni kweli tuko tofauti lakini tembea uone hii Tanzania kubwa na kuna mambo mengi yanayoendelea huko vijijini na baadhi ya mikoa usiyoyajua
 
Watz sisi ni manyumbu...! Tunapelekwa-pelekwa tu

Ila, Iringa wanakula Mbwa

Mtwara - Panya

Lindi/Mtwara - Nyoka
 
Fitna,unafiki,kuoneana wivu, udini na ukabila. Kabla hujauzungumzia ustaarabu wetu na kuulinganisha na ustaarabu wa wenzetu hebu zungumzia kidogo haya nilio yataja hapo juu, maana haya tunafanyiana sisi kwa sisi, so napata mashaka juu ya huu ustaarabu unao hubiriwa kua tuko nao watanzania. Kwa upande wa vyakula hilo jiongelee ww au ongelea tamaduni ya kabila lako, lakini kwa wengine ni shida bro, Panya,konokono,Punda,kichuri nikatika vitu vinavyoliwa ndani ya nchi hii.
 
Walaji viboga (0713) tu sio vyakula vingine
 
Wanasema eti binadamu wa kwanza alitokea hapa bongo,ndo maana tuna tabia kama za mbinguni.
 
ni sisi Watanzani pekee ndiyo tunaokula vyakula vya maana yaani hatuli vyakula vya ajabu ajabu

Sijui una elimu ya kiwango gani na umesomea taaluma ipi. Lakini nimejiuliza, nikasikitishwa na kushangazwa sana na andiko lako kwa ujumla, lakini hasa statement hiyo kuwa sisi (watanzania) ndo tunakula vyakula vya maana kuliko waafrika wengine. Na kwamba sisi ndiyo tumestaarabika kuliko waafrika wengine. Kwanza suala la chakula gani mtu anakula linatokana na mambo mengi ikiwemo utamaduni wake, uwezo wa kifedha, masuala ya kiafya, umri, jinsi na mengine mengi mengine. Na huwezi sema kuwa wewe unakula vzr kuliko wengine bila kuwa na utafiti wa kisayansi kuthibitisha hilo kwa kuzingatia nutritional values za chakula unachokula n.k.

Wataalamu wa masuala ya chakula na lishe wanaweza kutusaidia lakini nadhani kuandika ulichokiandika hakuna tofauti na yule anayeona binadamu wengine ni nyani na yeye ndo binadamu, au mzungu anayeona kuwa utamaduni wake ndiyo unafaa na wa wengine (mf. waafrika) haufai.
 
Kuhusu kula mizizi mie sioni tatizo kwani mizizi mingine ni dawa, kama haidhuru basi kula ruksa na wale isiwe kioja, MBONA VIAZI NI MIZIZI NA NDIO INAPENDWA SANA KAMA FAST FOOD kwenye majiji hasa Dar


Sisi tunakula vyakula vya kistaarabu hiyo mizizi tunayokula ni ya kistaarabu kama vile Viazi, Mihogo n.k lkn hao wengine mizizi yao ni sumu na wengine hufa baada ya kula kwa maana wkt mwingine hawajui ipi ni sumu na ipi siyo sumu!
 
Hili nimeliona kwamba sisi tuko tofauti sana na Waafrika wa nchi nyingine kitabia, sisi tumestaarabika sana ikilinganishwa na Waafrika wa nchi nyingine na hapa naongelea Waafrika weusi tuishio Kusini mwa Sahara!

Na hili utaliona karibia kila mahali kwamba tunawazidi Waafrika wengine sana kuanzia kwenye ustaarabu, vyakula tunavyokula, ni sisi Watanzani pekee ndiyo tunaokula vyakula vya maana yaani hatuli vyakula vya ajabu ajabu kama Waafrika wengine kwa mfano Kongo wanakula Nyani na Sokwe kwetu hatuli, ukienda Afrika Magharibi kuanzia Kameruni mpaka Nigeria huko wanakula Kono kono, Mende, miti shamba na mizizi ya ajabu ajabu kwetu hatuli wanyama wa ajabu ajabu Tanzania tunakula nyama ya Ng'ombe, Mbuzi, Kuku, Kondoo baadhi Nguruwe, samaki lkn pia siyo wa aina zote kuna Samaki wengine Watanzania hatuli na tunachagua!

Ukija kwenye swala tu la maisha ya kila siku, Waafrika wengi hawawezi kusema tafadhali, asante, samahani, nakupenda, uniwie radhi, kwa heri ya kuonana, maneno ya kistaarabu kama haya hawana kwenye Misamiati yao kwa mfano ukienda Kenya ni kawaida mtu hata asiyekujua kukwambia ,,we kuja hapa", sasa Mtanzania hawezi kusema hivi bali tutasema kistaarabu na kiheshima samahani nakuomba uje, sasa ni kwa nini tuko tofauti na Waafrika wengine?

Utaona hata mambo ya uhalifu ingawaje ni kweli kwamba tuna uhalifu Tanzania lkn ukilinganisha na nchi nyingine za Kiafrika Tanzania yetu ni Paradiso, kuna nyumba nyingi sana Tz wala walinzi hazina na watu wanalala usingizi lkn nchi nyingine hili haliwekani, mimi huwa natembea mpaka saa kumi Alfajiri na poa kabisa sijawahi kutishiwa wala kukabwa, huko kwingene Uhalifu ndiyo nyumbani...

Yaani sisi tumestaarabika zaidi klk Waafrika wengine wote niwajuwao, na hili hata sehemu zilizoendela kama AK nimefika huko Waafrika wa huko hawana ustaarabu kama wetu, Je kuna sababu maalumu kwamba sisi tuko tofauti na wao?
au imeandikwa kwenye vitabu vya Dini labda tumetabiriwa ...

*Ustaraabu wetu haujaletwa na CCM wala Chama chochote cha Siasa, hivyo sisemi kwamba sisi ni Wastaarabu kwa sababu ya CCM na isitoshe Mada haihusu Siasa bali ni mambo ya Jamii!
mi nadhani wazee wetu wa zamani wamechangia sana..maana kuna makabila tunasikia wakali(wakurya,masai) ila jamaa ukikuta wanaishi na sisi wengine ni jamaa wastaarabu san
 
Ni kweli ila hii utakuwa umesimuliwa, wamakonde, wanaokula hii ni wale wenye asili ya msumbiji, ambao ambao unaweza wakidilia kama theludhi mbili ya wa wamakonde wote. Kama umefika Mtwara na vijiji vyake kule wengi ni Waislam, mkristo ni wakutafuta na tochi, angalau sehemu za mijini unawza wakuta wasio waislam. Wamakonde wa wenye asili ya msumbiji kama hawafiki theludhi mbili ya wamakonde wote, ukiwaingiza kwenye idadi ya watanzania wote ni kama hawapo kabisa, kwahiyo mwenye mada bado yupo sahihi.
 
Hizi criteria za ustaharabu ulizoziweka hapa ni viwango tu ambavyo mtu, watu au jamii flani imejiwekea, lakini haimaanishi kwamba ndio viwango vya ustaharabu kwa kila mtu. Unaweza ukawa unakula kuku au mbuzi na ukajiona mstaharabu lakini mwingine akala konokono akajioona mstaharabu. Unaweza ukamshangaa mtu anayekula nyani lakini vile vile mtu mwingine akakushangaa wewe kwa kula ngombe.
Na vilevile kama mdau alivyokuambia hapo juu, ulaji wa chakula/vyakula flani flani kwa mtu au watu flani, unakuwa pia impacted na "mazingira".

Na kwenye issue ya nidhamu, kwa kiasi flani sasa, hasa nikiongelea kwenye jamii yetu ya kitanzania, ustaharabu tulionao, maadili tuliyonayo na nidhamu tulizonazo, vimekuwa vya kinafiki sana. Maadili na nidhamu vinatumika either kwa woga au kama nyenzo ya kufunika maovu yaliyojificha ndani ya mtu au watu, na ndani ya jamii kwa ujumla.

Ni afadhali mtu ale konokono na akiondoka asiseme "kwaheri" kuliko yule anayekula kuku, akiondoka anasema "nakupenda kwaheri", lakini kumbe anakwenda kumchinja binadamu mwenzake.

Tena navyoona, kilichokusukuma ulete hii mada ya kuwasifia watanzania ni wastaharabu, ni "feel good factor" iliyoko kwasasa among wewe na wenzako wengine... Well, utajiju mwenyewe namaanisha nini.
 
Back
Top Bottom